Kamuachisha shule binti yangu, kamuoa. Anasema hakuna wa kumfanya lolote Serikali hii

Kamuachisha shule binti yangu, kamuoa. Anasema hakuna wa kumfanya lolote Serikali hii

Mbona kama unaandika kwa woga? Andika no za simu vizuri ili usaidiwe!
 
Huyo jamaaa si akamatwe afymuliwe rinda asee apate adabu
 
Yule mganga anayefanya watu Kama Hawa wajinga kuwa mahanithi bado yupo hapo Handeni?
Kuna issue huku Mwanza.
 
Kwanza tuanzie hapa mtoto anasemaje, ukute ukuni umemkolea na kataka mwenyewe ww unaangaika tulia utakufa kabla ya Siku zako.

Ukimpeleka polisi mtoto akisema mimi nataka utafanya nn, sidhani kama uyo mwamba kamfungia mwanao ndani
Hakunaga kitu kama icho chief. Kuwa mzazi
 
Mama kama jamaa ana maisha mazuri mwache tu mtoto wako jifanye kama hujui ,navyomfikiria huyo mtoto wako hana uwezo wa kufika mahali kielimu bora aanze maisha tu na dingii
Ila kweli..mwanafunzi anayependa shule huwa anaonekana tu...! 😀! Muda wote anawaza kusoma..sijui lkin
 
Kwanza tuanzie hapa mtoto anasemaje, ukute ukuni umemkolea na kataka mwenyewe ww unaangaika tulia utakufa kabla ya Siku zako.

Ukimpeleka polisi mtoto akisema mimi nataka utafanya nn, sidhani kama uyo mwamba kamfungia mwanao ndani
Hata Kama mtoto anataka,kwa kuwa ni mwanafunzi na kama bado Ni minor sheria itafuata mkondo wake sahihi.

Sent from my TECNO B1f using JamiiForums mobile app
 
Habari za leo wapendwa. Sijui ni dharau kwa serikali ama siasa moe sielewi. Kuna baba mtu mzima ana watoto wakubwa.

Binti yangu alikuwa anasoma Sengerema kidato cha sita. Huyo baba kamuachisha binti yangu shule na kumuweka ndani kinyumba. Huyo baba anasema Serikali hii hakuna wa kumfanya chochote hata twende wapi hawezi kukamatwa.

Mimi mama yake ni mgonjwa nahudhuria dialysis Bugando maana mie ni mgonjwa wa figo.

Katumia udhaifu wangu kunifanyia hivyo. Nina imani na Serikali iliyoko madarakani na wapigania haki popote walipo kuwa watanisaidia.

Mimi niko Mwanza
Namba yangu ya Simu ni 0745 317 ***
Jina langu ni Sekunda
Binti yangu ni Ph***

Aliyemuachisha shule anaitwa Razaro
Namba yake ya simu ni 0757262*** na yuko hapa hapa Mwanza

Naomba serikali ioneshe kwamba ipo. Katika utawala huu nina imani mama atatupigania.
Mama naona kuna mambo mengi unaficha Wa sukuma mna tabia ya kuchukua mali za watu arafu mnageuka mkishinda kugawana hiyo mali, unatelekeza mtoto akiolewa unajitokeza kudai eti katoroshwa, huenda hata huyu bint kakaa zaidi ya miaka miwili bila kusoma kwa kukosa msaada wa elimu,
Kwahiyo funguka vizuri usiwe muongo wakusikia tetezi tu.....mbona unaficha hata number za muhusika kama kweli unataka msaada.
 
Umeficha maelezo mengi na namba, usingeziweka kabisa maana nia ya kuziweka ni kuthibitisha unachosema ili usaidiwe.

Fuata taratibu kwenye vyombo vya sheria utapata msaada.
 
Dah pole sana mkuu lakin pia najiuliza binti yenu akiwa form six anashindwa kujitambua kweli na kuwaonea huruma ninyi wazazi wake akubali kuakatishwa masomo
Huyo hajakatishwa masomo. Kaacha shule, kwa hiari yake!!
 
Nenda kwa Mkuu wa wilaya, panda ngazi ya Mkoa peleka hilo suala kwanza serikali inapambana kupunguza suala la wanafunzi kukatishwa masomo.acha kuwa na moyo wa unyonge simama kupigania Haki yako.
 
Hatua ya Kwanza.....alimuachisha shule......hatua ya pili alimuoa( je Nani kabariki ndoa hiyo na nyinyi wazazi mlikuwa wapiii mpaka ndoa inapita, Nani kachukua mahaliii..) mmpaka Sasa wamekaa MDA ganiii kwenye ndoaa.....

Watuhumiwa wafuatao wanaitajika
Mzazi
Walezi
Shekh/ mchungaji
Mwalimu mkuu WA shule
Muhisika WA tendo/ mume
Bint WA shule
Mshenga
Mtoa Cheti cha ndoa
Hawa wataisaidia polisi....na itakuwa fundisho
 
Back
Top Bottom