#COVID19 Kamati ya Corona: Serikali itoe taarifa uwepo wa Ugonjwa wa COVID-19 na kuruhusu matumizi huru ya chanjo

#COVID19 Kamati ya Corona: Serikali itoe taarifa uwepo wa Ugonjwa wa COVID-19 na kuruhusu matumizi huru ya chanjo

Tunashukuru sana maprofesa wetu maana nyie mnapata mishahara yenu minono na hata sasa mmepata pesa ya kutosha ktk kamati hii.
mmeona wananchi wa kawaida wanavyoishi kwa uhuru Tanzania pamoja na kujazana kwenye daladala hawafi inawauma sana.

mmeamua kutengeneza janga jingine la corona ili mnufaike na overtime na masemina ya kujikinga na corona ambayo kwa sasa haipo.
mmetumia usomi wenu kumpotosha rais ili atangaze visa ili kuleta hofu.Huku mkijua hofu ni mbaya kuliko ugonjwa wenyewe.

sasa nyie mnavaa barakoa zenye ubora kabisa na mnaweza kubadilisha kila baada ya masaa manne, wananchi wakiwa hawana huo uwezo wa kubadilisha hivyo.

Jueni kuwa nyinyi ni binadamu siku moja Mungu atawahukumu kwa madhara yote yatakayotokea ktk Taifa kutokana na mapendekezo yenu.

kama mmeleta ushauri wa kutaka kumfurahisha rais bila kuangalia uhalisia damu itatakwa mikononi mwemu.
 
Hayo mavitabu au yatakuwa kwenye mfumo wa audio tuwe tunasikiliza tu, kwa muda mfupi namna hii wamekuja na hayo mavitabu yote huo muda wameupata wapi, hili swala la kuchanjwa lipelekwa kwa wananchi wenyewe ndio waamue anayetaka kuchanjwa iwe kwa hiari yake mwenyewe, tusileteana kampeni.
 
Kwani kama ipo hawa watoto wanaojaa darasa watoto 500 kungekuwa na hosptali ya kuwalaza? na hawavai barakoa.
ilikuwepo kweli tulifunga siku 3 Mungu akaiponya nchi ndo maana maisha yakaendelea shule zikafunguliwa.
Kwa hiyo huyu Mungu ni kigeugeu kwamba alizuia Corona kipindi kile na sasa hivi ameiruhusu tena ije?
 
Kwa nini tusiishi nao kimya kimya kama hayo magonjwa mengine, lakini tahadhari zichukuliwe na sio promo na matakwimu kila siku.....kama chanjo ikija anaetaka achome na isiwe lazima....Ukweli usemwe kipindi corona inaingia zile takwimu za kila siku zilileta hofu kubwa sana ya maisha....naamni mpaka leo hii tungekuwa ndani tumekwisha kwa njaaa na hofu...Hivi hivi tunaishi watu wanaendelea na shughuli zao kama kawaida,leta hayo wanayoyataka hiyo tume uone maisha yatakavyo badilika.
Maprofesa wetu haya maisha ya kawaida hawayajui na hayawahusu wanashindwa kujua mama akikosea hapa italigharimu taifa na yeye itamgharimu maana ndo mtu pekee wananchi wanaweza kumhukumu 2025.ila akitenda kwa busara itakuwa heri kwake.
 
Tumefikia kutukanana kwa ajili ya chanjo? Serikali iweke Uhuru anaetaka achanjwe asiyetaka akae wala tusilazimishane.
 
Kwa hiyo huyu Mungu ni kigeugeu kwamba alizuia Corona kipindi kile na sasa hivi ameiruhusu tena ije?
Corona ipo hupo nyumbani kwako? Maana mimi na wenzangu tulisha sahau kitambo?
Unaihitaji? Basi ikija ianze na wewe na ukoo wako maana mnaitamani
 
Mkuu Covid ipo toka 2019 imepiga waves zote kwa nguvu nchi ambayo kwa sasa covid inaitesa ni INDIA ,Tanzania tuliamua kuchukua uamuzi wa wachache yani No Lockdown kuvaa mask ni utashi wako na kutozuia mikusanyiko na Mungu alikuwa upande wetu kwa maana hatuna athari kubwa sana za covid mpk sasa

Dunia inakwenda kufunguliwa kwa maana nchi nying zimeshaachana na masharti yale makubwa kuhusu covid (Lockdown,Mask On , Social Dis nk)na maisha yanaendelea kurudi kawaida tu.. sasa nitashangaa sana huyu mama kuturudisha nyuma yani mtoto anatembea kisa hakupitia stage ya kutambaa unamwambia arudie step ya kutambaa by the way Covid Funds wazungu hawatoi siku hz... coz trend ya Ugonjwa inakwisha Kenya wamekula sana hii hela sisi tukasema watusamehe madeni hatukuchukua sasa sijui huyu anataka nini

Hakuna Sehemu ambayo Mtanzania amepigwa Burn kuwa tusiende kote tunaenda ni kupima tu covid test then unajichanganya .. Ngoja tuone kilichokuwa nyuma ya yale mabarakoa waliokuwa wanavaa
The issue is Dunia inafunguliwa sikwamba ugonjwa umeisha isipokuwa ni baada ya kupatikana Chanjo so ikiwa huchanji watu wako pia hawataruhusiwa kuingia kwenye Nchi za watu tatizo jiwe aliaminisha watu kuwa tz ni kisiwa inaweza kuishi yenyewe bila kuitegemea Dunia sikweli...na uzuri wa hiyo chanjo halazimishwi mtu

Sent from my Nokia 8.1 using JamiiForums mobile app
 
Ndo wameandika hayo mavitabu yote au wamekopi tu maandishi ya wengine na kuyakusanya na kuyaweka yaonekane kama mavitabu?

Halafu sidhani kama Samia atayasoma 🤣.

Sidhani kama ni mtu wa kusoma mavitabu kama hayo.

Yeye ni mitandao tu 🤣🤣.
Hutaki kuchanjwa mfuate ndugu yako akhera ukamshitaki Samia
 
Maadhimio ya kikanda na kimataifa[emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787]
Aiseeh! Ila hapo tutatandikana marungu, hali ya kiuchumi sio poah, tukifungiana maisha haya tutatoboa kweli, na ajira kwa Sasa ni nguvu zako!
 
Back
Top Bottom