Kamati Kuu ya CHADEMA, mkiteua wabunge wa Viti Maalumu kuingia Bungeni, mtakuwa mmefanya kosa kubwa sana

Kamati Kuu ya CHADEMA, mkiteua wabunge wa Viti Maalumu kuingia Bungeni, mtakuwa mmefanya kosa kubwa sana

Kususa ni bad idea na wakisusa watasahaulika kabisa kwa nature ya jpm yeye hajali na wataeneza propaganda kuwa hawataki maendeleo ukichangia na vichwa vya watanzania vilivo vichwa panzi
 
Kuwasemea kwa mamlaka ipi? Wakati wizi umebarikiwa na rais, waziri mkuu, spika na majaji.

Hao wabunge watakaokuwa bungeni watakuwa wamepatikana kwa uchaguzi gani (halali) na watakuwa wanalalamika uchaguzi gani (haramu)?

Mpk hapa tayari kuna mgawanyiko ndani ya upinzani. Wapo wanaotaka wabunge waende kwa maslahi mapana ya wao na matumbo yao na jamaa zao. Wapo wanasema wasiende kwa maslahi mapana ya chama. Kazi kwao.

Mamlaka ya walio wapigia kura. Uchaguzi kutokuwa halali hakumaanishi kuwa hawakupigiwa kura ( zilizohesabiwa, zisizohesabiwa na zile zilizohamishiwa upande mwingine). Hiyo peke yake itawapa moral authority ya kuwasemea watanzania na kulalamikia uchaguzi mzima kuwa ungekuwa wa haki wangekuwepo wengi zaidi bungeni. Wanachopasa kukataa ni ubunge wa kuteuliwa maana watakuwa wanakubali mamlaka ya aliowateua na watakuwa wamekubali fadhila.

Mpasuko unazidishwa na wale ambao wanakuwa wepesi kuwaita wenzao wasaliti, wachumia tumbo na wenye maslahi binafsi. Hakuna mtu mwenye hati miliki ya maslahi ya chama. Mawazo ya pande zote yanatakiwa kuheshimiwa, kuthaminiwa na kujadiliwa kwa uhuru kabisa na chama.

Amandla...
 
Una maoni mazuri sana, wakibanwa kwenye hoja wanakimbilia mambo ya maslahi binafsi ili kuonesha mnaopinga mgomo ni wanufaika, kumbe hamna kitu.
 
Mkuu kususa kutawaumiza Sana. Watakosa fedha za kuendeshea serikali yao.

Zanzibar hawakupata taabu hii kwasabb walibebwa na bara. Halafu Zanzibar siyo nchi kwa mujibu wa katiba yetu. Subiri mbinyo atakaoupata Magufuli na CCM. Wataomba poo.

Unadhani Ile hand shake ya Uhuru na Odinga ilikuja kwa hiari ya Uhuru?

Watakosaje pesa za kuendesha serikali? Kama unategemea serikali za kigeni kuiwekea vikwazo vya kiuchumi unajidanganya. Wataishia kutoa ujumbe wa kutoridhishwa na jinsi uchaguzi ulivyofanyika basi. Au unategemea wafuasi wa vyama vya upinzani watakataa kulipa kodi?

Amandla...
 
Njia pekee ya kuleta significant impact ni maandamano, tatizo hatuiwezi, nyingine zote ni kupoteza muda tu.
Wengi wetu tunaangalia tuu, upande wa CCM, sisi hatujaweza kuimarisha vyama vyetu, na hili ni la lazima sana kabla ya kutaka mengine. Mfano : Wakati nipo Hai katika Uchaguzi mkuu, wajumbe ambao watasimamia vituo vya kupiga kura,

1) Hawakutosha.
2) Na waliokubali walitaka walipwe na wengine kuodoka vituo.
3) Na mkubwa baada ya kuona maji yanazidi unga hata kura hakupiga.
4) Poor organisation in the Party members from rank to file.
 
Ni ushauri mzuri na umekuja kwa wakati hata mahesabu ya CCM ni kwamba mshindwe kwenye majimbo ili maateenheid vitu vya kugawiwa kwa ajiri ya kulinda misaada CHADEMA Meijer mkaingia kwenye mtegi wa hivo. Hata mbunge huyo mmoja na madiwani endapo hawatajitoa wafukuzeni kwenye chama. Demokrasia ni muhimu zaidi ya hao mapndikizi kwenye chama chenu. Hakuna hata mmoja aliyeshinda kwakuwa hakuna kura zilizohesabiwa matokeo yaliandaliwa kabla hata ya kupiga kura ndo maana kura za rais zilijulikana tangu tarehe 27 hadi Tundu Lissu akasema anataarifa NEC wamempa Rais kura milioni 12 wakala kutangaza hizo hizo
 
Ndugu yangu unaongea vitu gani?
Chama kitajiendesha vipi?
Yale magari mafuta yatapatikana vipi?

Umewaza kuhusu pesa za kuwalipa waajiriwa wa chama?

Au lengo lako chama kife au sio
 
Chadema, kujiimarisha na kujiporomosha vyote viko mikononi mwenu.
Bora kufa kishujaa kuliko kuishi ukiwa unamuabudu, unasujudu, na kumsifu nyapara jiwe

Then unakuwa umepata faida gani?
Ushujaa huu huko kwa kukaa nyuma ya keyboard tu
 
Kuna tetesi kuwa kikao kinachoendelea kati ya Kamati Kuu ya Chadema na Tume ya uchaguzi, Chadema wamepewa nafasi 22 za viti maalumu.

Kitendo cha Chadema kukubali kupeleka hayo majina kimsingi ni kukubaliana na mchakato mzima wa Tume, na itakuwa hadaa kwa wanachama na jumuiya za kimataifa kuwa wameibiwa kura.

Chadema ijue huo ni mtego wa fisi kuonyeshwa kipande cha mfupa, mkikubali mjue mmekwisha, dhihaka mtakazopata hamtaweza kuzijibu, ile hoja ya kuwa chama cha ruzuku itathibitika wazi.

Kutoa hayo majina ni kuwadhulumu wagombea waliojitoa kwa damu kupigania haki majimboni ambao baadhi yao wamepoteza viungo wengine wamepoteza uhai na baadhi hadi leo bado wapo magerezani.

Kamati kuu haitamtendea haki mgombea urais Tundu Lissu ambaye hadi sasa amekimbilia ubalozi wa Ujerumani kunusuru maisha yake.

Vile vile haitawatendea haki wapenzi, wanaharakati na wafuasi wa mitandaoni wanaohatarisha maisha yao kuitetea CHADEMA.

Kwa hadhi ya Chama kilipofikia na kwa gharama mliyopoteza kukijenga haiwezi kulipwa kwa kupewa ruzuku ya viti maalumu 22 tena na watu waliowadhulumu ushindi wenu.
 
Hapo ndipo mnyukano utakapo tokea, maana wapo watakao kataa wasipeleke na pia wapo watakao ona wapeleke kwasababu hata wasipo peleka tayari maamuzi yalisha fanyika na UCHAGUZI UMEISHA×3
 
Kuna mnyukano huko wa hatari kina Matiko, Mdee, Bulaya, Magelesi and the likes wameunda women wing kushinikiza kamati kuu kuwaruhusu wateuliwe na kushiriki bingeni kama viti maalum, vinginevo wakiwahama wasilalamike.
Ulishiriki hicho kikao?
 
CCM baada ya kukwapua bakuli zima la nyama..sasa wanawatupia CDM kipande kimoja cha nyama kuwapima imani.!!
Na hicho kipande kimoja ccm wanatambua kwamba hakito watosheleza, hivyo mpango kazi hapo ni kuwagombanisha kwa kipande kimoja cha nyama
 
Back
Top Bottom