Kampuni Kutoka China Kujenga Daraja la Dar- Zanzibar

Hata kulijadili hili ni ujinga sana, hata haiingii akilini, tuna changamoto nyingi sana zinahitaji utatuzi.

Anga na maji vinatosha!!
 
Upembuzi yakinifu ni hatua muhimu sana kabla ya kufanya uwekezaji. Kuna wakati tulinunua boti ya kufanya safari za Dar Bagamoyo bila upembuzi yakinifu, bila shaka tunajua hasara tuliyopata.
Safi 2050 daraja itaanza kujengwa nguzo ya kwanza bagamoyo!
 

Mkuu kwani hawajui...hii mipango inahitaji mwamba jasiri...mwenye uthubutu...Mundele anatisha anakupa proposal hupangui..unaitikia tu..Yes sir na iwe hivyo..
 
Mods unganisha huu uzi tayari Kuna Uzi humu uko page ya 5
 
 

Payback period yake ni muda gani? Account rate return inasemaje ili kujua iyo Capital Expenditure itakuwa na faida zipi? Feasibility na Appraisal zake zimekaaje? Sio tu mtu anatoa majibu kiholela afu nawe unabeba unayaleta kwenye hii platform aisee
 
Mimi ninaunga Mkono Serikali kuunda Daraja litakalo unganisha Dar na Zanzibar ni maendeleo makubwa tutapata wageni wengi kuja kutembelea na tutapata pesa za kigeni nyingi kwa ajili ya hilo daraja la Dar to Unguja wanaopinga wache wapinge hawapendi maendeleo ya nchi yetu. Ona Video wenzetu wazungu wanavyo endelea kutengeneza madaraja yanayopita juu ya bahari na chini ya bahari. Sisi tunapinga paipo an limu yoyote ile.

The Insane Scale of Europe’s New Mega-Tunnel​


Türkiye to open world’s longest and tallest suspension bridge in Canakkale​


World's longest sea bridge - BBC News​


How the world's longest underwater tunnel was built - Alex Gendler​


Inside The World’s First Undersea Roundabout​


Eurasia Tunnel: Tunnel beneath Bosphorus is now in business​


The Longest Bridge In The World​


 
Daraja la nini? Jamani, tuna mambo makubwa mno ya kufanya, daraja la nini?
 
Mradi usiokuwa na tija kabisaaaa!.
Kwa kuwa unajengwa kwa mpango wa PPP, hauna tabu yoyote, kila jambo linalofanyika ni endeleo kwa taifa letu, chochote cha kujenga iwe kiwanda au lolote lile ni MAENDELEO.
#stop ignorant!
 
Payback period yake ni muda gani? Account rate return inasemaje ili kujua iyo Capital Expenditure itakuwa na faida zipi? Feasibility na Appraisal zake zimekaaje? Sio tu mtu anatoa majibu kiholela afu nawe unabeba unayaleta kwenye hii platform aisee
Wewe upinde umetokea wapi? Haya maswali unamuuliza Nani? Sometimes kama hujui kitu kaa kimya lofa wewe..
Heading inasema "kampuni ya China yaonesha nia" unauliza feasibility wakati kilakitu bado hakijakaa sawa?
 
Tuna hayo mawazo kaka we acha tu.
 
Zanzibar ina hela gani za kujenga daraja wakati bajeti ya nchi nzima ya Zanzibar 2022/2023 ilikuwa Tsh trill. 2.5 kwanza itaweka dhamana ipi kuchukua mkopo wa bank labda kama alivyowahi kusema J.k kuwa walichonacho ni virungu vya polisi tu.
True Zanzibar ukitoa watalii hakuna cha maaana.
 
Naomba unisaidie! Ni faida gani Watanzania bara watazipata kutokana na daraja hilo tofauti na sasa?
 
Sina wasi wasi hili daraja ni ndoto tu halitajengwa katika karne hii. Wachilia mbali mambo ya gharama eneo linapotaka kujengwa litahitaji mipango mikubwa sana. Ikitajwa kujengwa baina ya Dar es salaam na Zanzibar lazima daraja hilo litaingia./Litatokea maeneo ya mpakani baina ya dAR na Bagamoyo sijui ni Bunju au wapi pale.Eneo hilo bado lina mawimbi makali ya bahari na bahari inapochafuka ndio kazi zaidi. Hilo daraja itabidi liwe pana ili kutoa njia za uokozi na si njia mbili tu.Tuseme kumetokea kimbunga cha ghafla na gari ziko katikati ya daraja.Lazima ziwe na njia ya kukatisha safari na kurudi ilikotoka.Haitowezekana gari ikishaelelekea Zanzibar basi iwe ni kwenda tu.Hii siku ikitokea athari hiyo ya hali mbaya basi tutapoteza watu wengi baharini.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…