Sasa ni Rasmi.Kamati Kuu ya CHADEMA katika kikao chao leo cha kikatiba kimewapitisha Freeman Mbowe na Cecil Mwambe kugombea nafasi ya Mwenyekiti Taifa katika uchaguzi utakaofanyika Jumatano Desemba 18.
Katika kuonyesha kukomaa kwa Demokrasia ndani ya chama hicho Kamati Kuu iliwahoji wagombea wote bila upendeleo wowote huku Freeman Mbowe akiachia kwa muda nafasi yake ya Uenyekiti na kukaimiwa na Mwenyekiti wa Baraza la Wazee.
Hata hivyo majina yote mawili yatapelekwa katika kikao Cha Baraza Kuu kesho kwa uteuzi wa mwisho na kuidhinishwa rasmi
Freeman Mbowe mwenye ufuasi mkubwa ndani ya chama hicho atakabiliana na mpinzani wake huyo aliyejinasibu kuleta mageuzi makubwa ya kiuongozi na kiutawala ndani ya chama hicho chenye wanachama milioni 6.
Uchaguzi ndani ya chama hicho umegeuka kuwa agenda kuu ya kitaifa kwa sasa kutokana na mvuto wa uchaguzi huo na jinsi unavyoendeshwa kidemokrasia na hivyo kuvuta hisia za watanzania ndani na nje ya nchi.
Kwa siku mbili zilizobaki zitakuwa muhimu kwa wagombea kujinadi na kuomba kura