Kamati Kuu ya CHADEMA yawakuta na hatia Kubenea na Komu. Wavuliwa nyadhifa zote chamani na kupewa onyo

CCM hawatakubaliana na uamuzi uliofikiwa na Chadema hivyo wataelekeza makombora yao yakichina kwa Mbowe, tusubiri tutayaona yakipita.
 
Walioomba radhi wameomba radhi, tatitzo lako ni nini? au kwa sababu ulichotarajia hakikutokea? CHADEMA ijifunze kwa CCM? haya, Nyerere alikalia uenyekiti wa chama kwa miaka mingapi? anzia TANU halafu njoo CCM. lakini pia, uenyekiti wa CCM unaendana na urais. Mwenyekiti wa CHADEMA siyo rais wa nchi. Mwenyekiti wa CCM anaondoka ili kumpa nafasi rais ashike kofia zote mbili. siyo kwa kulazimishwa na kanuni bali ni utaratibu au mila za CCM tu. katiba ya CHADEMA iko wazi kabisa. NINI KINACHOKUWASHA?
 
Mkuu wako chini ya uangalizi wa karibu kwa mwaka mmoja.
 
Chadema imejaa udikteta tupu
 
Nilisema cdm imekaa kibiashara hawawezi thubutu kufukuza mbunge na kupunguza ruzuku ya chama. Hao wanaotoka ingewezeka kuwafunga mnyororo wangefanya hivyo.
Je kuhusu huyo mashavu kubwa waliyekua wanamjadili ni kweli hafai? Huyo jacob ni wale watu kwa kuzaliwa wakorofi wabishi na wabinafsi. Hafai kuongoza chochote. Ni kama lissu ila lissu msomi na jacob ni mjinga tu. Watu wa aina hiyo kwenye ubishi hata ukikubaliana nao wataendelea kukupinga hivyo kupinga hata kile walichokua wanadai ndio sawa.
 
Huku ni kuminya Uhuru wa kutoa maoni .

Haiwezekani kila anayekuja na mawazo mbadala anakumbana na adhabu kali namna hii.

Watu wote wataogopa kitakachobaki ni ndiyo mzee kwa kila kitu.

Mbowe acha udikteta
 
Uongozi wenye Busala ndo unaohitajika Hususa kweny vyama vyetu vya siasa .....na pia Tukumbuke teknologia ni kubwa kuliko tunavyo fikilia inaweza kukutia hatiani wakati wowote Tujiadhali kwa kauli zetu na mahara tuwapo....
 
Ni maamuzi ambayo wenye busara WOTE duniani tuliyategemea. Wapo watakaoponda kwa sababu ya itikadi na walichotumwa na waajiri wao kuja kusema humu. Tusiofuata upepo na tunaojua gharama ya kujenga upinzani madhubuti tunasema mmefanya jambo kubwa. Ccm ni Chama kikubwa nchini na ni Chama Tawala kinachojichotea fedha serikalini bila kuhojiwa. Lakini mbali ya nafasi hiyo hawakuwahi kuthubutu kuwafukuza hata WATUHUMIWA maarufu wa ukwapuaji kina mzee Chenge , mama Tibaijuka, Ngeleja na hata huyu anayepiga marufuku watu kujadili mtanzania mwenzao kupotea (LUGOLA) ambaye aliwahi kufikishwa kabisa mahakamani. Mmefanya vema kwa faida ya wapenda demokrasia. Hata baba alimsamehe mwana mpotevu aliyetapanya mgao wake kwa ukahaba.
 
Pole ulivyotegemea imekuwa ndivyo sivyo.
 
Hao wote wa ccm unaodai wamebadilishana uenyekiti wamewahi kuwa marais wa nchi hii, sasa unataka Mbowe aachie wakati bado hajawa rais??
 
Isije ikawa akina Komu na Kubenea wameomba radhi ili waandae mazingira yakuhamia kule CCM,hao waangalizi wawe makini hasa na teknolojia yao amabayo Komu kasema imewazidi ujanja.
 
Said Kubenea na Antony Komu Wamekiri kuwa ile audio ilikuwa kweli na mpango wao ni sawa.
Je Wangefanikiwa Je Tungesema ni serikali.?Je chadema wangekuja hadharani kuwaammbia wananchi kuwa ni michezo yao ndani ya chama ya siku Nyingi.?

Tuzidi Kumwombea Jpm Atunze amani ya nchi na Taifa.
Kuletwa kwa Jpm Ndani ya Taasisi ya Urais Ni Makusudi ya Mwenyezi Mungu.
 
Huku ni kuminya Uhuru wa kutoa maoni .

Haiwezekani kila anayekuja na mawazo mbadala anakumbana na adhabu kali namna hii.

Watu wote wataogopa kitakachobaki ni ndiyo mzee kwa kila kitu.

Mbowe acha udikteta
Uhuru una mipaka, naona umeumia sana kwa kutofukuzwa pole.
 
yaani sikujua kama hawa jamaa wana michezo hiyo, kumbe ben nae sasa tuwatuhum wao
 
Acha hizo! Mungu hawezi kuleta dictator!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…