Kamati Kuu ya CHADEMA yawakuta na hatia Kubenea na Komu. Wavuliwa nyadhifa zote chamani na kupewa onyo

Kamati Kuu ya CHADEMA yawakuta na hatia Kubenea na Komu. Wavuliwa nyadhifa zote chamani na kupewa onyo

Yericko naona utakuwa na furaha sasa ni muda wako kuanza kunyemelea nafasi ya Kubenea huenda ikakufaa.
 
Yericko Nyerere ataiweka wapi sura yake,alikurupuka?
Ana uhuru wa kutoa maoni. Ila siyo kila maoni yanafaa kuchukuliwa na kufanyiwa kazi. Mengine yanasikilizwa na kuchambuliwa na kupimwa kwanza kabla ya kuchukua uamuzi. Maoni yake kutofanyiwa kazi hakomi kuwa mwanachadema na wala hana sababu ya kuacha kuendelea kukipigania chama.
 
Hahahaha habari nzuri Sana hii kwetu Wana CCM ..Vita ya panzi =furaha ya kunguru
 
Ahsante mnyika na kamati kuu kwa ujumla kwa hatua kama hiyo itayoendelea kutunza heshima ya chama chetu.
 
Hawa wahuni sijui ni kwa nini wameachwa na kamati kuu waendelee kuwa kirusi lakini kubwa zaidi ikiwa walijituma hii si jinai na wamekiri? Iweje serikali ya ccm isiwachukulie hatua?
 
Ukiona sarakasi kama hizo zinatukia ujue uchaguzi ndani yacdm umewadia..... hususan ngazi ya mwenye kiti chake milele.
 
Mnyika:
Wahusika walifika mbele ya Kamati Kuu na kujieleza. Walikiri kuwa sauti zilizosikika ni zao na Kamati Kuu iliwahoji kwa muda mrefu.

Kamati Kuu ya Chama imefikia maamuzi kuhusiana na hili. Wamekutwa na hatia ya ukiukwaji wa Katiba ya Chama na Taratibu zake.

Wamepewa Onyo na kutakiwa kuandika barua ya kuomba radhi kwa chama na wanaotajwa kwenye Clip iliyosambaa.

Kamati Kuu imeamua kuwaweka kwenye kipindi cha uangalizi wa mwaka mmoja juu ya mienendo yao.

CHADEMA imeamua kuwavua nafasi zao zote za uongozi ndani ya chama na kubaki na nafasi ya uwakilishi wa wananchi tu (Ubunge).

Kubenea:
Nachukua nafasi hii kusema kuwa yaliyotokea ilikuwa bahati mbaya sana na hatukuwa na nia ovu yoyote. Naomba radhi sana kwa wanachama na watanzania wote kwa kilichotokea

Komu:
Nachukua nafasi hii kukishukuru chama kwa kulipa uzito suala hili; nakubali kuwa chama ni kikubwa kuliko sisi wote. Chama kina mikono yake. Baada ya Kamati Kuu kukaa na kutafakari yote yaliyotokea, kimeelekeza kama ilivyoazimia! Nitayatekeleza yote yaliyoelekezwa mara moja. Naomba radhi kwa chama, wanachama na watanzania kwa ujumla.

Mazungumzo yale yalikuwa ya faragha lakini teknolojia ilinizidi ujanja; nawaomba radhi Mh. Mbowe na Meya Boniface kwa kilichotokea. Tunataka tuanze upya.

MASWALI:​
Kwanini kila inapofikia karibu na Uchaguzi Mkuu huwa chama chenu kinaibuka na matatizo kuhusu nafasi ya Uenyekiti?

Kubenea, kwanini uliandika suala la Ben Saanane kwenye gazeti lako kwa mtindo ule?

Kubenea na Komu, wakati chama chenu kina changamoto tunazoziona; mmepata wapi ujasiri wa kupanga haya dhidi ya wenzenu ndani ya chama?

Kama wabunge walikuwa wakipanga kumhujumu Mwenyekiti wao na Meya wao, chama kinajipangaje juu ya hili?

Kubenea na Komu, wakati mnapanga haya - mlikuwa mmelewa?

Je, Mbowe kama mhusika kwenye clip alipisha wakati wa mjadala?

Mnyika, kuna chuki kati ya Jacob na Kubenea?

Kubenea, kuna tetesi zinazoashiria una mpango wa kuhamia CCM; haiwezekani kuwa hii clip inaashiria kuwa uko njiani kuhama?

MAJIBU:​

Komu: Hakuna shida kubwa iliyoonekana kwenye Kamati Kuu. Suala la kudhuru ni suala la jinai. Kilichopelekea kuonekana tuna mpango wa kumdhuru mtu ni kwa sababu clip ilitoka kwa bahati mbaya. Mtu angesikiliza maongezi yote angeona kuwa hakukuwa na dhamira ya kumdhuru mtu. Wewe ukigonga gari nyuma, ikawa breki ndizo zilikatika, huwezi kukwepa kuwa ni kosa.

Komu: Hatukuwa na dhamira ya kumdhuru mtu. Tulikuwa very sober, ni kuwa tulikuwa tunajadili hoja flani tuliyokutana nayo na ndio kilichotufikisha kwenye maongezi yale.

Komu: Suala la ruzuku nilishaliongelea mara nyingi huko nyuma; tunaye auditor na hata zipo ripoti za CAG. Nilisema, kama kuna mtu ana wasiwasi wa matumizi wa fedha za ruzuku (ambazo ni za umma), basi hiyo ndio ilikuwa hoja yetu (kuwa ungefanywa uhakiki).

Kubenea: Kuhusu suala la Ben Saanane - nimesikitika, mimi ni mmiliki wa gazeti. Aga Khan hawezi ulizwa kuhusu suala lililoandikwa na gazeti la Mwananchi. Mimi ni mmiliki, japo ni mwandishi. MwanaHALISI ina wahariri wake na wala sikuandika mimi story hiyo. MwanaHALISI inafuata misingi ya uandishi na ni gazeti 'serious'. Suala hilo waulizwe wahariri wa gazeti hilo na sihusiki na gazeti hilo.

Kubenea: Wapo vijana flani, wapo kwenye mitandao ya kijamaa ambao wanatumika kukichafua chama.

Kubenea: Kuhusu kuhama chama - Mimi ni imara sana! Ningekuwa legelege nisingeenda Kamati Kuu, walioondoka hata hawakuitwa Kamati Kuu, walikimbia wenyewe. Wambieni CCM - Sifanani nao!

Kubenea: Kuhusu Meya Jacob - Mimi ni Mbunge wa Ubungo, Jacob ni Meya wa Ubungo. Hatuna mgogoro na Jacob, tunafanya kazi pamoja na kushirikiana bila shida yoyote.

Kubenea: Meya Jacob ni miongoni mwa marafiki zangu wa karibu

Mnyika: Nimekuwepo kwenye chama tangu 2004, nimeziona chaguzi kadhaa ndani ya chama; ningeomba waandishi mfanye uchunguzi juu ya tuhuma za utovu wa nidhamu - hayajajadiliwa nyakati za uchaguzi tu. Anatoa maelezo kufafanua... Jambo hili lisionekane linatokea nyakati za uchaguzi. Katika vyama vingi vya siasa, tuhuma zinapotokea jambo la kutazama ni maamuzi ya chama yanapotokea mambo kama hayo.

Mnyika: Ukubwa ni Jalala, kitendo cha Mbowe kuwa kiongozi wetu, yeye ndiye mashambulizi mengi huelekezwa kwake. Ndo maana hata CCM wakifanya mashambulizi kwa CHADEMA humlenga Mwenyekiti wa chama. Wakati wote tunakuwa mstari wa mbele kama wanachama kumlinda Mwenyekiti wetu kwakuwa tunaujua mchango wake kwa chama katika safari ya kuiondoa CCM Madarakani.

Mnyika: Ile clip iliyosambaa, Mwenyekiti hakuwa mlalamikiwa, mlalamikaji wala mtuhumiwa. Hivyo, alishiriki kikao cha chama. Taarifa ya wabunge hawa iliwasilishwa na Katibu Mkuu wa chama, sitaingia kwa undani juu ya kilichotokea Kamati Kuu. Mwenyekiti hakuongoza mwenendo wa mahojiano, niliongoza mimi kwakuwa sisi ndio tulikuwa na hoja hii.

Mnyika: Kamati Kuu ilijiridhisha kuwa waheshimiwa walifanya makosa na ndio maana imechukua maamuzi haya. Wameandika barua za kuomba radhi na watakuwa kwenye uangalizi juu ya mienendo yao kwa miezi 12. Ni funzo kwa wengine kuwa wazingatie Katiba na Kanuni za Maadili za chama; yeyote atakayekiuka atawajibishwa.

Soma=>Wabunge Saed Kubenea (Ubungo) na Anthony Komu (Moshi Vijijini), wahojiwa na Kamati Kuu ya CHADEMA - JamiiForums
Wamepewa onyo kali baada ya kutaka bi kilembwe aachie madaraka chamani..
Maskini akina mtolewa hawajui kuwa chadema ni saccos ya wachaga..
Wasijaribu tena kumtaka bi kilembwe aachie ngazi yatawakuta ya zitto na chacha wangwe
 
Waombe radhi kwa kosa gani?

Kutoa maoni yao kwamba chadema ipate mwenyekiti mwingine ni kosa?

Kwa nini hawajifunzi kwa ccm iliyobadilisha mwenyekiti kutoka Nyerere, Mwinyi ,Mkapa ,Kikwete na sasa Magufuli?

Kwa hiyo Bavicha kutwa wanalilia Uhuru wa kutoa maoni kutoka kwa Magufuli lakini hawataki Uhuru wa kutoa maoni kutoka kwa Mbowe??
Mkuu lazma waombe radhi kwani wao hawajui kuwa kile ni chama cha mbowe na baba yake Bob makani?
Wataanzaje kutaka mwenyekiti abadilishwe kwenye chama cha watu?
 
Nilitaka chadema iwatimue wote hata wakicheza chikichichikichi emhh! fyekelea mbali.
 
Back
Top Bottom