Kamati kuu ya CCM yakutana Mwanza: Yampongeza Rais Magufuli, Walio hama vyama vya Upinzani waongeza Ruzuku ya chama hadi Bil 13

Kadhalika Dr Magufuli amewapongeza wanaccm kwa kuwapokea wabunge na madiwani waliotokea upinzani kwani ujio wao umeiongezea ruzuku CCM kutoka sh bilioni 12 mwaka 2015/16 hadi zaidi ya sh bilioni 13 mwaka 2018/19
Ueni kabisa vyama vya upinzani ruzuku yote ije kwenu.
 
Mzee Pinda amesema japo katiba hairuhusu lakini kutokana na utendaji uliotukuka wa Rais Magufuli anamuomba Rais Magufuli atawale walau kwa miaka 15 badala ya ile 10 ya kikatiba.......japo anaamini kuwa Dr Magufuli hawezi kukubali.
Khaa Pinda naye anashikwa na ugonjwa gani? Sasa utmuombaje mtu afanye kitu ambacho hakiruhusiwi na katiba na si hivyo tu pia una amini unaemuomba hawezi kukubali
 
Hakika mzee pinda aliyoyasema anafaa kupingezwa!raisi wetu tunaomba ukubali tukuingezee mda ukamilishe miradi yako sisi hatuna shida na wewe katiba ni yetu wqnanchi tunaweza kubadilisha mda wowote

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Pia watuambie,pamoja na ruzuku kuongezeka,wametumia shilingi ngapi kununua viongozi wa kutoka vyama vya upinzani ?
 

Wamewaondoa mafisadi wa zamani wameingia wao mafisadi wapya

Hakuna jipya hapo
 
Mambo ya aibu sana haya;
Mapato ya Chama kwa Mwaka tshs bilioni 50
Mali za Chama tsh bilioni 900
Chama kipo huru kufanya mikutano bila ya bugudha,
Polisi wameagizwa kutii na kufuata maelekezo ya Chama
Serikali ni ya Chama,
Bunge la Chama,
Spika wa Chama,,
Tume ya Chama

Lakini Chama hicho hicho kinaogopa kushiriki Uchaguzi wa haki unaotoa ushindani sawa.
Hizi ni akili au mafanikio ya Sayari ipi na kwa manufaa ya nani?
 
Mzee pinda umenena sawa Rais mwenye uchungu na Nchi aongezewe muda
Nadhani angetakiwa awataje baadhi ya marais ambao hawakuwa na uchungu na nchi
Hii ingetusaidia kuwalinganisha na rais huyu mwenye uchungu kweli kweli na inchi hii
 
Lazima kumpongeza na ni lazima kumshukuru.
,Rais dokta muweza wa yote na asieshindwa kwa lolote.” TEAM KUABUDU/KUSUJUDIA
Huu ni ukichaaa
Kuweni na hofu hata na Shetani kama Mungu hamumuoni
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…