Kujitenga na siasa ni wenda wazimu ila kwa siasa za bongo na ccm ni mwenda wazimu tu asiyejitenga nayo ili nyinyi maccm muendelee
Na wanaojitenga wapeni uhuru, na huo uhuru ndio unaokamilisha jibu la kwamba, October 29 hakuna uchaguzi
JIBU la kwamba, October 29 hakuna uchaguzi ni UONGO!
Ilitakiwa kusema October 29 kuna baadhi ya watanzania ambao kwa sababu zao binafsi ambazo wao wanaona ni sahihi wameamua kuwa hawatoshiriki uchaguzi!
Kushiriki uchaguzi ni haki ya msingi kwa kila raia ila akiamua kwa hiyari yake mwenyewe bila kulazimishwa na mtu yoyote kutoshiriki uchaguzi hakuna sheria inayomlazimisha kushiriki uchaguzi.
Mimi binafsi mara ya kwanza na ya mwisho kupiga kura ni mwaka 2000.
Na nakumbuka urais nilimchagua professor Ibrahim Haruna Lipumba wa chama cha CUF.
Ubunge nilimchagua Omar Said Mbalamwezi mgombea ubunge wa CUF jimbo la Mwanza mjini (siku hizi ni Nyamagana)
Udiwani nilimchagua Hussein Chilwan mgombea udiwani wa CUF kata ya Pamba Mwanza mjini.
Miaka kama miwili baadae nilijiwekea msimamo kwamba SITAPIGA KURA KATIKA UCHAGUZI WA KIDEMOKRASIA MAISHA YANGU YOTE na ndio msimamo wangu hadi leo na sina mpango wa kubadilika.
Kwahiyo Mimi kwa sababu zangu binafsi sina mpango wa kupiga kura October 29 ,2025 lakini haimaanishi kwamba naunga mkono NO REFORMS NO ELECTION kwa sababu reforms ninazoziamini mimi najua haziwezi kupatikana katika nchi kama ya Tanzania ndani ya miaka kama 120 ijayo ila Allaah aamue kuleta nusura yake.
Lakini nitatii na kuheshimu serikali ya chama chochote itakayokuwa madarakani na ikiwa na rais wa dini yoyote na jinsia yoyote, na sitapekuapekua kutaka kujua serikali imeingiaje madarakani.
Habari ya serikali imeiba kura au haijaiba, uchaguzi ulikuwa huru au hakuna uhuru , hizi habari Mimi hazinihusu kwasababu hata serikali isipoiba kura, na hata uchaguzi ukiwa huru na wa haki kabisa, bado utawala uliopo hapa Tanzania na nchi nyingine nyingi kwa dunia ya sasa ni kinyume na mfumo ambao Allaah kauchagua kuweza kuongoza dunia na viumbe wanaoishi duniani hiyo ndio sababu ya Mimi kutojishuhhulisha na siasa za KIDEMOKRASIA lakini nitaitii , kuitambua na kuiheshimu serikali iliyopo madarakani na bila kujali, inaongozwa na mtu wa chama gani, dini gani, wala jinsia gani kwa sababu serikali ipo kwa ajili ya kuangalia maslahi mapana ya watu wa dini zote, vyama vyote na jinisia zote.
Ahsante sana kwa kunisoma.