Kampuni inaweza kuanzisha ligi ya mpira wa miguu tofauti na hii iliyo chini ya TFF?

Mbona nimekujibu haiwezekani kama lengo lako ni timu zilizo chini ya tff kushiriki.

Na kila mtu kakupa jibu hilo hilo na mfano wa European Super League nikakupa.
Kwahiyo timu ikiwa chini ya TFF haiwezi kutoka? Aho ESL si kwamba haikuwezekanaa kisheria ni nguvu tu za mashabiki ndiyo zimezuia.
 
Kamuulize perez na super league yake iliishia wapi na hajaambulia hata mia mamaeeeee.......na wadhamini wake chali
 
Boris akapigilia msumari wa mwisho kwenye jeneza la perez 😀😀😀😀😀
 
Hakuna mchezaji hata mmoja alietaka iyo esl kwanza
 
Kwahiyo timu ikiwa chini ya TFF haiwezi kutoka? Aho ESL si kwamba haikuwezekanaa kisheria ni nguvu tu za mashabiki ndiyo zimezuia.
Inabidi aongezeke mwingine wa kukuelewesha naona kabisa jamaa peke yake hatoweza ............
 
Haikuwa FIFA ila ni UEFA ndiyo waliokuwa against nalo FIFA walikuwa against na utaratibu tu wa namna ligi itakavyochezwa.

Kuna kipindi kuna sekeseke la kuundwa kwa football federation nyingine duniani kwajili ya kucompete na FIFA lakini sijui liliishia wapi. Walitaka Football iwe kama boxing kuwe na mashirikisho mengi lakini hiyo move ilikufa.
 
Inawezeiana lakini inabidi mkubaliane kua mnahitaji kushawishi sana vilabu viachane na fifa maana fifa haina mamlaka ya kuzuia biashara nyingine sema itabidi uweoe mpunga mwingi sanaaaaaaa hadi ushawishi dunia iitenge fifa
 
Kwahiyo timu ikiwa chini ya TFF haiwezi kutoka? Aho ESL si kwamba haikuwezekanaa kisheria ni nguvu tu za mashabiki ndiyo zimezuia.
Mashabiki?

Mbona tamko la kwamba mchezaji atakayeshiriki ESL anakua amejitoa kushiriki world cup, copa america na euro halikutoka kwa mashabiki?

Tamko la kuzishusha timu shiriki kwenda daraja la tano halikutoka kwa mashabiki.

Adhabu za fedha zilizotolewa hazijatolewa na mashabiki.
 
Yaani timu shiriki mpaka leo bado zinaadhibiwa
Hahahahahaha ed akaamua kukimbia kiti mwenyewe......

Uingereza wana nguvu sana kwenye soka la ulaya perez alipaswa kula sahani moja na hawa watu yule boris angekubali tu cl ilikua inakufa
 
Sahihi. Uefa
 
Hao ni FIFA walikuwa wanalinda ugali wao nafikiri. Lakini kuna sheria inayokataza timu kujitoa kwenye mashindano ya FIFA au UEFA na kwenda kuingia kwenye mashindano mengine? Au tuseme nchi hazitaki world cup inayosimamiwa na FIFA. Hivi Football wakati wa Olympic, inakuwa chini ya FIFA?
 
Ndiyo mimi nauliza kitu hichi hasa. Mashirikisho ya mpira kama UEFA, TFF, au vyama vya mikoa. Vinaweza kuwa zaidi ya kimoja. Yaani uunde TFF yako na ushawishi timu zishiriki huko na kwenye ligi utayoanzisha.

Hivi FIFA wana mamlaka yoyote kwenye Mchezo wa soka unaopigwa wakati wa Olympics?
 
Ni ngumu sana
 
Sio lazima...

Umiseta ..
Umishumta..zote haziko chini ya Tff..

Binafsi nawaza kuanzisha ligi ya Vyuo..

Mfano Fainali udsm na Udom..
Hii Tff haitahusika..
Wanahusika BMT Tu..
Hata TFf iko chini ya BMT
Nutakuunga mkono boss. Hizi ligi zipo sana na sijawahi ona mkono wa TFF, ni mwendo wa kuongea na serikali za wanafunzi kwanza fedha za uendeshaji hutolewa na vyuo. Wewe unatoa zawadi tu
 
Yes , FIFA wanayo Mamlaka kwenye Olimpiki. Ndiyo maana Olimpiki wanashiriki Vijana wa Chini ya miaka 23 na wakubwa watatu tuu na nia ni kutoifanya Olimpiki iwe World Cup.

Messi alitwaa Medali ya Dhahabu kwenye Olimpiki mwaka 2006 lakini hadi Karibuni ilikuwa inahesabika hajawahi kutwaa Kombe kubwa duniani.

Soka ya kwenye Olimpiki haina mvuto kihivyo
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…