Kamusi ya kichaga cha Marangu kwenda kiswahili

Kamusi ya kichaga cha Marangu kwenda kiswahili

Mae inatumika wapi kama mwanaume?

Najua kibosho "mbe" inatumika nadhani kwa mtoto wa kwanza nadhani hata akiwa wakike.

min -me sijui nipo sawa hapi mnama, nirekebishe kama nimekosea.

Ila kivunjo "mbe" ni mwanaume.
Katika kumbukumbu zangu kuna mahali tu sijui wapi mae kama sio mae basi ni ile neno "MA" mfano mwanamke kwenye ukoo wa chuwa unaeza muita Machuwa kwa vile ni mwanamke kutoka ukoo wa chuwa sasa kuna maeneo hii machuwa ni mwanaume 🤔🤔
 
Katika kumbukumbu zangu kuna mahali tu sijui wapi mae kama sio mae basi ni ile neno "MA" mfano mwanamke kwenye ukoo wa chuwa unaeza muita Machuwa kwa vile ni mwanamke kutoka ukoo wa chuwa sasa kuna maeneo hii machuwa ni mwanaume 🤔🤔
Hilo nadhani ni uchaga wote wana huo utaratibu. Mwanamke kuitwa "ma" mbele ya jina lake la ukoo.

Ila kama ulivyosema kuna koo za kichanga zinaanza na hiyo ma.
 
Yeah nilitaka kumwambia asiseme hutu haika amalizie na title ya anaemwambia haika.

Kama ni baba/babu/mume unasema "haika mbe"
Bibi/mama "haika mae"
Kaka/dada "haika awae"
Mtoto wa kwanza anatumia mbee wa pili anatumia saa Mimi naitwa ndeyanka(jina halisi kabisa) opposite ya manka na mzee wangu ananiita saa huwa najikuta kama nimepewa bonge la heshima kama sir alex fegurson 😎😎🙌
 
Aichi—Anajua

iachikyia--Kujenga

Ichele—Kichaga

Ichondi- --- Kondoo

Iikyelyia—Kuogelea

Ikawilyia—Kupalilia

Ilyingoi---Jogoo

inyi—Mimi

Ipalipali- --Bahari

Ipore---Yai

Irikoso—Taji

Isewa—Kibuyu

Itukuo—Kushangaa

Iwuwu—Kuona makengeza

Iyesho---- Majaribu

Kiamba---Shamba

Kyasaka—Ugenini (Mswahili)

Kyiaatyi—nafasi

Kyo_kyimaryu—Ndiyo sababu

Kyuwere—Kumebakia nafasi ndugu

Lakucha—Usiku mwema

Linyala—Kuzarau

Maakulembecherye—Unafiki

Mapore—Makande

Mapuchi—Mawingu

Masaanga—Mataifa

Matu matu—Tafadhali

Mbuya---Rafiki

Mchola--Kichochoro

Mkuuchu—Kiburi

Mkuuma---Upepo

Mlenya—Mchanga

mmesa—Adui Mtiima—Giza nono

Mmmbaryi—Jua

Momrasa—Jirani

Momu- hori la ng’ombe

Msasariko—Masazo

Msotsa---Kushuka

Na-Ngoseraa—Na zaidi

Ndekye—Ndege

Nduwa-- Dimbwi

Ngambura--kipande cha nyama

Njoonyi—Ngozi

Nyi Kryirumi—Ni Utukufu

ote=hapana

Parapara—barabara

Pfinya—Nguvu

Rumbu—Mdomo

Sera’—Mgomba mchanga

Shira’—vita

Tao—Ng’ombe jike

Tikira- sogea

ukou=Jana

Ulakuso—Tafadhali

Ulowo—Habari

Unga—msoo

Unyamari’—Dhambi

Ushanguny—Usoni

Walutsa—Geuza

Wanda—chini
Kamusi ulitakiwa uweke maneno ya kuombea ndoa ingependeza zaidi!
 
Hii nitaisoma mnama kwa sababu kama ukoo wangu una utata sana kihistoria
Pamoja sana mnama.

Huko kuna historia za kustaajabisha sana za koo za kichagga, utajua kwanini mfano unakuta kuna Mushi wa Uru, Kibosho, Kirua na Marangu. Utajua kwanini kuna Mushi, Munisi, Munishi, Mosha, Moshi, Chaki, Mchaki na utajua ukoo wa Mboro uliishia wapi.

Pia utazijua koo za kichagga ambazo sio maarufu na wengi hawazijui kama Chacky, Tillya n.k
 
Back
Top Bottom