Kuna mambo hayahitaji elimu ya juu kujua kwamba Kuna mambo ya ajabu ajabu yanafanyika kwenye mpira wetu. Hivi hata kama Meneja wa uwanja hana taarifa kutoka kwa kamishina wa mchezo kwa uzoefu wake wa uendeshaji wa uwanja anajua kabisa ni lazima timu ngeni itakuja kufanya mazoezi.
Kwa busara tu ya kawaida tu alishindwa vipi kumtafuta kamishina wa mchezo huo na kumuuliza mbona bado yeye kama Meneja wa uwanja hapewi au hajapewa taarifa kuhusu ujio wa timu ambayo itakuwa mgeni kuja kufanya mazoezi??
Lakini pia baada ya hiyo sintofahamu kutokea hapo uwanjani kwanini yeye kama Meneja wa uwanja hakumtafuta kamishina wa mchezo au viongozi wa TFF Ili wampe go ahead ya kuiruhusu Simba kufanya mazoezi?? Hapa Kuna kitu hakipo sawa.
Why always Simba ndio anakuwa (victim) mhanga kwenye haya mambo ya figisu figisu kwenye mechi zake??
Anayetakiwa kumueleza mwenzie kuwa siku fulani timu fulani itafanya mazoezi sehemu fulani, ni nani? Asipofanya hivyo, nani anatakiwa kulaumiwa?
Kanuni inasema, mgeni atafanya mazoezi angalau mara moja kabla ya siku ya mechi. Sasa kabla ya siku ya mechi, inaweza ikawa a week before, two days before, one day before, au five days before etc. Mind you, anayepanga mazoezi afanye lini na akafanyie wapi ni club husika, inayotaka kufanya mazoezi hayo. In this regard, 51mba hakwepi lawama za kutosema lini na siku gani alitaka afanye mazoezi taifa.
Wewe mtu hujamwambia kama unakuja kufanya mazoezi, usipomkuta je...!!;
1. Nani atakufungulia mageti?
2. Nani atakuwashia taa za pitch?
3. Nani atakufanyia maandalizi ya kikanuni?
KWA HILI LALEO, 51MBA MMEZINGUA PAKUBWA. Kumbuka kuna gharama za maandalizi za;
1. Mashabiki (nauli, mahoteli, usafiri ndani ya Dar, etc)
2. Wadhamini (to mention few, mtoa tuzo ya mchezaji bora)
3. Watu wa TV na redio kwenye kurusha matangazo
4. Ball boys
5. Timu (in this regard Yanga)
ETC