Mbona umepaniki hivyo,au mpango wenu umebuma hivyo inawauma??? Mtavuna mlichopanda!
Hivi nyie Mnawasikiliza akina Mbowe mnafikiri wana nia njema na nchi hii?
Jiukize kwa nini Mnyika hakugombea ubunge?
Kwa nini wagomee viti maalum ?
Hivi unaweza kuumbia umma kuna umuhimu gani wa kuwanyima wale akina mama fursa ya kwenda bungeni kuendeleza mapambano ndani ya bunge ?
Je, wewe binafsi unafaidika nini wale wa kina mama kunyimwa fursa hiyo iliyopo kikatba kwa kuchukua form na kuzikalia ofisini tu bila kuwapa fursa ya kutoa maoni yao kuwa waende au wasiende?
Demokrasia ni pamoja na kuwasikiliza wale waliopinga wazo la kuvunja katiba ya nchi kwa kukataa kupeleka wabunge wa viti maalumu.
SWALI la kujiuliza ni Je, Mbowe ametumia kifungu kipi cha katiba ya nchi kuzuia wabunge waliotakiwa kuteuliwa kikatiba kuingia bungeni!
Je, kuna sheria inayoruhusu Chama cha siasa kuamua mambo yake kinyume na katiba ya nchi!?
Je, ni kifungu kipi cha katiba ya Chadema kinachowapa mamlaka viongozi kuacha kupeleka wabunge wa viti maalumu Bungeni kwa sababu za kizushi kuwa uchaguzi ulivurugwa bila ushahidi wa kutosha zaidi ya kulalamika tu?
Ni lini uchaguzi ulikua huru na haki ?
Kama hakuna sheria wala katiba inayowaruhusu viongozi wa Chama cha siasa kukiuka matakwa ya kikatiba basi Mbowe anapaswa kukamatwa na kuburuzwa mahakamani pamoja na Mnyika na kufungwa jela miaka mia.