Kamati Kuu ya CHADEMA yawavua nyadhifa na uanachama Halima Mdee na wenzake 18 walioapishwa kuwa Wabunge wa Viti Maalum

Kamati Kuu ya CHADEMA yawavua nyadhifa na uanachama Halima Mdee na wenzake 18 walioapishwa kuwa Wabunge wa Viti Maalum

Hawajavuliwa uanachama bali Kamati kuu imewavua vyeo vyote na kuazimia kuwavua Uanachama

Sio Wewe tu hata Waandishi wengi wameshindwa kutofautisha kati ya kuwavua Uanachama na kuazimia kuwavua Uanachama
Narudia tena,kuna tatizo kubwa sana la uelewa huko nyumbani,na wewe ni mmojawapo wa wenye tatizo hilo.
Wapi nimeshindwa kutofautisha kati ya kuwavua uanachama na kuazimia kuwavua uanachama!?
 
Ila Akina ESTHER huwa wana matatizo sana.Hamnaga Esther ambaye sio cheap
 
Ila Akina ESTHER huwa wana matatizo sana.Hamnaga Esther ambaye sio cheap
Acha bwana! Chademaaa mmeamua kuwatukana sasa makamanda wenzenu...Ila Watanzania wote tunajua hawa wanawake ni mashujaa.
 
Kamati kuu imefanya makosa makubwa sana kuwafukuza Halima Na wenzake
 
Kwanza, napenda kumpongeza Mwenyekiti wa CHADEMA Mh Freeman Aikael Mbowe kwa uamuzi madhubuti na sahihi kwa kuwafukuza uanachama kundi lote la Covid 19. Adhabu uliowapa inaonyesha wazi kuwa usaliti wao ni hatari kwa CHADEMA. Pili, niseme kuwa nadhani adhabu hiyo haitoshi kwa sababu upo uwezekano wa jinai ambayo inatokana na kughushiwa nyaraka zilizopelekwa TUME ya Uchaguzi na hatimaye Bunge. Kwa msingi huo basi ipo haja ya kufanya uchunguzi wa kina ili kujua nani hasa alighushi nyaraka husika na sheria ya JMT ichukue mkondo wake.
Mwisho napenda kuuliza inakuwaje sasa Ndugai, NEC, AG, na wengine wanawapenda na kuwalinda wapinzani wakati wao hao hao ndio walioabambika kila aina majina kipindi cha Uchaguzi? Ushauri wangu kwa Halima Mdee ni kwamba ngoma imefika mwisho. Kaa kimya anza maisha mengine. Kama unao ubavu wafichue waliokushindikiza ufanye uliyoyafanya, ila uwe tayari kupata madhara ya maamuzi yako. CCM haina tofauti na MAFIA ni kundi la watu wanaojali maslahi yao tuu, kama ukiwaingilia wanakuondoa na hawana huruma yoyote.

Unampongeza Mbowe wakati chama kina mwifia mikononi mwake, ulipaswa umshauri ajiuzulu apishe nguvu mpya ijenge chama kwani yeye kashindwa, kila kukicha chama kina puputika
 
Umeuliza kuhusu rais,Lissu imekuwaje tena?

NB.Usifananishe volcano na jivu la mabua!

nakushauri kwa saaahv jitahidi sana kwenye mshahara wako wa mwisho wa mwezi tenga fungu la kupeleka ufipa otherwise ni kilio zaidi
 
Inaonekana imekuuma sana eeh!!?
[emoji38][emoji38][emoji38][emoji38][emoji38]

Hapana haijaniuma mana hakuna ndugu yangu kati ya wale 19 lakini hawa wanasiasa wanacheza na akili za watu sana.
Watu wamegombea wakijua kuwa hakuna Tume huru na awamu yenyewe ni Tata kwenye masuala ya vyama. Sasa wamenyolewa kichwa bila maji wanajifaya wanagomea kunyolewa ndevu bila maji!

Wanafiki sana, wengine tuliwapigania wapinzani tangu mwaka 1995 lakini tunaona kuwa hawajui hata wanachokitafuta.

Watu wameuawa ,ndio ,ni kosa kubwa , hivi akili ya kuwasaidia ndugu wa marehemu ni kuzuia wabunge wanawake wanaoteuliwa kwenye vyama kwenda Bungeni!!?
 
Tarehe kama ya leo mwezi uliopita Halima Mdee alikamata kura feki zilizotengenezwa na hao hao ccm, yaani ndani ya mwezi mmoja anashirikiana nao hao hao watesi wake! Simwelewi kwa kweli
 
Ukiwa na short sitness uwezi ona impact yake.
Hivyo sikulaum maana sio kosa lako.
Hapana haijaniuma mana hakuna ndugu yangu kati ya wale 19 lakini hawa wanasiasa wanacheza na akili za watu sana.
Watu wamegombea wakijua kuwa hakuna Tume huru na awamu yenyewe ni Tata kwenye masuala ya vyama. Sasa wamenyolewa kichwa bila maji wanajifaya wanagomea kunyolewa ndevu bila maji!..
 
Hunijui sikujui ila nimekuwa mfuasi wako siku zote. Mimi ni mwalimu tena wa shule ya wasichana,nimekuwa nikiwahimiza na kuwaasa waige mfano wako maana wewe Ni mwanamke shupavu na mfano wa kuigwa.

Nakuomba rudi kwenye mstari, kuombe msamaha chama chako, ulinde heahima na reputation ulitumia muda mwingi kuijenga. Ulikuwa binti mdogo ungekuwa unakula bata na kujirusha lakini hukufanya hivyo, nakuomba linda heshma uliyoijenga, omba msamaha chama kitakusamehe.
 
Back
Top Bottom