Kamati Kuu ya CCM chini ya Mwenyekiti Samia yaridhia Daniel Chongolo kujiuzulu Ukatibu Mkuu

Kamati Kuu ya CCM chini ya Mwenyekiti Samia yaridhia Daniel Chongolo kujiuzulu Ukatibu Mkuu

Kiswaswadu popote ulipo jiandae,zile kashfa za vitenge na kuchepuka na nke wa tumbili haikuwa bahati mbaya ujue.
 
Kijana kutatuliwa marinda siyo poa, lakini ndiyo hivyo hakuna namna hicho ni kilema cha maisha!
Kumbe na wewe unampata huyo choko Gilbert Masawe, akilewa anazuga kuanguka kifudifudi ili wahuni wamfokoe fresh. Mama yake ameshajaribu kujiua mara mbili kwa fedheha ya ushoga wa mwanawe.
 
Jamaa kishaandika barua ya kujiuzulu na imeletwa kwenu na imepokelewa, mmemkubalia, sasa mnachunguza kitu gani tena?

Hakuna haja ya kupoteza muda kuchunguza yanayojulikana, hivi Kinana akijiuzulu kesho kutwa ( kama tunavyotarajia ) naye atachunguzwa?

Acheni kutupotezea muda, jazeni nafasi zilizoachwa wazi
 
Jamaa kishaandika barua ya kujiuzulu na imeletwa kwenu na imepokelewa , mmemkubalia , sasa mnachunguza kiitu gani tena

Hakuna haja ya kupoteza muda kuchunguza yanayojulikana , hivi Kinana akijiuzulu kesho kutwa ( kama tunavyotarajia ) naye atachunguzwa ?

Acheni kutupotezea muda , jazeni nafasi zilizoachwa wazi
Wanajichekesha
 
Jamaa kishaandika barua ya kujiuzulu na imeletwa kwenu na imepokelewa , mmemkubalia , sasa mnachunguza kiitu gani tena

Hakuna haja ya kupoteza muda kuchunguza yanayojulikana , hivi Kinana akijiuzulu kesho kutwa ( kama tunavyotarajia ) naye atachunguzwa ?

Acheni kutupotezea muda , jazeni nafasi zilizoachwa wazi
Walisema kuna picha zake chafu zimevuja, kumbuka kuchafuana kwa namna hiyo kulifanywa kwa;
  1. Gwajima
  2. Majaliwa
  3. Chongolo
Nani yupo nyuma ya hiyo movement na kwanini?
 
Jamaa kishaandika barua ya kujiuzulu na imeletwa kwenu na imepokelewa , mmemkubalia , sasa mnachunguza kiitu gani tena

Hakuna haja ya kupoteza muda kuchunguza yanayojulikana , hivi Kinana akijiuzulu kesho kutwa ( kama tunavyotarajia ) naye atachunguzwa ?

Acheni kutupotezea muda , jazeni nafasi zilizoachwa wazi
Kwani pia yanakuhusu!
 
Walisema kuna picha zake chafu zimevuja, kumbuka kuchafuana kwa namna hiyo kulifanywa kwa;
  1. Gwajima
  2. Majaliwa
  3. Chongolo
Nani yupo nyuma ya hiyo movement na kwanini?
Mzee baba hakuna connection kama vijana wa mjini wanavyosema?😄
 
Kikao cha Kamati Kuu ya Halmashauri Kuu ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) Taifa kilichofanyika leo tarehe 29 Novemba, 2023 Jijini Dar es salaam na kuongozwa na Mwenyekiti wa Chama hicho, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Samia Suluhu Hassan kimeridhia kujiuzulu kwa aliyekuwa Katibu Mkuu wa Chama hicho Comrade Daniel Chongolo

Taarifa ya Katibu wa Itikadi na Uenezi na Mafunzo, Paul Makonda imeeleza walioteuliwa kugombea nafasi ya Uenyekiti kwa mikoa ya Arusha, Mbeya na Mwanza pamoja na Wilaya za Mpanda na Kusini Unguja.


---
Mwenyekiti wa CCM na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan ameijulisha Halmashauri Kuu ya CCM ya Taifa kupokea barua ya kujiuzulu kwa Katibu Mkuu wa CCM Daniel Chongolo, na ameridhia ombi hilo.

Katibu wa NEC, Itikadi, Uenezi wa CCM Taifa, Paul Makonda amesema hayo leo Jijini Dar es salaam wakati akitoa taarifa kuhusu Kikao cha kawaida cha Halmashauri Kuu ya CCM ya Taifa kilichoketi leo Jijini Dar es salaam chini ya Mwenyekiti na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Samia Suluhu Hassan.

Pamoja na mambo mengine, kikao hicho kimejadili hali ya kisiasa ndani ya Chama na nje ya Chama hicho nchini na kimefanya uteuzi wa mwisho wa Wagombea wa nafasi za uongozi ndani ya Chama kwa ngazi ya Mkoa na Wilaya ili kujaza nafasi zilizoachwa wazi kutokana na sababu mbalimbali ikiwemo kifo na uteuzi wa nafasi nyingine.

Pia soma:
- Katibu Mkuu wa CCM, Daniel Chongolo aandika barua ya kujiuzulu

View attachment 2828888View attachment 2828889

29 November 2023

ZIFAHAMU SABABU KADHAA ZA CCM KUTEUA WAGOMBEA NGAZI ZA WENYEVITI WA MIKOA NA WILAYA

CCM Wilaya ya Kusini Unguja itafanya uchaguzi baada ya kufariki ndugu Mgana Zidi Khamis aliyekuwa Mwenyekiti wa CCM Wilaya ya Kusini Mkoa wa Kusini Unguja.



Kutoka wilaya ya Mpanda habari ni kuwa CCM inategemea kumpata mwenyekiti mpya
ccm-mpanda.jpg
Mwenyekiti CCM Wilaya ya Mpanda marehemu Method Mtepa enzi za uhai wake. Picha na Mtandao

Huku CCM wilaya ya Mpanda
Mwenyekiti wa chama cha mapinduzi Ccm wilaya ya Mpanda Bw. Method Mtepa alifariki dunia tarehe 19/09/2023 baada ya kuugua kwa muda mrefu.

Kanda ya ziwa habari ni kuwa uchaguzi utafanyika baada ya utenguzi wa kiufundi uliofanyika
IMG-20230530-WA0099.jpg

Picha: Mwenyekiti wa CCM mkoa wa Mwanza ndugu Sixbert Jichagu (katikati) akiwa na mkuu wa mkoa CPA Amos Makala (kushoto), wakati mkuu huyo wa mkoa wa Mwanza,alipofika ofisi za CCM kujitambulisha.

Na kwamba uchaguzi wa kumtafuta mwenyekiti wa CCM mkoa wa Mwanza, unakuja baada ya mwenyekiti wa mkoa wa Mwanza ndugu Sixbert Jichagu kuteuliwa kuwa DED mkurugenzi mtendaji wa Halmashauri ya wilaya ya Masasi. Ndugu Sixbert Jichagu alichaguliwa kwa kishindo kikubwa mwezi September 2022 lakini mwenyekiti wa taifa akampangia kituo cha kazi mwaka 2023 kuwa DED halmashauri ya Masasi.

1701301356503.png

Picha: mwenyekiti wa CCM mkoa wa Mbeya ndugu Dr. Stephen Mwakajumilo.

Wakati kwa mkoa wa Mbeya, mwenyekiti wa CCM mkoa wa Mbeya ndugu Dr. Stephen Mwakajumilo aliye mjumbe wa Halmashauri Kuu ya CCM Taifa NEC alileta mtafaruku kwa kuhoji sababu za miradi mingi kusimama baada ya Magufuli kufariki.

Pia mwenyekiti huyo wa CCM mkoa wa Mbeya ndugu Dr. Stephen Mwakajumilo alisema kunahitajika mjadala mpana kuhusu mkataba wa bandari na kuungana mkono wananchi walioomba kupatiwa sababu za, uhalali wa bandari kupewa DP World kwa mkataba ulioolekana kuwa na utata. Msimamo wa ndugu Dr. Stephen Mwakajumilo ukaistua CCM na hata makamu wa rais akasema kuwa wanaCCM hawana utamaduni wa kuhoji waziwazi bila kupitia vikao vya ndani vya CCM kama alivyofanya ndugu Dr. Stephen Mwakajumilo mbele ya vyombo vya habari.

Na mwisho CCM mkoa wa Arusha walimpoteza mwenyekiti wao wa mkoa, Kamishna Mstaafu Zelothe Stephen ambaye alifariki dunia hivi karibuni mwaka 2023.
 
Back
Top Bottom