Kampuni ya Energizer imeanza kutengeneza Simu ya Smartphone Yenye Uwezo wa kukaa na Chaji kwa Muda wa usiopungua Siku 50 bila kucharge tena

Simu kilo 2 nani abebe, hiyo sio business
 
Iliishia charge inachargiwa kwa muda gani? Usikute ndio unakaa siku 15 bila simu kisa iko charge 😂😂
By the way ni nzuri kwa watu wa adventures and tourists
 
Maendeleo ya Teknolojia

Huwa najiuliza Kuna Siku nasi Tanzania tunaweza kufikia uvumbuzi wa namna hiyo?

Maana gari tu la Masoud Kipanya (KP) Serikali ilishindwa kumsapoti.
Tatizo alianza kutengeneza bila kuangalia hitaji la soko .huaanzii tu kutengeneza soko kwanza lipo?Watu wangeona Ina soko wafanyabiasha binafsi wenye pesa wangejiunga naye huo mradi sio serikali .Au kama angependa kukomaa na anaamini hiyo gari yake itakuwa na soko angeenda kukopa Benki andeleze huo mradi wake
 
Pamoja na hilo Mkuu ila jitihada za Serikali zingeonekana kwenye kumsapoti as Serikali ina tools zote za kumfanya jamaa ubunifu wake ujue.

Nakumbuka wakati tupo Sekondari, Kuna Dogo wa form II aliwahi kubuni helicopter akiwa kwenye kazi za workshop as Shule yetu ilikuwa ya mchepuo wa ufundi Kwa O'level

Lakini pamoja na ubunifu ule, Serikali haikuwahi kumsapoti Kwa chochote zaidi ya kumwambia hana license ya kufanya ule ubunifu 🙌

Kama hali ni hiyo, unadhani tutapata nafasi ya kutengeneza vyetu?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…