Kamati ya Mambo ya Nje ya Umoja wa Ulaya (EU) wataka kujua msaada wa Euro Mil. 27 za COVID-19 kwa Tanzania uliahidiwa kwa vigezo gani?

Kamati ya Mambo ya Nje ya Umoja wa Ulaya (EU) wataka kujua msaada wa Euro Mil. 27 za COVID-19 kwa Tanzania uliahidiwa kwa vigezo gani?

Hatuwezi broo.. Izo ni mbwembwe za Bongo comedy. Hapa wakiamua kutukazia mtarudi kwa mlango wa nyuma kupiga magoti na kulamba miguu turudishiwe misaada..
Hiyo ni sawa wewe uwe mfanyabiashara mkubwa kisha unamzuia machinga asiingie kweye soko lenye wateja kisha ujisifu kuwa machinga hawezi kukua na kufikia uwezo kama wako
Muache awe huru kuuza hadi pale unapouza uaone kma hatakuwa mfanya biashara mkubwa.
Sasa hawa wanatubana ili waendelee kutuibia kisha na sisi tulizike eti hatuwezi?
Ni lazima tubanane nao hadi waachie ili tusiwe tegemezi kwao.
 
Sisi tunataka kujitegemea siyo kuegemea kwa mtu kama wana chadema wanavyolilia
Tukibaguana hivi, tukitesana na kuoneana hivi tutaishia kuwa nchi ya hovyo.
Mataifa makubwa macho yao yapo Afrika, wanafanya kila namna ili waendelee kuifaidi Africa.
Africa tuna shida sana ya uongozi kwani viongozi wengi ni wabinafsi sana na ni mafisadi.
Uroho wa madaraka ni moja ya chanzo kikubwa cha ufisafi Africa.

Mataifa makubwa yanatafua mianya ya kuingilia Afrika, na mianya hiyo tunaitengeneza wenyewe kwa kushindwa kuunganisha wanannchi.

Baadhi ya watu wanaitazama hoja ya kuitafsiri demokeasia ya Afrika kama ni kigezo cha kutawala kidikteta.

Hulka ya binadamu ni kupenda kuwa uhuru,, lakini uhuru unatakiwa uwe na mipaka ambapo mipaka hiyo ndiyo sheria zetu.
Bado unakuta kiongozi wa Afrika anachagua sheria za kuziheshimu na zile zinazombana anatafuta namna ya kuziondoa au kuzibadilisha.
Ameshau kuwa na yeye pia ni binadamu ambaye uhuru wake una mipaka.(sheria zetu)

Mzungu anatumia vizuri utengano wetu (mianya) katika kuendelea kututawala.
 
Huyu Lord dening inabidi Mbowe sijui ampe cheo gani maana ana mawenge ya kushindwa
Huu ni mfumo wa kivuta Bangi kwani bado unashinda ukivuta Bangi hapo gheto kwa cyprian Musiba bado?
 
Kumbe unajua kuwa wapinzani hawatenewi haki?

Bora tuumie wote,sio kila siku wanaumia wafuasi wa upinzani kwa kutekwa,kupigwa,kubambikiziwa kesi,kupigwa risasi,kufungwa na hata kuuwawa!

Walau mbinyo ukiendelea kuwa mkali,wote tutapata maumivu!Na hiyo kwangu ni sawa mpaka pale uhuru na haki vitatamalaki kwa wote bila kujali itikadi zetu za kisiasa!



Ni zaidi ya miezi minne sasa akina Nusrat Henje wako mahabusu kwa kuimba "mungu ibariki chadema......",wakati uvccm hakuna aliyeguswa japo na wao waliimba "Mungu mmbariki Magufuli. ....."



Bora tuumie wote,waongeze na vikwazo kabisa!
Kama unategemea kuumia wote basi tegemea kuumia wachache tena sana.

Msikilize balozi wetu Belgium utapata habari mpya.

Hao wapinzani washindwe kuheshimu mamlaka wawe wanatukana tu mamlaka wanavyojisikia halafu serikali ikae tu kimya kwa kigezo cha demokrasia!!.
 
Huu ni mfumo wa kivuta Bangi kwani bado unashinda ukivuta Bangi hapo gheto kwa cyprian Musiba bado?
[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]Inaonekana Musiba kakuvutisha sana bangi pale chumbani kwake, maana huachagi kumtaja kwa mtindo huu,!

Hebu twambie alikuwa anakuvutisha bangi tu kweli au kuna mambo yenu ya faraga aliyomwambia mgombea wenu kwamba atawapa uhuru myafanya alikuwa anakufanyia?
 
Unabisha kwamba sio Binadamu wa Kwanza? niambie mwafrika gani aliwahi kumkoloni Mzungu...mpaka sasa mtu mweusi ameweza nini ikiwa hata uchaguzi mnashindwa kujiamini mnapigia Kura kwenye magodown mnazileta na mabegi kwenye vituo
Hiyo habari ya kura za magodown ni ya kutengeneza hapo ufipa.

Mimi nimepiga kura Bunju B palikuwa na amani na hakuna aliyefanya lolote kama zile picha za Mdee zinavyoonyesha.

Huyo dada tulimchoka mazima akawa anazomewa mikutanoni, katengeneza sinema ya kihindi akidhani itamsaidia.
 
Kila mtu ashinde mechi zake wewe umewekeza katika nchi kuwekewa vikwazo mimi nipo katika imani ya MAENDELEO makubwa miundo mbinu,kuongeza ajira kwa vijana kwa kuhakikisha viwanda vinastawi, Kuboresha sekta ya afya na mengine mengi mazuri yanayokuja...ila nyie mpo bunge la Ulaya ni utumwa mkubwa wa fikra.
Nioneshe hivyo viwanda na bidhaa gani tunazouza nje kutokana na hivyo viwanda
 
Bunge la Ulaya kwa kauli moja limeazimia kuifutia Tanzania misaada na mikopo yote ambayo imeomba kwenye Umoja wa Ulaya (EU) na mashirika yake.

Moja ya misaada mikubwa ambayo Tanzania imefutiwa ni ule wa ยฃ626M (sawa na TZS Trilioni 1.6) ambazo tumekuwa tukipewa kila mwaka tangu 2014 kwa ajili ya kuimarisha demokrasia, utawala bora, kujenga miundombinu na kusambaza nishati ya umeme vijijini.

EU imefikia uamuzi huo kwa madai kwamba kulikuwa na ukiukwaji wa demokrasia kwenye uchaguzi mkuu uliofanyika mwezi Oktoba mwaka huu. Pia vitendo vya uvunjaji wa haki za binadamu vinavyodaiwa kufanywa na vyombo vya dola na madai ya serikali kushindwa kudhibiti matukio ya ugaidi kusini mwa Tanzania.

Mwenyekiti wa Kamati ya mambo ya nje wa bunge la Ulaya (Chairman of the European Parliament Foreign Affairs Committee), David McAllister amesema pamoja na kuinyima Tanzania msaada huo wa TZS Trilioni 1.6 pia EU inafikiria kuiwekea Tanzania vikwazo vya kiuchumi (Economic sanctions) ikiwa ni pamoja na kuizuia Tanzania kufanya biashara na nchi yoyote ya Ulaya.

McAllister amesema vikwazo hivyo vikiwekwa havitaondolewa mpaka pale serikali ya Tanzania "itakapojicommit" kwa maandishi kuheshimu demokrasia, kuruhusu ushindani wenye usawa wa vyama vya siasa na kulinda haki za binadamu. Mjadala wa kuiwekea Tanzania vikwazo vya kiuchumi bado unaendelea.

BUNGE LA ULAYA LIELEZWE BILA KUPEPESA MOJA KWA HERUFI KUBWA KWAMBA: TANZANIA NI TAIFA HURU KWA ASILIMIA MIA MOJA na kwamba kimsingi ina haki zifuatazo:-

1) Haki na Demokrasia:

Kama ambavyo Tanzania haina mamlaka ya kuwatafsiria watu wa Ulaya haki na demokrasia zao, halikadhalika watu wa Ulaya hawana madaraka ya kuwatafsiria Watanzania haki na demokrasia zao. Tanzania ni Taifa huru kama ilivyo hizo nchi za Jumuiya ya Umoja wa Ulaya.

2) Hiyo inayodaiwa kuwa ni misaada haikuwa misaada:

Mtu akikupora shilingi 1,000 kwa mfano, halafu akaamua kukurudishia shilingi 250, hapo hajakupa msaada wowote.

Kwa miaka nenda rudi mataifa na mashirika ya Ulaya na nchi zingine zinazojiita zilizoendelea, walilazimisha Tanzania na nchi za Afrika kwa ujumla kuwapa wawekezaji wao kitu kilichoitwa "tax holidays" yaani misamaha ya kulipa kodi. Na hii ilikuwa ni uhalalishaji wa wizi, "tax holidays are a legal fraud."

Kampuni moja imewahi kufanya biashara Tanzania kwa miaka 18 bila kulipa kodi kwa madai ya kuwa ilikuwa haipati faida. Hiyo kweli inaingia akilini? Kwa nini kampuni ya kibiashara iendelee kufanya biashara miaka 18 wakati ilikuwa haipati faida?

Ukweli ni huu: Makampuni na mataifa ya Ulaya yamekuwa yanatuibia kupitia ukwepaji na misamaha ya kodi. Hivyo basi, hizo ยฃ626 milioni ambazo wamekuwa wanatupa tangu hiyo 2014, haikuwa ni msaada bali fedha zetu ambazi walitakiwa watulipe kama kodi.

Marekani, mathalani, bajeti yake yote ya Ulinzi inakuwa - "covered by corporate tax". Kodi za makampuni ni mipesa mingi sana. Halafu wao (the developed countries) wanalazimisha makampuni yao yasilipe kodi yanapowekeza nje ya nchi zao. What a con?

3) Jumuiya ya Ulaya haina demokrasia:

Kama kuna Jumuiya hapa duniani ambayo haina demokrasia na inaminya uhuru wa raia wake, basi ni Jumuiya ya Ulaya. 'Structure' ya Umoja wa Ulaya ni ya kitapeli ' per se.' Kwa nini ninasema hivyo:
Umoja wa Ulaya una mihimili mitatu.
(a) Bunge la Umoja wa Ulaya: Hili lina wabunge waliopigiwa kura na raia wa nchi wanazotoka.

(b) Halmashauri au 'Council'. Hapa kuna wajumbe walioteuliwa na Serikali za nchi wanachama.

(c) Kuna 'Commission' au Kamisheni. Wajumbe wa hii Commission wamejichagua wenyewe - ni 'self-appointed clique.'
Hawapigiwi kura; na raia wa Jumuiya ya Ulaya hawana njia ya kuwatoa hawa watu kwenye nyadhifa zao.
Utapeli mkubwa zaidi unakuja kwenye mgao wa madaraka. Hii Commission ndiyo inayotunga sheria na kuzipeleka Bungeni. Na hao wabunge hawaruhusiwi kubadili sentensi, neno hata nukta au koma kwenye mswaada. Wabunge kazi yao ni kupiga kura ya "ndiyo" au "hapana." Jamani hivi, hiyo ndiyo demokrasia ya rangi gani? Umoja wa Ulaya kweli wana miguu ya kusimamia na kutukosoa Watanzania?

4) Soko la Umoja wa Ulaya.

Umoja wa Ulaya, ni asilimia kumi na mbili tu (12%) ya Soko la Dunia. Hata kama wakitutenga, Tanzania au Afrika itakuwa na asilimia 88 (88%) ya soko la dunia la kufanya nalo biashara.

Ushauri Wangu.

Serikali ya Tanzania isitishike na maamuzi ya kikoloni yaliyotolewa na Umoja wa Ulaya. Tanzania siyo koloni, ni Taifa huru; na tupo huru milele (we are free forever."

Cha Kufanya:

  • Tanzania ifute misamaha yote ya kodi kwa makampuni ya nje.
  • Tanzania iendelee kukusanya kodi kwa dhati kama inavyofanya.

Matokeo yatakuwa ni Taifa kunufaika kwa sababu mirija ya waliokuwa wanatunyonya tutakuwa tumeikata.

Tanzania ilipata kuwa kisiwa wakati wa vita vya kulikomboa bara la Afrika; kwa maana ya kuwa hakuna nchi ambayo ilijitolea kwenye masuala ya ukombozi kwa upeo ambao Tanzania ilifanya - ndiyo kusema zama hizo tulikuwa ni kisiwa. Leo, tusihofu kuwa kisiwa tena kwenye vita hii ya kujikomboa kiuchumi. Hivyo,basi tutake tusitake tutakuwa ni kisiwa kwa sababu hakuna atatupigania, zaidi ya sisi wenyewe.
Kwa hiyo kauli za 'hatuwezi kujifanya kisiwa ni za kipuuzi sana.'
Hawa, yaani Umoja wa Ulaya inawauma kuona kuwa taifa ambalo walisadiki kuwa ni duni, si duni tena.Ila pamoja na juhudi zote hizi za EU kuturudisha nyuma,bado tunao marafiki wanaotambua juhudi zetu za kujiletea maendeleo.Sweden is a classic example, asanteni Sweden.





mkali@.co.uk
19/11/2020
 
Tukibaguana hivi, tukitesana na kuoneana hivi tutaishia kuwa nchi ya hovyo.
Mataifa makubwa macho yao yapo Afrika, wanafanya kila namna ili waendelee kuifaidi Africa.
Africa tuna shida sana ya uongozi kwani viongozi wengi ni wabinafsi sana na ni mafisadi.
Uroho wa madaraka ni moja ya chanzo kikubwa cha ufisafi Africa.

Mataifa makubwa yanatafua mianya ya kuingilia Afrika, na mianya hiyo tunaitengeneza wenyewe kwa kushindwa kuunganisha wanannchi.

Baadho ya watu wanaitazama hoja ya kuitafsiri demokeasia ya Afrika kama ni kigezo cha kutawala kidikteta.

Hulka ya binadamu ni kupenda kuwa uhuru,, lakini uhuru unatakiwa uwe na mipaka ambapo mipaka hiyo ndiyo sheria zetu.
Bado unakuta kiongozi wa Afrika anachagua sheria za kuziheshimu na zile zinazombana anatafuta namna ya kuziondoa au kuzibadilisha.
Ameshau kuwa na yeye pia ni binadamu ambaye uhuru wake una mipaka.(sheria zetu)

Mzungu anatumia vizuri utengano wetu (mianya) katika kuendelea kututawala.
Mfano Uzalendo wa kuwabambikia kesi kesi uonevu kuwapiga risasi wapinzani ni Uzalendo gani huo, Uhuru wa Nchi kufanya uchaguzi wa maigizo kuubaka kuunajisi kuulawiti uchaguzi mkuu huo ni uhuru gani? Kuwa Nchi huru siyo kupora haki za wapiga kura, sasa IGP kaja na visingizio vya ugaidi Zanzibar ili wapate kisingizio vya kuwabambikia kesi wapinzani hakuna maendeleo kwenye Nchi yenye vioja manyanyaso kwa wapinzani , ni vigumu Tanzania ipate maendeleo kwani pesa nyingi inapotelea kwenye matumizi ya kuminya demokrasia badala ya maendeleo
 
Kila mtu ashinde mechi zake wewe umewekeza katika nchi kuwekewa vikwazo mimi nipo katika imani ya MAENDELEO makubwa miundo mbinu,kuongeza ajira kwa vijana kwa kuhakikisha viwanda vinastawi, Kuboresha sekta ya afya na mengine mengi mazuri yanayokuja...ila nyie mpo bunge la Ulaya ni utumwa mkubwa wa fikra.
Ndio mnaloenda kuomba msaada mataga kama hamna shida ondoeni gari zote zilizoandikwa DFP ili muendeshe nchi kila ofisi ya mkuu wa mkoa DFP hujui kuwa mliomba mkasaidiwa
 
Hovyo! Kabisa. Mazuzu wanaojitekenya na kujichekesha wenyewe wanatia kichefuchefu!
Wanashindwaje kujua km hatua zozote za kuihujumu Tanzania na raia wake, zitamuathiri hata yeye na jamaa zake, kwa namna moja ama nyengine!

Wakati huu ambapo tunajitambua kuwa maendeleo yetu lazima yaletwe na jitihada za sisi wenyewe, badala ya kutegemea bakuli la wafadhili ni muhimu kila raia kuunga mkono jitihada hizo, na kuwa mstari wa mbele kutetea uhuru wetu kama taifa na utashi wetu kama binaadamu. Akili ya kuambiwa changanya na ya kwako!
Hatuoni wakutupa msendeleo shame on you
 
[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]Inaonekana Musiba kakuvutisha sana bangi pale chumbani kwake, maana huachagi kumtaja kwa mtindo huu,!

Hebu twambie alikuwa anakuvutisha bangi tu kweli au kuna mambo yenu ya faraga aliyomwambia mgombea wenu kwamba atawapa uhuru myafanya alikuwa anakufanyia?
Makonda Bashite alipiga kelele juu ya ushoga ni wabunge hao hao wa CCM walimpinga Bungeni wakiongozwa na kange lugola aliyekuwa waziri wa mambo ya ndani huku wewe ukiwa unaishi kinyumba na cyprian Musiba na Le mutuz ndiyo maana umejitoa fahamu zote unatetea ufedhuri uovu mateso manyanyaso uonevu wote wa CCM kwa wapinzani.
 
Mkuu unajua ICC inachunguza kesi za aina gani?

Then hawa jamaa hawajawahi kuidiscuss Africa in a positive way....haijawahi kutokea.......

Inawezekana kama nchi kuna mambo hayako sawa,ila kama jamii forum ninayoamini wengi ni watu wa kufuatilia mambo na kuyaelewa vizuri,ila kuendelea kushangilia na kufurahia nchi kusemwa vibaya,ukidhani ndiyo maisha yako yatakuwa bora ni kujidanganya tu.....

Mabadiliko yanaanza na sisi WaTz wenyewe,hakuna wakutusaidia maana kila mtu anaangalia maslahi yake
Kwa sababu waafrika tulio wengi hatujitambui
 
Yule mwenyekiti yuko bold vibaya sana. Amenufurahisha pale aliposema tunawezaje kutoa hela za walipa kodi wa ulaya kwa mtu ambae anadidimiza Haki za binadamu!!
๐Ÿ˜‚๐Ÿ˜‚๐Ÿ˜‚
Lissu akiwa uwanja mwingine wa medani๐Ÿ˜‚๐Ÿ˜‚๐Ÿ˜‚
Wacha wabweke tu watatulia wenyewe
Alafu raia tunachekelea na kushangilia kwel kwel duh! So sad
 
Mfuja jasho yupi
Pesa zote za wafuja jasho zinaliwa na akina Polepole kwa kisingizio cha kurejeshwa mfumo wa chama kimoja, CCM ndiyo chama pekee Duniani hutumia pesa nyingi kukandamiza demokrasia badala ya maendeleo
 
Back
Top Bottom