Kamati Kuu ya CHADEMA yawavua nyadhifa na uanachama Halima Mdee na wenzake 18 walioapishwa kuwa Wabunge wa Viti Maalum

Kamati Kuu ya CHADEMA yawavua nyadhifa na uanachama Halima Mdee na wenzake 18 walioapishwa kuwa Wabunge wa Viti Maalum

Again CDM wanakubali kupoteza msingi wa kwanza wa chama (watu) kama ilivyokuwa kwa wakina Zitto,Prof Kitila,Dr.Slaa na Prof.Mashinji kwa kutaja wachache.
Hivi hawaoni CCM ilivyodili na wakina Nape,Mzee Makamba na Katibu Kinana? Kwanini hawajifunzi jinsi ya kutatua matatizo yao kwa wakati (Taking all time they needed) kulikuwa na haraka gani ya kufanya maamuzi makubwa kama haya ndani ya masaa 72 ?
Kwanini kila uchaguzi au kwenye michakato ya uongozi ndani ya Chadema inaondoka na watu ?

CDM ili ifike mbali ni lazima ijijengee uwezo wa kumudu,kutunza na kukaa na watu/wanachama wake wa aina zote kwa maana Kuna msemo wa pwani usemao “Mtu si mbwa” leo hii wanapoteza wanachama 19 ambao wengi wao wanaushawishi mkubwa kwenye Ngome ya wanawake ya CDM na mbaya zaidi wanawapoteza kwa mtego wa kawaida sana.

CDM inacheza ngoma ya vyama vingine na kusahau shughuli yao ! Tokea M4C izimike na Dr.Slaa hakuna jambo la kimkakati la kujenga chama au kukuza chama limefanyika zaidi CDM imekuwa iki-REACT kutokana na matukio na matendo ya CCM pamoja na Serikali badala ya ku-ACT katika mipango na mikakati yake .

Itachukua muda sana kujenga watu wengine kulikoni ingepatikana suluhu ya kunufaisha chama zaidi.
Wamefanya makosa,wanaitwa hawaendi kwa dharau!Watu wa hivyo ni kheri kuwafukuza maana wakishajiona wana mapembe kuliko chama ni hatari!
 
Wanafukuzwa chadema,wanaoumia ni CCM,kaaaz kweli kweli mataga.
Unanijua mimi? Watu wa aina yako wanakimbilia kuegeneralize wasiliopenda au wanalopenda kusikia tu ni mbugila kweli kweli. Kila CHADEMA inapufukuza au inapokimbiwa na wanachama hudai yenyewe iko iko imara wakati namba zinaonyesha wazi kuwa inaelekewa kwenye oblivion. Mimi nilikuwa mwana CHADEMA thabiti sana kati ya 2007 hadi 2015; niliondoka mwaka 2016 ingawa bado nina kadi.
 
NEC taasisi nyeti imefikia hatua ya kugushi? Kwani shida nini, tuliaaambia hivo viti wawape polisi
Tume imeundwa na timu ya welevu na wasomi tatizo ni hao vilaza wa CDM,,, huu ni mpasuko mkubwa ndani ya CDM na tulisema kuwa mwisho wa upinzani umewasili,,, wanadai waliibiwa kura bila kupeleka vidhibiti hata kwa Armterdam wao ni kama Trump tuuu, Polisi na jesho walihusika kuangalia uchaguzi unapita kwa amani baada ya vilaza kuwaambia wavuta bangi wao ati walinde kura mita 200 hiyo ndiyo sababu ya polisi na jeshi kutumika,,, hamsemi vilaza.
CDM,, marehemu kwani wadada wana mengi sana na mjue pussy power and no man continues to argue in front of a naked woman!!!!!
 
1.Wakienda magakamani kwa ajili ya judicial review wanashinda asubuhi na mapema

2.Ukisoma vizuri theory ya aud alteram partem suala la kupewa muda wa kutosha wa kuandaa utetezi pale unapofikishwa kwenye judicial au quasi judicial ndio msingi wa hiyo rule....hivyo kitendo cha mabinti hao kuimba haki hiyo ya msingi tena kwa mwaandishi na wao wakaamua ku mute bila hata ya kuwajibu sababu za kufanyika hiyo haki ambayo kimsingi hawakupaswa hata kuimba bali wangepewa...lakini kinyume chake wakajisikilizisha na kuandaa hukumu in absentia ambayo kimsingi kuna baadhi ya mojito ilichatoa majibu kwenye mitandao hayo maamuzi yatafyekelewa mbali na mahakama asubuhi na mapema
 
Viongozi wao wanasoma sana mitandao badala ya kufanyia SWOT analysis maamuzi yao.

Tatizo la CDM kwa sasa ni Lissu
Ile ya kusindikizwa na mabalozi watatu ni jambo la kibabe sana.Mlishindwaje kumzuia?.Ona sasa.Hahahahaaaa
 
Eti NEC waghushi, wajumbe wa kamati kuu waarifiwe, waende Dodoma, wakubali kuapishwa kuwa wabunge!! Inaingia akilini kabisaaa! ????? Kweli nyumbu ni nyumbu tu!
Hayo ni mawazo ya vilaza wa CDM hawioni NEC ivyojaa wasomi wabobezi siyo vilaza na msubiri tu hapo kuna vitu vitatoka kwa hao warembo subirini watamwaga radhi
 
1.Wakienda magakamani kwa ajili ya judicial review wanashinda asubuhi na mapema

2.Ukisoma vizuri theory ya aud alteram partem suala la kupewa muda wa kutosha wa kuandaa utetezi pale unapofikishwa kwenye judicial au quasi judicial ndio msingi wa hiyo rule....hivyo kitendo cha mabinti hao kuimba haki hiyo ya msingi tena kwa mwaandishi na wao wakaamua ku mute bila hata ya kuwajibu sababu za kufanyika hiyo haki ambayo kimsingi hawakupaswa hata kuimba bali wangepewa...lakini kinyume chake wakajisikilizisha na kuandaa hukumu in absentia ambayo kimsingi kuna baadhi ya mojito ilichatoa majibu kwenye mitandao hayo maamuzi yatafyekelewa mbali na mahakama asubuhi na mapema
Chama cha siasa kina autonomy ya kuendesha mambo kwa katiba ya chama.

Hapo cha kuangaliwa ni katiba ya chama.

Kwa mfano tu, katiba ya chama ikisema Mwenyekiti anaweza kumfukuza mwanachama yeyote bila mjadala, na wanachama wakakubali hilo na kujiunga na chama, siku mwenyekiti akimfukuza mtu uanachama, bila mjadala, mwanachama hatakiwi kulalamika mahakamani.

Maana aliikubali katiba ya chama.

Sasa katiba ya chama inasemaje?
 
Again CDM wanakubali kupoteza msingi wa kwanza wa chama (watu) kama ilivyokuwa kwa wakina Zitto,Prof Kitila,Dr.Slaa na Prof.Mashinji kwa kutaja wachache.
Hivi hawaoni CCM ilivyodili na wakina Nape,Mzee Makamba na Katibu Kinana? Kwanini hawajifunzi jinsi ya kutatua matatizo yao kwa wakati (Taking all time they needed) kulikuwa na haraka gani ya kufanya maamuzi makubwa kama haya ndani ya masaa 72 ?
Kwanini kila uchaguzi au kwenye michakato ya uongozi ndani ya Chadema inaondoka na watu ?

CDM ili ifike mbali ni lazima ijijengee uwezo wa kumudu,kutunza na kukaa na watu/wanachama wake wa aina zote kwa maana Kuna msemo wa pwani usemao “Mtu si mbwa” leo hii wanapoteza wanachama 19 ambao wengi wao wanaushawishi mkubwa kwenye Ngome ya wanawake ya CDM na mbaya zaidi wanawapoteza kwa mtego wa kawaida sana.

CDM inacheza ngoma ya vyama vingine na kusahau shughuli yao ! Tokea M4C izimike na Dr.Slaa hakuna jambo la kimkakati la kujenga chama au kukuza chama limefanyika zaidi CDM imekuwa iki-REACT kutokana na matukio na matendo ya CCM pamoja na Serikali badala ya ku-ACT katika mipango na mikakati yake .

Itachukua muda sana kujenga watu wengine kulikoni ingepatikana suluhu ya kunufaisha chama zaidi.
Kukua kwa CHADEMA hakuhitaji mikakati kihivyooooo.Kinakua automatically kulingana na watu kutoridhishwa na mwenendo wa serikali iliyopo madarakani.Hivyo kukua kwa CHADEMA ni kugusa tu.
 
Mwenyekiti wa CHADEMA Taifa, Freeman Mbowe atazungumza na Umma wa Watanzania kupitia mkutano na waandishi wa habari, leo Novemba 27, 2020, kuanzia saa 3.00 (usiku huu), kuhusu maamuzi ya Kikao cha Kamati Kuu ya Chama

Vyombo vya habari vya Kitaifa na Kimataifa vimealikwa.

Stay Tuned for Updates

======================
Waandishi wanaanza kuwasili ukumbini wanaoingia wanatakiwa kuwa vitambulisho.
Muda wowote kuanzia Viongozi wa Chadema wataingia ukumbini kuongea na waandishi wa habari.
22:08
Bado Viongozi wa Chadema hawajafika ukumbini
Mkutano huo utakuwa live kupitia
Tayari Mwenyekiti wa CHADEMA Taifa Freeman Mbowe ameshafika ukumbini
Tunawashukuru Watanzania wengi ambao wanafuatilia kikao maalum cha ajenda moja ya kujadili, kushauriana na kutafakari juu ya wanachama wetu 19 waliokwenda kuapa kuwa wabunge wa viti maalum- Freeman Mbowe
"Sisi kama kamati kuu ya chama kikuu cha upinzani, tumeona na kuridhishwa kuna ukiukwaji mkubwa umekiukwa katika mchakato mzima wa uchaguzi na huu wa viti maalum. Tumejiridhisha ndani ya chama kuhusu mapungufu kadhaa yaliyofanyika-; Mbowe
“Chama chetu hakijateuwa Wabunge wa Viti Maalum lakini tunaona wapo Bungeni wanaapishwa”Mbowe
Tangu nchi hii ipate uhuru hatujawai kuona Mbunge/Wabunge wakiapishwa garage, mambo ya kihuni kabisa haya..." Mbowe
“Hiki chama kinaongozwa na principles bila kujali maumivu makubwa tuliyopitia chama chetu kitafuata utaratibu siku zote, kwahiyo kamati kuu imewavua nafasi zao za uongozi viongozi wote waliokua na nafasi katika mabaraza ya chama.”
@freemanmbowetz

“Kamati Kuu imewavua Uongozi wale wote ambao walikuwa Viongozi kwenye Mabaraza kati ya hao Dada zetu 19 sitaki kupoteza muda kuwataja majina, kwahiyo kuanzia sasa hawapaswi kushughulika na lolote kama Viongozi na tumeelekeza nafasi zao zizibwe haraka” -MBOWE

"Ili kanuni ambayo Spika ametumia iweze kufanya kazi kuapisha wabunge wetu. Kwanza wangestahili kubadilisha Katiba iruhusu wabunge kuapishwa nje ya utaratibu ambao ni ndani ya Bunge" -

Nusrate Hanje Katibu wa Bavicha amefungwa jela siku 133 kwa makosa yenye dhamana, hawa Watesi wetu wanakwenda kumtoa saa moja usiku akaape.”

”Chama chetu hakijateua Wabunge wa Viti Maalum tunaona tu Watu wetu wanaapishwa na hatuna taarifa, hatujapeleka majina, fomu za Tume zipo ofisini Mama zetu hawa Dada zetu hawajajaza fomu, ila tunaona tu wanaaapishwa”-

"Sisi kama chama cha siasa, hii 'process' yote hatuijui, tunaona tu wabunge wetu wanaapishwa. Chama chetu hakijateua wabunge wa viti maalum" -

"Wabunge hawa 19, mama zangu na dada zangu wameapishwa kiapo batili kwani Katiba inasema waapishwe mbele ya Bunge. Sasa kanuni zimebadilishwa ili kumruhusu Spika kumwapisha popote hata eneo la gereji-

“Tangu Nchi yetu imeanza hatujawahi kuona Wabunge wanaapishwa Gereji, lakini Dada zetu na Mama zetu hawa wameapishwa nje ya Bunge, wakati Katiba inataka waapishwe ndani ya Bunge, kwahiyo wamekula kiapo batili”
Mwenyekiti wa CHADEMA Freeman Mbowe amesema Kamati Kuu ya Chama hicho iliyoketi leo Nov 27,2020 imeazimia kuwavua uanachama Halima Mdee na wenzake 18 waliopishwa juzi kuwa Wabunge Viti Maalum “wamekinajisi Chama na wamekataa kuja kwenye Kamati Kuu”

”Chama chetu hakijateua Wabunge wa Viti Maalum tunaona tu Watu wetu wanaapishwa na hatuna taarifa, hatujapeleka majina, fomu za Tume zipo ofisini Mama zetu hawa Dada zetu hawajajaza fomu, ila tunaona tu wanaapishwa”

“Kamati Kuu imewavua Uongozi wale wote ambao walikuwa Viongozi kwenye Mabaraza kati ya hao Dada zetu 19 sitaki kupoteza muda kuwataja majina, kwahiyo kuanzia sasa hawapaswi kushughulika na lolote kama Viongozi na tumeelekeza nafasi zao zizibwe haraka”
"Kamati Kuu imeazimia kuwavua uanachama wake wote 19 wakiongozwa na Halima Mdee , walioapa kule Dodoma.-Mbowe
Duh! tumeshayakosa ma-trilioni.Mbowe ana balaaa.Labda wazime mtandao tena.Kwa vyovyote vile hizi habari zitawafikia wahisani tu.
 
Chama cha siasa kina autonomy ya kuendesha mambo kwa katiba ya chama.

Hapo cha kuangaliwa ni katiba ya chama.

Kwa mfano tu, katiba ya chama ikisema Mwenyekiti anaweza kumfukuza mwanachama yeyote bila mjadala, na wanachama wakakubali hilo na kujiunga na chama, siku mwenyekiti akimfukuza mtu uanachama, bila mjadala, mwanachama hatakiwi kulalamika mahakamani.

Maana aliikubali katiba ya chama.

Sasa katiba ya chama inasemaje?
Mahakama kuu ina unlimited jurisdiction kwenye masuala ya judicial review pale ambapo mtu anakwenda kwake kudai haki msingi baada ya kuvunjwa na judicial au administrative body yoyote iliyokuwa inafanya quasi judicial function na ina aibu sana na haitaki kuwekewa kikwazo chochote cha derivative au oyster claws kama hili suala unalolisema la party autonomy
 
Mahakama kuingilia mambo ya chama sehemu ambapo chama kishajiwekea utaratibu wa kichama unaokubalika ni illogical, invasive and undemocratic.

Pia, hapo kuna hatari ya mahakqma kutumiwa kisiasa, hususan na chama tawala, kuvuruga vyama vya siasa, hususan vyama vya upinzani.

Hapo ndipo unaweza kupata mwanachama mamluki anafukuzwa uanachama na vikao halali vya chama, halafu analazimisha uanachama mahakamani na kushinda.

Ni kama Papa wa Wakatoliki ana mu excommunucate muumini, na kusema huyu kwa mujibu wa Canon Law kafanya makosa haya na haya, si Mkatoliki kuanzia leo, halafu huyo muumini akimbilie mahakamani kudai abaki kuwa Mkatoliki. Na mahakama imoe ushindi muumini abaki kuwa Mkatoliki. Litakuwa jambo la ajabu sana.

Kuhusu unlimited jurisdiction, tuchukue mfano kuichunguza hii unayoisema unlimited jurisdiction.

Tuchukulie mfano Rais akimfukuza kazi Mkuu wa Mkoa summarily, Mkuu wa Mkoa anaweza kwenda mahakamani na kudai haki yake kwamba hajasikilizwa na Mahakama itengue uamuzi wa rais?

Mkatoliki akifukuzwa Ukatoliki anaweza kwenda mahakamani kupinga maamuzi ya kanisa ili arudishwe Ukatolikini na mahakama?
 
Kukua kwa CHADEMA hakuhitaji mikakati kihivyooooo.Kinakua automatically kulingana na watu kutoridhishwa na mwenendo wa serikali iliyopo madarakani.Hivyo kukua kwa CHADEMA ni kugusa tu.
Inatakiwa chama kikue nakiwe bora na imara .
 
Back
Top Bottom