Kampuni inaweza kuanzisha ligi ya mpira wa miguu tofauti na hii iliyo chini ya TFF?

Nahisi utakua haujafuatilia ishu nzima.

Michuano ilitaka timu zinazoshiriki ligi kuu nchini mwao ndiyo zishiriki ESL.

Fifa ikaona ESL itaua mvuto wa CL na kutokana na wingi wa pesa timu zingefocus na ESL kuliko CL.

Hivyo likawekwa zuio kwa kila atakayeshiriki hatocheza WC. Perez akasema watatengeneza WC yao.

Pia wakasema timu shiriki za ESL zitashushwa daraja mpaka la 5.

Hayo yote yangetokea ESL ingekua nini?
Wewe...yaani Hata kama wangesema wanazifuta FiFa hizo timu...
Inshort world cup Yao ingedorola,UCL Yao ingedorola Na Maligi Yao yote yangedorola...inshort FIFA ingekufa.

IMAGINE kina Messi,Ronaldo,Mbappe,Neymar,Pogba,Debruyne, Lewandowski,Neymar wanakiwasha ESL halafu kwenye UCL wapo kina Jacob Ramsey,Chris Wood,Adama Traore,Ante budimir

Unahisi watu watafuatilia Nini?
 
Unaweza ila timu zako zikishinda ligi hazitaweza kushiriki kwenye mashindano makubwa ya ambayo yanatambuliwa na vyama vya mipia vya Africa, Dunia n.k.

Bingwa wa Tanzania anatambuliwa na nchi nyingine za Africa na chama kinachotambuliwa na nchi nyingine Africa cha mpira ni TFF

Ila kama una pesa unaweza kuwalobby timu kubwa zijiunge kwenye ligi yako na TFF mka-lobby mkawa na watu wenu hata jina mkabadilisha Premier League England ilianza tu 1992 baada ya top teams kuamua ku-break away kutoka football league
 
Ligi ya timu 15 au siyo? Hiyo WC ingekua ya nchi ngapi?

Waanzishaji walilenga ESL iwe sawa na CL na siyo kua mbadala wa Serie A, La liga, Ligue 1 au EPL.

So timu inayoshiriki hii ligi ingejitoa kwenye mashindano yote yanayosimamiwa na FIFA yaani hamna Carabao wala FA, CS wala SC, unawajua wachezaji wangapi ambao hawataki kucheza kombe la dunia?
 
Hivi Azam Federation haitambuliki FIFA?
Lile ni Kombe la FA la TFF inayotambulika Fifa, sio mashindano ya Azam, Azam Ni Mfadhili na anaweza Kubadilika kama kule Uingereza FA kwa sasa inaitwa Emirates FA Cup mkataba ukiisha anaweza kuingia mwingine.
 
Mkitaka kuanzisha mnakuja na aina mpya ya mpira wa miguu, labda wachezaji huku 20 kule 20, Magolikipa 8, goli upana kutoka kibendera cha kona hadi kibendera cha Kona, hakuna kupiga Kona, utaipigia wapi sasa, na kitu cha tofauti halafu mnakiita jina la tofauti labda fuseball au utopoball
 
Sio lazima...

Umiseta ..
Umishumta..zote haziko chini ya Tff..

Binafsi nawaza kuanzisha ligi ya Vyuo..

Mfano Fainali udsm na Udom..
Hii Tff haitahusika..
Wanahusika BMT Tu..
Hata TFf iko chini ya BMT
Hapa Boss nimekuelewa vyema.
 
Mkitaka kuanzisha mnakuja na aina mpya ya mpira wa miguu, labda wachezaji huku 20 kule 20, Magolikipa 8, goli upana kutoka kibendera cha kona hadi kibendera cha Kona, hakuna kupiga Kona, utaipigia wapi sasa, na kitu cha tofauti halafu mnakiita jina la tofauti labda fuseball au utopoball
Mi naona uvumbuliwe Mpira mwingine ambapo timu tatu zinacheza uwanja mmoja.
Viwanja vinapanuliwa kidogo halafu magoli yanakuwepo Pande tatu Kila timu Na goli lake.
 
Mkitaka kuanzisha mnakuja na aina mpya ya mpira wa miguu, labda wachezaji huku 20 kule 20, Magolikipa 8, goli upana kutoka kibendera cha kona hadi kibendera cha Kona, hakuna kupiga Kona, utaipigia wapi sasa, na kitu cha tofauti halafu mnakiita jina la tofauti labda fuseball au utopoball
Kwani TFF au FIFA wana hati miliki ya mpira?
 
Mkitaka kuanzisha mnakuja na aina mpya ya mpira wa miguu, labda wachezaji huku 20 kule 20, Magolikipa 8, goli upana kutoka kibendera cha kona hadi kibendera cha Kona, hakuna kupiga Kona, utaipigia wapi sasa, na kitu cha tofauti halafu mnakiita jina la tofauti labda fuseball au utopoball
Kwani TFF au FIFA wana hati miliki ya mpira
Yes anzishen tu ligi yenu ila haitatambulika na FIFA wala CAF so mnakua kama.Ndondo la kishua
Umaweza shangaa ikawa na hadhi kuliko ligi za CAF, FIFA nk
 
Timu ikishiriki ligi ya Tz ikiwa ya kwanza au ya pili inaenda shiriki michuano ya CAF.

Timu ya daraja la kwanza ikishinda inakua promoted ligi kuu.

Hii ligi ya vyuo bingwa anapata nini? Si inakua haina tofauti na ligi za ng'ombe zilizosambaa mitaani?
Hizi Ligi ni za ng'ombe ni kwa sababu uwekezaji mdogo. Unaweza ukaanzisha hadi timu za TFF zikahamia kwenye ligi yako.
 
Unaweza ila timu zako zikishinda ligi hazitaweza kushiriki kwenye mashindano makubwa ya ambayo yanatambuliwa na vyama vya mipia vya Africa, Dunia n.k.

Bingwa wa Tanzania anatambuliwa na nchi nyingine za Africa na chama kinachotambuliwa na nchi nyingine Africa cha mpira ni TFF

Ila kama una pesa unaweza kuwalobby timu kubwa zijiunge kwenye ligi yako na TFF mka-lobby mkawa na watu wenu hata jina mkabadilisha Premier League England ilianza tu 1992 baada ya top teams kuamua ku-break away kutoka football league
Nimekupata vyema.
 
Hizi Ligi ni za ng'ombe ni kwa sababu uwekezaji mdogo. Unaweza ukaanzisha hadi timu za TFF zikahamia kwenye ligi yako.
Tatizo timu za TFF zikihamia ndiyo hayo ya ESL yatakapotokea.

Yaani labda ufanye uwekezaji na kuiboresha ligi iliyopo tayari au upigane ianzishwe mpya ila iwe chini ya TFF kwahiyo CAF hawatoziadhibu timu zitakazoshiriki.
 
Siyo kuziadhibu. Zi zinajitoa TFF kwa amani tu. Kwamba kuna ligi tumeamua kwenda kushiriki.
 
Hebu fikiria.

Timu kama Simba au Yanga kwa historia zilizonazo zinaweza kubali kujitoa mashindano yote yaliyo chini ya FIFA na kwenda ligi daraja la tano?

Ila kwakua unasisitiza hebu execute plan tuone.
 
Siyo
Hebu fikiria.
Timu kama Simba au Yanga kwa histoEzekanAwlin zilizonazo zinaweza kubali kujitoa mashindano yote yaliyo chini ya FIFA na kwenda ligi daraja la tano?

Ila kwakua unasisitiza hebu execute plan tuone.
Siyo Nasisitiza. Nimeuliza hilo suala linawezekana. Hujatoa sababu za kuonyesha kuwa haiwezekani. Nataka kujua kama TFF au vyama vya mpira vya wilaya na mikoa vimepewa Monopoly ya shughuli za mpira Tanzania? Mtu anaweza kuendesha shughuli za mpira nje ya watu hao?
 
Mbona nimekujibu haiwezekani kama lengo lako ni timu zilizo chini ya tff kushiriki.

Na kila mtu kakupa jibu hilo hilo na mfano wa European Super League nikakupa.
 
Back
Top Bottom