Kamati Kuu ya CHADEMA yawakuta na hatia Kubenea na Komu. Wavuliwa nyadhifa zote chamani na kupewa onyo

chama Ni watu wastalabu wakikoseana huombana misamaha na yanaisha hongereni sana kamati kuu kwa maamzi yenye kujenga
 
Ni hatua stahiki kwa kila mkosaji. Pia hongereni Kubenea na Komu kwa ukomavu wa kisiasa.
 
Kwani mbowe n mwenyekiti wa kwanza wa chadema? Na vipi kuhusu Ccm uenyekiti wake form anaruhusiwa kuchukua mtu moja
 
chadema buana,, wasingeweza kufukuza.. ruzuku ipungue hahahah.
Wangefukuzwa tungesema ni hasara kwa kurudia uchaguzi ni bora kuwaacha wamalize kipindi chao cha ubunge ambacho ni muda mfupi umebaki then wanatoswa awamu ijayo. Me nadhan watakuwa na wakati mgumu kwao na ni bora wangefukuzwa wangekuwa na la kusema
 
We punguani ndezi mkubwa! watu wamepatikana na hatia lakini wameomba radhi shida yako wafukuzwe kwani wako kwenye chama chako cha utekaji? kafie mbele bwana!
Hao waliokuwa wanapanga jinai sio watekaji!
 
C.I.A wa chadema vipi baada ya hapo mda wa ruzuku ukiisha bado tutakuwa nao Said na Komu.

Je baada ya hapo nani atafuata?





"Ngoja nivae uhusika wa zitto"

Kamuulize aliyewatuma kuwa baada ya hawa maspy wao kuwa exposed watamtumia nani kukivuruga chama..
 
Yericko Nyerere uko wapi? Jamaa wamesamehewa yameisha!! Pole mkuu na mapovu yako ya jana!
 
Sasa mbona Kubenea amevaa miwani ya jua (gugoz) wakati anaongea na wanahabari kule uani ilhali kuna kivuli cha maturubai?
 
Habari wanaJF!

Katika pitapita zangu humu jamvini nimeshuhudia kuna kundi la watu ambalo halijafurahishwa kabisa na kitendo cha kamati kuu ya CHADEMA cha kutowafukuza makada wake Ndugu Kubenea na Komu. Wengine wameishia kuyakejeli maamuzi hayo ya kamati kuu wakidai hawajafukuzwa sababu wakifanya hivyo watakosa ruzuku madai ambayo bado sina ushahidi nayo.

Je unahisi ni sababu zipi zinapelekea kundi hili kutopendezwa na maamuzi hayo ya kamati kuu ya CHADEMA?

NB: Nimeliita kundi la upande wa pili nikiwa na maana kwamba ni kundi lenye mtizamo tofauti!
 
CHADEMA wamethamini matakwa ya wapiga kura na kodi za wananchi ambazo zingitumika kurudia uchaguzi endapo wabunge waliochaguliwa na wananchi wangevuliwa ubunge wao.
 
Nimeisikiliza clip ya akina Kubenea wakijadili jinsi ya kummliza Boniface Jacob, wanadai akishaondoka Boniface Jacob itakuwa kazi rahisi kumng'oa Mbowe kwenye uenyekiti
Aisee ni hatari sana ,kama wangefanikisha adhimu yao bila shaka ingesingiziwa serikali kwamba imehusika .
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…