Kamati Kuu ya CHADEMA yawavua nyadhifa na uanachama Halima Mdee na wenzake 18 walioapishwa kuwa Wabunge wa Viti Maalum

Kamati Kuu ya CHADEMA yawavua nyadhifa na uanachama Halima Mdee na wenzake 18 walioapishwa kuwa Wabunge wa Viti Maalum

Haupo CCM wala CHADEMA, ila unakatishwa tamaa na muongozo wa CHADEMA, ila at the same time huoni mwenendo wa nchi chini ya CCM ulivyo tokea uhuru mpaka leo. Au umeridhika nao?

Sent from my SM-G955U using JamiiForums mobile app
Sijasema kwamba nimeridhika na mwenendo wa nchi chini ya CCM.

Kuna mambo ya kupigania kila siku sio mpaka siku/baada ya uchaguzi. Unajua kwamba tume ya uchaguzi sio huru, kwanini ulitegemea uchaguzi huru na wa haki?
 
Mwenyekiti wa CHADEMA Taifa, Freeman Mbowe atazungumza na Umma wa Watanzania kupitia mkutano na waandishi wa habari, leo Novemba 27, 2020, kuanzia saa 3.00 (usiku huu), kuhusu maamuzi ya Kikao cha Kamati Kuu ya Chama

Vyombo vya habari vya Kitaifa na Kimataifa vimealikwa.

Stay Tuned for Updates

=================

Waandishi wanaanza kuwasili ukumbini wanaoingia wanatakiwa kuwa vitambulisho.

Muda wowote kuanzia Viongozi wa Chadema wataingia ukumbini kuongea na waandishi wa habari.

22:08: Bado Viongozi wa Chadema hawajafika ukumbini

Mkutano huo utakuwa live kupitia

Tayari Mwenyekiti wa CHADEMA Taifa Freeman Mbowe ameshafika ukumbini

Tunawashukuru Watanzania wengi ambao wanafuatilia kikao maalum cha ajenda moja ya kujadili, kushauriana na kutafakari juu ya wanachama wetu 19 waliokwenda kuapa kuwa wabunge wa viti maalum- Freeman Mbowe

"Sisi kama kamati kuu ya chama kikuu cha upinzani, tumeona na kuridhishwa kuna ukiukwaji mkubwa umekiukwa katika mchakato mzima wa uchaguzi na huu wa viti maalum. Tumejiridhisha ndani ya chama kuhusu mapungufu kadhaa yaliyofanyika-; Mbowe

“Chama chetu hakijateuwa Wabunge wa Viti Maalum lakini tunaona wapo Bungeni wanaapishwa”Mbowe

Tangu nchi hii ipate uhuru hatujawai kuona Mbunge/Wabunge wakiapishwa garage, mambo ya kihuni kabisa haya..." Mbowe

“Hiki chama kinaongozwa na principles bila kujali maumivu makubwa tuliyopitia chama chetu kitafuata utaratibu siku zote, kwahiyo kamati kuu imewavua nafasi zao za uongozi viongozi wote waliokua na nafasi katika mabaraza ya chama.” @freemanmbowetz

“Kamati Kuu imewavua Uongozi wale wote ambao walikuwa Viongozi kwenye Mabaraza kati ya hao Dada zetu 19 sitaki kupoteza muda kuwataja majina, kwahiyo kuanzia sasa hawapaswi kushughulika na lolote kama Viongozi na tumeelekeza nafasi zao zizibwe haraka” -MBOWE

"Ili kanuni ambayo Spika ametumia iweze kufanya kazi kuapisha wabunge wetu. Kwanza wangestahili kubadilisha Katiba iruhusu wabunge kuapishwa nje ya utaratibu ambao ni ndani ya Bunge" -

Nusrate Hanje Katibu wa Bavicha amefungwa jela siku 133 kwa makosa yenye dhamana, hawa Watesi wetu wanakwenda kumtoa saa moja usiku akaape.”

”Chama chetu hakijateua Wabunge wa Viti Maalum tunaona tu Watu wetu wanaapishwa na hatuna taarifa, hatujapeleka majina, fomu za Tume zipo ofisini Mama zetu hawa Dada zetu hawajajaza fomu, ila tunaona tu wanaaapishwa”-

"Sisi kama chama cha siasa, hii 'process' yote hatuijui, tunaona tu wabunge wetu wanaapishwa. Chama chetu hakijateua wabunge wa viti maalum" -

"Wabunge hawa 19, mama zangu na dada zangu wameapishwa kiapo batili kwani Katiba inasema waapishwe mbele ya Bunge. Sasa kanuni zimebadilishwa ili kumruhusu Spika kumwapisha popote hata eneo la gereji-

“Tangu Nchi yetu imeanza hatujawahi kuona Wabunge wanaapishwa Gereji, lakini Dada zetu na Mama zetu hawa wameapishwa nje ya Bunge, wakati Katiba inataka waapishwe ndani ya Bunge, kwahiyo wamekula kiapo batili”

Mwenyekiti wa CHADEMA Freeman Mbowe amesema Kamati Kuu ya Chama hicho iliyoketi leo Nov 27,2020 imeazimia kuwavua uanachama Halima Mdee na wenzake 18 waliopishwa juzi kuwa Wabunge Viti Maalum “wamekinajisi Chama na wamekataa kuja kwenye Kamati Kuu”

”Chama chetu hakijateua Wabunge wa Viti Maalum tunaona tu Watu wetu wanaapishwa na hatuna taarifa, hatujapeleka majina, fomu za Tume zipo ofisini Mama zetu hawa Dada zetu hawajajaza fomu, ila tunaona tu wanaapishwa”

“Kamati Kuu imewavua Uongozi wale wote ambao walikuwa Viongozi kwenye Mabaraza kati ya hao Dada zetu 19 sitaki kupoteza muda kuwataja majina, kwahiyo kuanzia sasa hawapaswi kushughulika na lolote kama Viongozi na tumeelekeza nafasi zao zizibwe haraka”

"Kamati Kuu imeazimia kuwavua uanachama wake wote 19 wakiongozwa na Halima Mdee , walioapa kule Dodoma.-Mbowe

ORODHA YA WABUNGE WA VITI MAALUM WA CHADEMA 2020 WALIOVULIWA UWANACHAMA NI:
1. Halima Mdee
2. Grace Tendega
3. Ester Matiko
4. Cecilia Pareso
5. Ester Bulaya
6. Agnesta Kaiza
7. Nusrat Hanje
8. Jesca Kishoa
9. Hawa Mwaifunga
10. Tunza Malapo
11. Felister Njau
12. Naghenjwa Kaboyoka
13. Sophia Mwakagenda
14. Kunti Majala
15. Stela Fiayo
16. Anatropia Theonest
17. Salome Makamba
18. Conchesta Rwamlaza
19. Asia Mohammed

MBOWE hana tofauti na OBAMA, huyu jamaa ni zaidi ya Presidential material, anaongea mpaka machpzi yanatoka, yaani HALIMA MDEE amepambaniwa na watu mpaka wameingia kaburini matumbo ya marehemu hayapasuka kishawasaliti?
Bulaya umesaliti maiti 5 zilizokuwa zinakupigania sasa umejiunga na watesi?
Hakika nawaambia Usaliti wa COVI -19 utawatafuna.
 
Sijasema kwamba nimeridhika na mwenendo wa nchi chini ya CCM.

Kuna mambo ya kupigania kila siku sio mpaka siku/baada ya uchaguzi. Unajua kwamba tume ya uchaguzi sio huru, kwanini ulitegemea uchaguzi huru na wa haki?
Unapokuwa na matatizo mengi, kuna yale unayoamua kuyapa kipaumbele. Ww kipaumbele chako ni nini?

Sent from my SM-G955U using JamiiForums mobile app
 
Halima angekuwa na akili na ustaarabu asingeshawishi wenzie kuwa na tamaa ya viti maalum kwa maana wakati wa kura za maoni aliomba ridhaa ya kugombea jimbo sio viti maalumu it means wahusika wa viti maalumu wapo angewapigania hao na si kujipa yeye nafasi isiyomuhusu pamoja na viongozi wengine wa bawacha yeye aligombea kawe na si viti maalumu amefanya makosa makubwa si wa kumuamini
 
Baada ya maamuzi haya Chadema imekuwa bora zaidi kuliko awali, imejipambanua kwa matendo juu ya madai yake ya kukiukwa kwa kanuni za msingi za uendeshaji wa chaguzi zetu na ukandamizaji wa haki za binadamu.

Ni katika hili, mimi binafsi na mamilioni ya watanzania tunapoitaka chadema kuitisha harambee ya kuchangia fedha ili kuonesha furaha zetu.

Fedha hizo zitatumika kwa jinsi chama watakavyoona inafaa.

Viva chadema2020. - Imeisha hiyo.

Sasa turudi kwenye kashfa ya fedha za corona. Maana European tax payers wanataka maelezo huko.
Kesho Jumapili ya kwanza ya Majilio,leo jumamosi ya mwisho ya mwezi sisi wakatoliki katika jimbo letu huwa tunakuwa na ibada ya kigango ikiwa ni mkusanyiko wa jumuia zote za kigango."Imani bila matendo ni kazi bure" Nachukua fursa hii kukipongeza chadema kwa kuwaondoa wote walioshiriki tendo ovu na kujawa na kiburi na dharau kisa umaarufu walionao.Ibada yangu ya leo imekuwa ya furaha na amani kwa kuwa chadema wameadhibu bila kuogopa vitisho toka serikalini, bunge na vyombo vyake vyote.Ibada ya toba ya majilio inaanza roho yangu ikiwa safi na ya kuheshimu kilichoamriwa.Chadema idumu kwa msimamo thabiti.Hongera kamati kuu.
 
Kwanza, napenda kumpongeza Mwenyekiti wa CHADEMA Mh Freeman Aikael Mbowe kwa uamuzi madhubuti na sahihi kwa kuwafukuza uanachama kundi lote la Covid 19. Adhabu uliowapa inaonyesha wazi kuwa usaliti wao ni hatari kwa CHADEMA. Pili, niseme kuwa nadhani adhabu hiyo haitoshi kwa sababu upo uwezekano wa jinai ambayo inatokana na kughushiwa nyaraka zilizopelekwa TUME ya Uchaguzi na hatimaye Bunge. Kwa msingi huo basi ipo haja ya kufanya uchunguzi wa kina ili kujua nani hasa alighushi nyaraka husika na sheria ya JMT ichukue mkondo wake.
Mwisho napenda kuuliza inakuwaje sasa Ndugai, NEC, AG, na wengine wanawapenda na kuwalinda wapinzani wakati wao hao hao ndio walioabambika kila aina majina kipindi cha Uchaguzi? Ushauri wangu kwa Halima Mdee ni kwamba ngoma imefika mwisho. Kaa kimya anza maisha mengine. Kama unao ubavu wafichue waliokushindikiza ufanye uliyoyafanya, ila uwe tayari kupata madhara ya maamuzi yako. CCM haina tofauti na MAFIA ni kundi la watu wanaojali maslahi yao tuu, kama ukiwaingilia wanakuondoa na hawana huruma yoyote.
 
Inaonekana imekuuma sana eeh!!?
[emoji38][emoji38][emoji38][emoji38][emoji38]
Haisaidiii chochote kutukana mitandaono lakini mtaani mnajikunyata kama mbwa koko!!

Jitokeze hadharani unyoshekidole.
Mimi ninaweza nikakuelekeza mpaka ninapokaa na huna cha kunifanya.

Mnashindwa kufanya siasa za kistarabu mnabaki kuwaumiza wakina mama kwa sababu mmeshawatumia sasa mnataka kuwadanganya wengine.
 
Hongera sana chama hiki kwa kuonyesha ukomavu wa kisiasa sasa yule Mbunge Msukuma alosema halima wakifukuzwa atajua na kujifunza democracy iliyopo Chadema sasa nadhani ameiona na amejua kwa kutambua ushauri wangu kwake yeye kama kijana ajifunze kuwa chama chochote chenye watu wanaosimamia haki huwa hawaangalii maslahi kwanza wanaangalia nchi yao kwanza
 
Naam mkuu. Na ule wimbo wa Mbowe ndio kawapitisha ndio maana hajitokezi kuongea siusikii tena.
 
Kwanza, napenda kumpongeza Mwenyekiti wa CHADEMA Mh Freeman Aikael Mbowe kwa uamuzi madhubuti na sahihi kwa kuwafukuza uanachama kundi lote la Covid 19. Adhabu uliowapa inaonyesha wazi kuwa usaliti wao ni hatari kwa CHADEMA. Pili, niseme kuwa nadhani adhabu hiyo haitoshi kwa sababu upo uwezekano wa jinai ambayo inatokana na kughushiwa nyaraka zilizopelekwa TUME ya Uchaguzi na hatimaye Bunge. Kwa msingi huo basi ipo haja ya kufanya uchunguzi wa kina ili kujua nani hasa alighushi nyaraka husika na sheria ya JMT ichukue mkondo wake.
Mwisho napenda kuuliza inakuwaje sasa Ndugai, NEC, AG, na wengine wanawapenda na kuwalinda wapinzani wakati wao hao hao ndio walioabambika kila aina majina kipindi cha Uchaguzi? Ushauri wangu kwa Halima Mdee ni kwamba ngoma imefika mwisho. Kaa kimya anza maisha mengine. Kama unao ubavu wafichue waliokushindikiza ufanye uliyoyafanya, ila uwe tayari kupata madhara ya maamuzi yako. CCM haina tofauti na MAFIA ni kundi la watu wanaojali maslahi yao tuu, kama ukiwaingilia wanakuondoa na hawana huruma yoyote.
Siasa imekuja kuwa tamu nyakati hizi yani hutamani kucheki move za intelligence bali siasa ya bongo imetosha kabisa. Inakupa kuwaza kwa kina what next.
Ni tayari kina mdee wamesha vuliwa uwanachama je watakuwa tayari kungana na ccm au chama kingine cha upinzani. Naomba maoni ndugu yangu.
 
Hivi watu mmeamini kabisa tu kuwa Halima Mdee huyuhyu amefanya jambo kama lile kwa kukurupuka tu?
 
Back
Top Bottom