Kampuni ya kubet TZ (Pigabet) ni wezi wakubwa, nimekula mkeka mil. 6 online, haitoki eti kuna shida ya mtandao siku ya 10 leo

 

Attachments

Mmefanya vyema kuliweka hili vizuri.
 
Jina lenyewe tu, piga bet unategemea nini.
 
Mkuu, mbona namba uliyoweka hapa kwenye kampuni yetu ya PigaBet hatuifahamu japokuwa tunawapiga kweli kweli wa tz, ID yenyewe haina verification, hatari na nusu
 
Pole sana mkuu, sisi ni wapigaji kama lilivyo jina letu! Siku nyingine muwege mnaacha ujinga[emoji23][emoji23][emoji23]

Eti turudishe pesa, halafu sisi ka pesa kenu ka kunywea tukatoe wapi! Emu fanyeni kubet sisi tupate pesa ya kujitupia kasino na warembo wakali[emoji41]
 
Waambie una mpango wa kupeleka hili suala mahakamani.
Tafuta hata wakili awapigie simu.

Wakiendelea, nenda mahakamani, wanaweza kutoa zaidi ya hiyo.
 
Jina lenyewe tuu limekaa kiwizi. Kuna kampuni za kubeti zenye reputation nzuri tuu umeziacha ukafuata Piga beti ukapigwe!
 
Kama una evidence za kutosha wafungulie kesi mkuu. Kuna Father mmoja kitaa alishakutana na hii kwenye kampuni flan aliwapiga KO mahakamani akalipwa 100m+.
 
Kwann msizuie pia kudeposit?
 
Ndugu wateja
TTungependa kuomba radhi kwa usumbufu uliojitokeza katika upande mfumo wa utoaji wa fedha(miamala) kupitia njia ya mtandao uliojitokeza kwa wiki kadhaa. (tigo,voda,airtel,halotel).

Tunapenda kuwafahamisha kuwa changamoto hio imefanikiwa kutatulika na huduma imerejea vyema kama awali.

Pigabet inawahakikishia wateja wetu wote kuwa fedha zao zipo salama ndani ya waleti zao za Pigabet hivyo basi kwasasa wataweza kutoa pesa muda wowote masaa 24 kupitia mtandao husika

Asante!


PigaBet Management
 
Jackpot yenu huwa mnatoa bonus kuanzia game ngapi?
 
hakuna wezi kama hawa
Mimi niliweka 80,000 nikabeti mikeka mingine ikachanika mingine ikashinda, mpaka usiku nikwa na 120,000 Sasa nikasema nipunguze hapo hata 30,000 TU alafu nyingine niache. chakushangaza pesa haitoki, nikawatafuta kwenye chat live wakaniambia wanashughulikia nikawatafuta kwenye Instagram bado sound ni zile zile . siku moja wakaniambia niongeze (deposit) kiasi chochote alafu ni kibetia ndipo hiyo pesa itatoka lakini wapi, mwingine akaniambia mara nitume tarifa zangu binafsi za miamala ya mpesa nikatuma pamoja na kitambulisho lakini wapi. nikawa nawauliza Sasa mbona wakati na_deposit hamkuniuliza kuhusu vitambulisho Sasa hivi ndio mnauliza? majibu eti ni utaribu wa betway.
 
Hakuna kampuni ya kubeti wezi)majambazi wa waziwazi kama hawa betway. ni Bora mtu ukatumia kampuni waaminidu kama sportpesa ambao pesa yako unaipata chapu
 
Hakuna kampuni ya kubeti wezi)majambazi wa waziwazi kama hawa betway. ni Bora mtu ukatumia kampuni waaminidu kama sportpesa ambao pesa yako unaipata chapu
Betway Wana Nigeria matapeli
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…