Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Aaaah! Ticha! Mpe basi angalau maksi za wino jmnkiingereza bado sana
NEC siku hizi kimekuwa chama Cha siasa?Ni hatari Sana.Atatoa tamko ila ni uchwara kwa serikali ya CCM, hata akiwafukuza uanachama bado wana baraka za NEC watashinda tuuu
Ngoja waisome namba, usaliti haujawahi kumwacha mtu salamaMwenyekiti wa CHADEMA Taifa, Freeman Mbowe atazungumza na Umma wa Watanzania kupitia mkutano na waandishi wa habari, leo Novemba 27, 2020, kuanzia saa 3.00 (usiku huu), kuhusu maamuzi ya Kikao cha Kamati Kuu ya Chama...
Wenyewe wanamuita Mzee wa konyagi kubwa! Ila mambo anayoyafanya tofauti na mlevi! Kwenye makorido ya Lumumba hapakaliki.Mwamba amewaachia kilio Mataga mmebaki mnahaha 🤣 🤣 🤣
Yaani hata wewe Ustaadh hujaelewa!?
Kuna tatizo kubwa sana huko Tanzania la uelewa.
haha mataga roho imewauma hadi mmetamani pasikuche.Kwani hicho chama au saccos ni yetu mkuu!!? Mbona hamjitambui nyinyi nyumb?
View attachment 1636534
haha mataga roho imewauma hadi mmetamani pasikuche.
Acha ubinafsi ,kafungwe wewe unaeshabikia watu kughushi sahihi za wengine .CCM wamezoea wizi kwa hiyo hao wamama kughushinsahihi ya Katibu hawaoni shida.Mungu tusaidie hii dhambi wasiridhi wajukuu zetu ndio maana umakini imekuwa kama laana Tanzania.Tuna raslimali lakini kwa miaka 50 walioko madarakani wanaghushi tuHivi nyie Mnawasikiliza akina Mbowe mnafikiri wana nia njema na nchi hii?
Jiukize kwa nini Mnyika hakugombea ubunge?
Kwa nini wagomee viti maalum? Hivi unaweza kuumbia umma kuna umuhimu gani wa kuwanyima wale akina mama fursa ya kwenda bungeni kuendeleza mapambano ndani ya bunge ?
Je, wewe binafsi unafaidika nini wale wa kina mama kunyimwa fursa hiyo iliyopo kikatba kwa kuchukua form na kuzikalia ofisini tu bila kuwapa fursa ya kutoa maoni yao kuwa waende au wasiende?...
Eti NEC waghushi, wajumbe wa kamati kuu waarifiwe, waende Dodoma, wakubali kuapishwa kuwa wabunge! Inaingia akilini kabisaaa? Kweli nyumbu ni nyumbu tu!
Mwenyekiti wa CHADEMA Taifa, Freeman Mbowe atazungumza na Umma wa Watanzania kupitia mkutano na waandishi wa habari, leo Novemba 27, 2020, kuanzia saa 3.00 (usiku huu), kuhusu maamuzi ya Kikao cha Kamati Kuu ya Chama
Vyombo vya habari vya Kitaifa na Kimataifa vimealikwa.
Stay Tuned for Updates
=================
Waandishi wanaanza kuwasili ukumbini wanaoingia wanatakiwa kuwa vitambulisho.
Muda wowote kuanzia Viongozi wa Chadema wataingia ukumbini kuongea na waandishi wa habari.
22:08: Bado Viongozi wa Chadema hawajafika ukumbini
Mkutano huo utakuwa live kupitia
Tayari Mwenyekiti wa CHADEMA Taifa Freeman Mbowe ameshafika ukumbini
Tunawashukuru Watanzania wengi ambao wanafuatilia kikao maalum cha ajenda moja ya kujadili, kushauriana na kutafakari juu ya wanachama wetu 19 waliokwenda kuapa kuwa wabunge wa viti maalum- Freeman Mbowe
"Sisi kama kamati kuu ya chama kikuu cha upinzani, tumeona na kuridhishwa kuna ukiukwaji mkubwa umekiukwa katika mchakato mzima wa uchaguzi na huu wa viti maalum. Tumejiridhisha ndani ya chama kuhusu mapungufu kadhaa yaliyofanyika-; Mbowe
“Chama chetu hakijateuwa Wabunge wa Viti Maalum lakini tunaona wapo Bungeni wanaapishwa”Mbowe
Tangu nchi hii ipate uhuru hatujawai kuona Mbunge/Wabunge wakiapishwa garage, mambo ya kihuni kabisa haya..." Mbowe
“Hiki chama kinaongozwa na principles bila kujali maumivu makubwa tuliyopitia chama chetu kitafuata utaratibu siku zote, kwahiyo kamati kuu imewavua nafasi zao za uongozi viongozi wote waliokua na nafasi katika mabaraza ya chama.” @freemanmbowetz
“Kamati Kuu imewavua Uongozi wale wote ambao walikuwa Viongozi kwenye Mabaraza kati ya hao Dada zetu 19 sitaki kupoteza muda kuwataja majina, kwahiyo kuanzia sasa hawapaswi kushughulika na lolote kama Viongozi na tumeelekeza nafasi zao zizibwe haraka” -MBOWE
"Ili kanuni ambayo Spika ametumia iweze kufanya kazi kuapisha wabunge wetu. Kwanza wangestahili kubadilisha Katiba iruhusu wabunge kuapishwa nje ya utaratibu ambao ni ndani ya Bunge" -
Nusrate Hanje Katibu wa Bavicha amefungwa jela siku 133 kwa makosa yenye dhamana, hawa Watesi wetu wanakwenda kumtoa saa moja usiku akaape.”
”Chama chetu hakijateua Wabunge wa Viti Maalum tunaona tu Watu wetu wanaapishwa na hatuna taarifa, hatujapeleka majina, fomu za Tume zipo ofisini Mama zetu hawa Dada zetu hawajajaza fomu, ila tunaona tu wanaaapishwa”-
"Sisi kama chama cha siasa, hii 'process' yote hatuijui, tunaona tu wabunge wetu wanaapishwa. Chama chetu hakijateua wabunge wa viti maalum" -
"Wabunge hawa 19, mama zangu na dada zangu wameapishwa kiapo batili kwani Katiba inasema waapishwe mbele ya Bunge. Sasa kanuni zimebadilishwa ili kumruhusu Spika kumwapisha popote hata eneo la gereji-
“Tangu Nchi yetu imeanza hatujawahi kuona Wabunge wanaapishwa Gereji, lakini Dada zetu na Mama zetu hawa wameapishwa nje ya Bunge, wakati Katiba inataka waapishwe ndani ya Bunge, kwahiyo wamekula kiapo batili”
Mwenyekiti wa CHADEMA Freeman Mbowe amesema Kamati Kuu ya Chama hicho iliyoketi leo Nov 27,2020 imeazimia kuwavua uanachama Halima Mdee na wenzake 18 waliopishwa juzi kuwa Wabunge Viti Maalum “wamekinajisi Chama na wamekataa kuja kwenye Kamati Kuu”
”Chama chetu hakijateua Wabunge wa Viti Maalum tunaona tu Watu wetu wanaapishwa na hatuna taarifa, hatujapeleka majina, fomu za Tume zipo ofisini Mama zetu hawa Dada zetu hawajajaza fomu, ila tunaona tu wanaapishwa”
“Kamati Kuu imewavua Uongozi wale wote ambao walikuwa Viongozi kwenye Mabaraza kati ya hao Dada zetu 19 sitaki kupoteza muda kuwataja majina, kwahiyo kuanzia sasa hawapaswi kushughulika na lolote kama Viongozi na tumeelekeza nafasi zao zizibwe haraka”
"Kamati Kuu imeazimia kuwavua uanachama wake wote 19 wakiongozwa na Halima Mdee , walioapa kule Dodoma.-Mbowe
ORODHA YA WABUNGE WA VITI MAALUM WA CHADEMA 2020 WALIOVULIWA UWANACHAMA NI:
1. Halima Mdee
2. Grace Tendega
3. Ester Matiko
4. Cecilia Pareso
5. Ester Bulaya
6. Agnesta Kaiza
7. Nusrat Hanje
8. Jesca Kishoa
9. Hawa Mwaifunga
10. Tunza Malapo
11. Felister Njau
12. Naghenjwa Kaboyoka
13. Sophia Mwakagenda
14. Kunti Majala
15. Stela Fiayo
16. Anatropia Theonest
17. Salome Makamba
18. Conchesta Rwamlaza
19. Asia Mohammed
Watabaki kuwa vitu maalum vya ccmWacha wavuliwe tamaa zao zimewaponza, hivi huo uanachama waliovuliwa bado wataendelea kukaa bungeni kama viti maalum au itakuwaje?
Acheni kujidanganya hao bado ni wanachadema halali, hao wanawazuga tuu mtulize jazba upepo ukitulia mambo yanaendelea.Watabaki kuwa vitu maalum vya ccm
Tunaruhusiwa kujipa matumaini mwana ccm mwenzangu.Acheni kujidanganya hao bado ni wanachadema halali, hao wanawazuga tuu mtulize jazba upepo ukitulia mambo yanaendelea.
Komwnti hii ndiyo nimekuwa nikisubiri, na ndiyo kitu imetokea KABISA!Nawasalimu wanajukwaa,
Kwanza nianze kwa kuwapongeza Chadema kwa kutumia strategy kali ili " kuwazuga" mashabiki wenu wa mitandaoni ambao wao kazi yao ni kuwapa moyo na siku ya kupiga kura hawaendi kuwapigieni kura.
Hivi ni nani asiyetaka ruzuku ili chama kiendelee kufanya kazi yake? Msitudanganye hapa mliwaruhusu hawa wakina Mama waende wakaape na pia mkaandaa strategy ya kupambana na wanazi wenu wa mitandaoni na kwakweli mmefanikisha.
Kwasasa ni bao moja kwa moja mmesawazisha, wao hawakuenda kuwapigia kura na mlipo waamasisha hawakuitikia wito wenu na nyie mkaamua tusikie ruzuku nendeni mkaape ili kila mtu apambane na lake.
Hongereni sana Chademaa law strategy kali namna hii.
Hongereni wakina Mama kwa ushujaa,
Hongereni Watanzania kwa umoja na mshikamano.
Absolute truth!!! Kudos!Baada ya kusikiliza kile kilichoitwa maamuzi ya kikao cha kamati kuu haya ndiyo nimejionea.
1. Wamevuliwa uanachama wa Chadema kwa sababu hawajatokea kuhojiwa na kamati kuu na siyo sababu ya ubunge wa viti maalum!
2. Wameambiwa wanaweza kuandika barua ya kuomba radhi ili warejeshewe uanachama wao!
3. Ndani ya siku 30 wanaweza kukata rufaa kwa kupinga hukumu ya kamati kuu kwenye baraza kuu la Chadema!
4. Chadema iliwaandikia barua mara mbili kuwabembeleza wafike kuhojiwa na kamati kuu pia kamati kuu ililazimika kubadili eneo la kuwahoji kutoka makao makuu ya chadema hadi kwenye hoteli ya kitalii ili kulinda usalama wao.!
Mtu ambaye ni msaliti unaweza kumbembeleza kwa kumwandikia barua mbili na hadi kuingia gharama za kukodi hoteli ili kumuhoji?
Ni vipi msaliti aruhusiwe kuandika barua ya kuomba radhi tu na atarudishiwa uanachama wake?
Mbona Zito Kabwe na Kitila Mkumbo wakati wanafukuzwa hawakupewa nafasi ya kuomba radhi na kurudishiwa uanachama wao?
Hapa kuna sinema inachezwa na ndani ya siku 30 tutaona matokeo yake, kama mtu alikuwa tayari kutengeneza igizo la kuangushwa na konyagi na kisha kusingizia wasiojulikana, hapa kuna mengi yanakuja.
Mi kinachonifurahisha ni kuwa, hao wanao ghushi wana uwezo mpaka wa kughushi wajumbe wa Kamati Kuu ya chama makini, chenye makamanda jembe, vichwa na wenye weledi kwenda kuapishwa lakini hawawawezi mashabiki maandazi wa mitandaoni. Hilo tuIkiwa wanaghusi kura fake washindwe barua ya chama? Nec ndio serikali mkuu
Hiyo future ya kisiasa ingewasaidiaje kuvuka hapo waliokuwa?Maana kama ni ubunge wengine tayari wameuishi Sana,na tayari walikuwa wameukosa.Wasichana wadogo wameharibiwa future yao kisiasa kwa mambo ya kipuuzi kabisa.