Kamati Kuu ya CHADEMA yawavua nyadhifa na uanachama Halima Mdee na wenzake 18 walioapishwa kuwa Wabunge wa Viti Maalum

Kamati Kuu ya CHADEMA yawavua nyadhifa na uanachama Halima Mdee na wenzake 18 walioapishwa kuwa Wabunge wa Viti Maalum

Si kweli Kama wamevuliwa uanachama bali Kamati Kuu imeazimia kuwavua uanachama. Hivyo hilo ni bado azimio, halijapitishwa. Kiswahili lugha yetu tuielewe. Kwa maana hiyo ya Kamati Kuu, Halima Mdee navwenzake bado wanachama wa Chadema, bado wabunge mpaka hapo azimio la kuwavua uanachama litakapopitishwa! Maneno yana maana, tutambue maana, tusitafsiri hisia zetu.
 
Mkuu mleta mada

1. Nusrat hakuapishwa saa moja usiku kama ulivyomnukuu Mbowe kila mmoja aliona tukio hilo ilukwa ni mchana kweupe;
2. Mh Freeman Mbowe kudai taratibu na kanuni za kudumu za bunge zimekiukwa na kwamba mbunge anaapishwa ndani ya bunge pekee wakati akijua anasema uongo wa wazi kabisa maana yeye pamoja na wabunge wengine walishiriki kubadilisha kanuni Agosti 2020 (Rejea TANGAZO LA SERIKALI NA. 626 la tarehe 7/8/2020) na mabadiliko ni haya:
(2) Bila ya kujali masharti ya fasili ya
(1), endapo Mbunge atachaguliwa au kuteuliwa baada ya Uchaguzi Mkuu, Spika atamwapisha katika: (a) kikao chochote cha Bunge iwapo kuna Mkutano wa Bunge; au (b) eneo litakalopangwa na Spika iwapo hakuna Mkutano wa Bunge unaoendelea na baadaye Spika atatoa taarifa Bungeni kwenye Kikao cha Kwanza cha Mkutano wa Bunge unaofuata.

(3) Wakati wa kuapa, Mbunge anayeamini kuwa kuna Mungu, atalazimika kushika Biblia au Kuran au kitabu kingine kitakatifu kinachotambuliwa na imani ya dini yake.
(4) Iwapo Mbunge haamini kuwa kuna Mungu, hatashika Biblia au Kuran au kitabu chochote kitakatifu au kutamka maneno, “Ewe Mwenyezi Mungu nisaidie,” bali atalazimika kuinua mkono wake wa kuume juu.
(5) Kiapo cha uaminifu cha Mbunge kitakuwa na maneno yafuatayo: “Mimi, ………..., naapa kwamba, nitakuwa mwaminifu kwa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na kuitumikia kwa moyo wangu wote na kwamba nitaihifadhi, nitailinda na kuitetea Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa mujibu wa Sheria iliyowekwa. Ewe Mwenyezi Mungu, nisaidie.”
Umesoma na kuelewa kuhusu kiapo kilikuwa kinaongelewa ?
"Nusrat Hanje, amekaa gerezani siku 133 kwa makosa yenye dhamana. Wamekwenda kumtoa jela usiku saa 1 kwa sababu Jamhuri haina nia ya kuendelea na mashtaka, mimi nimekaa jela, huwezi kutolewa saa 1 usiku watu wamekwisha lala ila walimtoa Nusrat na kumwapisha" Freeman Mbowe.
 
Si kweli Kama wamevuliwa uanachama bali Kamati Kuu imeazimia kuwavua uanachama. Hivyo hilo ni bado azimio, halijapitishwa. Kiswahili lugha yetu tuielewe. Kwa maana hiyo ya Kamati Kuu, Halima Mdee navwenzake bado wanachama wa Chadema, bado wabunge mpaka hapo azimio la kuwavua uanachama litakapopitishwa! Maneno yana maana, tutambue maana, tusitafsiri hisia zetu.
😄😄😄😄😀😀😀😀🤣🤣🤣😆😆Wape moyo
 
"Kamati Kuu ya ChademaTz imewavua uanachama Halima Mdee na wenzake 18 waliopishwa juzi kuwa Wabunge Viti Maalum kwa kosa la utovu wa nidhamu na usali" Mhe. Freeman Mbowe
Lakini mjengoni wataendelea kuwa wabunge wa CDM na hamna kitu mtu atawafanya.

Huwezi kushindana na dola.
 
Hata yuda kwenye biblia alisamehewa sema dhambi ya kujiua ndo ilimpeleka kwa shetan...
 
1.Wamevuliwa uanachama wa Chadema kwa sababu hawajatokea kuhojiwa na kamati kuu na siyo sababu ya ubunge wa viti maalum.

2. Wameambiwa wanaweza kuandika barua ya kuomba radhi ili warejeshewe uanachama wao.

3. Ndani ya siku 30 wanaweza kukata rufaa kwa kupinga hukumu ya kamati kuu kwenye baraza kuu la chadema.

4. Chadema iliwaandikia barua mara mbili kuwabembeleza wafike kuhojiwa na kamati kuu pia kamati kuu ililazimika kubadili eneo la kuwahoji kutoka makao makuu ya chadema hadi kwenye hoteli ya kitalii ili kulinda usalama wao.!

Mtu ambaye ni msaliti unaweza kumbembeleza kwa kumwandikia barua mbili na hadi kuingia gharama za kukodi hoteli ili kumuhoji?

Ni vipi msaliti aruhusiwe kuandika barua ya kuomba radhi tu na atarudishiwa uanachama wake?
demokrasia iliyopevuka iliwasipate visingizio apo unahisi wanatokaje
 
Si kweli Kama wamevuliwa uanachama bali Kamati Kuu imeazimia kuwavua uanachama. Hivyo hilo ni bado azimio, halijapitishwa. Kiswahili lugha yetu tuielewe. Kwa maana hiyo ya Kamati Kuu, Halima Mdee navwenzake bado wanachama wa Chadema, bado wabunge mpaka hapo azimio la kuwavua uanachama litakapopitishwa! Maneno yana maana, tutambue maana, tusitafsiri hisia zetu.

Wabunge 19 wa Viti Maalum kupitia Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) waliokula kiapo kuwa wabunge wa viti maalum hivi karibuni akiwemo Mwenyekiti wa Baraza la Wanawake wa Chama hicho, Halima Mdee wamevuliwa uanachama wa chama hicho na nafasi zao za uongozi kwa maamuzi ya kikao cha dharura cha Kamati Kuu ya Chama hicho kilichoketi Leo jijini Dar es Salaam.

Katika hatua nyingine Mwenyekiti wa CHADEMA FREEMAN MBOWE amesema wanachama waliovuliwa Uanachama wao Leo na Kamati Kuu ya Chama hicho bado, wanayo nafasi ya kuomba radhi au kukata rufaa iwapo hawajaridhishwa na maamuzi yaliyotolewa dhidi yao.
 
Back
Top Bottom