Kanisa Katoliki Jimbo la Rulenge Ngara lafungwa kwa uvamizi

Kanisa Katoliki Jimbo la Rulenge Ngara lafungwa kwa uvamizi

Kanisa Katoliki halina shida na mtu yeyote, halitalipa kisasi kwa yeyote, halitakasirika, wala halitahuzunishwa kwa waliyofanyiwa.

Huwa wanasamehe, hawakumbuki ubaya waliotendewa. Lakini kusema ukweli ili kuwaokoa watanganyika, kamwe halitaacha.
 
ccm ni wapumbavu sana wanafikir kutuma vibaka ndio itazuia kusoma waraka wa TEC.
Kwani wamebainika au ni hisia za kale kama Hayati Bob Male?

Hisia nyingine za kale labda Kanisa hilo limetuma hao wahuni afu na Leo ratiba ya kusoma Waraka..aiseee
 
CCM inahusiana nini na hao wavamizi?
Wewe unaamini waliofanya tukio hilo ni vibaka au majambazi? Jambazi gani ataingia mahali afanye uharibifu na asiibe chochote?

Vituko hivi yumkini vina mkono wa CCM na Serikali yake ili kuwavunja moyo maaskofu wa Kanisa Katoliki waliosimama wazi na kupinga ule mkataba wa kishenzi wa DP World.

Tutarajie mengi zaidi ya haya dhidi ya Kanisa Katoliki na viongozi wake LAKINI Kanisa lililojengwa juu ya Mwamba (Petra) halitayumba wala kuanguka, maana mjenzi ni Kristo mwenyewe.
 
Washukiwa wakwanza wa hilo tukio wawe serikali, CCM na DP World
Jamani mnakosea msipotoshe.Kuna wakati kuna kanisa la RC huko huko kanda ya ziwa ilivamiwa hivi na mambo ya DPW yalikuwa bado. Vyombo viachwe vichunguze huenda kuna uhusiano wa tukio hili na lile la awali au vinginevyo.Msilete taharuki.Ccm ina madhaifu yake lakini ndio chama tawala sidhani kama wamekosa weledi kiasi hicho.Hapana
 
Kanisa Katoliki hakika linadhihirisha unyenyekevu wa moyo.

Ukisoma katika andiko hilo kuna sehemu wanahimiza. Naomba kunukuu;
"Kwa kipindi hicho jamii nzima ya waumini katika Jimbo la Rulenge - Ngara inahimizwa kusali,kufunga, kufanya toba na malipizi kwa Mwenyenzi Mungu ili abadilishe mioyo ya watu wenye nia ovu kwa mambo matakatifu"

Pamoja na najisi iliyofanyika na watu hao, kanisa haliwaombei laana. Kanisa haliwaombei kifo, wala haiitishi Albadiri kwa ajili ya kuwaombea mateso.

Bali kanisa linaomba ili Mwenyenzi Mungu aweze kubadili mioyo yao. Nia zao mbaya zikapate kutoweka na wapate kumrudia Mungu kwa moyo wa toba.

Hapa kanisa linaiishi neno la Mungu la kutotaka kulaani ili tusijelaaniwa.

Ee Mwenyenzi Mungu wasamehe watu hao na mioyo yao ikajihisi wenye kukosa na wapate kurudi kwako tena.

Amen.
 
Sijauelewa mstari unaosema "...malipizi kwa mwenyezi Mungu"
 
Nyei mnaosema kijani imehusika je mnaukakika na mkiitwa mahakamani mnao ushahidi pasipo shaka?

Tuliachie kazi jeshi la polisi,pia ni wakati sasa makanisa yaweke walinzi pamoja na cctv camera.
 
Hii dini ya maana Sana,hawajasema wanamvimbisha mtu tumbo Wala kusoma Alba stini ya kumshitakia mnyaazi mungu walio fanya ufedhuli wafe kifo kibaya
 
Sawa, ila ikimbukwe kwamba...

Hoja kuu zinazohitaji majibu ni hizi hapa

1.) Tofauti ya ‘Makubaliano’ na ‘Mkataba’ ni ipi hasa kiasi mseme ule sio mkataba, kwamba ni makubaliano tu ya awali, na je Mkataba huo (makubaliano hayo) ni wa miaka mingapi? (UKOMO)

2.) Ni kwa faida ya nani kwamba DPW anapewa haki ya bandari zote za Tanganyika, kwamba hakuna mwekezaji mwingine yeyote anaweza kuja kufanya uwekezaji kwenye bandari za Tanganyika bila udalali wa DPW, je, ukiritimba huu ni kwa faida ya nani?

3.) Ni kwa faida ya nani, DPW apewe haki ya kudai kipande chochote cha ardhi yenye ukubwa wowote anaoutaka yeye ndani ya ‘Territory’ ya Tanganyika na sisi tumpe ardhi hiyo kwa kuondoa watu na miradi yote ndani ya eneo alilolitaka, na tumpatie bire kabisa kwa gharama zetu sisi, hata fidia tulipe sisi ili kuondoa watu kumpisha, huu uwendawazimu ni kwa faida ya nani?

4.) Ni kwa faida ya nani, kwamba sisi tuliowekeza matrillion ya mikopo kuendeleza bandari na tukiwa kama wamiliki wa rasimali ya bandari, tupate 0% ya faida itakayotokana na uendeshaji wa huduma za kibandari, yaani ni kana kwamba yeye kawekeza 100% na hivyo achukue 100%? Uwendawazimu huu ni kwa faida ya nani?

5.) Ni kwa faida ya nani, kwamba mkataba unahusisha bandari za Tanganyika tu na sio za Zanzibar, ilihali bandari ni suala la Muungano? Je, Zanzibar haitaki kunufaika au yenyewe haitaki matunda ya mkataba huu? Ukizingatia walioongia huu mkataba wote ni waZanzibari, kuanzia Samiah Suluhu Hassan, Makame Mbarawah, Hamza Johari na wenzao, kwamba hawataki Zanzibar yao ipate matunda mazuri ya mkataba huu?!

6.) Ni kwa faida ya nani kusema kwamba, hata DPW akavunja mkataba na kukiuka kanuni na taratibu zote zinazotambulika kimataifa, bado hatutaweza kuvunja , kuusema vibaya au kujitoa kwenye mkataba, milele! Uwendawazimu huu ni kwa faida ya nani?

7.) Ni kwa faida ya nani kwamba pamoja na kuwa DPW watachukua 100% ya faida, bado tena faida hiyo watapewa Msamaha wa kodi kwa 100%, yaani hata hicho wanachovuna nacho hatuchukui kodi, na wakti huo huo tunakamuliwa kodi za miamala, uwendawazimu huu ni kwa faida ya nani?
 
Kanisa Katoliki hakika linadhihirisha unyenyekevu wa moyo.

Ukisoma katika andiko hilo kuna sehemu wanahimiza. Naomba kunukuu;
"Kwa kipindi hicho jamii nzima ya waumini katika Jimbo la Rulenge - Ngara inahimizwa kusali,kufunga, kufanya toba na malipizi kwa Mwenyenzi Mungu ili abadilishe mioyo ya watu wenye nia ovu kwa mambo matakatifu"

Pamoja na najisi iliyofanyika na watu hao, kanisa haliwaombei laana. Kanisa haliwaombei kifo, wala haiitishi Albadiri kwa ajili ya kuwaombea mateso.

Bali kanisa linaomba ili Mwenyenzi Mungu aweze kubadili mioyo yao. Nia zao mbaya zikapate kutoweka na wapate kumrudia Mungu kwa moyo wa toba.

Hapa kanisa linaiishi neno la Mungu la kutotaka kulaani ili tusijelaaniwa.

Ee Mwenyenzi Mungu wasamehe watu hao na mioyo yao ikajihisi wenye kukosa na wapate kurudi kwako tena.

Amen.
Ni kweli umewahi kutokea uharibifu ndani ya makanisa ya Kanisa Katoliki, lakini mara zote uharibifu huo uliambatana na wizi. Lakini kwenye hili, hatuambiwi kama kuna wizi umetokea.

Kule Sumbawanga, kanisa liliwahi kuvunjwa, na kikombe cha dhahabu cha hostia kiliibiwa. Ilitolewa siku moja kwa wahusika kukirudisha, hakikurudishwa. Wanaoaminika kufanya uovu ule, nyumba yao ilikuwa umbali usio mrefu kutoka Kanisani. Padre alitamka kuwa hawataenda polisi kwaajili ya tukio lile bali kama hakitarudishwa kikombe kile, kesho yake ambayo ilikuwa siku ya Jumatatu, mchana saa 6 atafanya ibada maalum kuomba mkono mrefu wa Mungu uwafikie waovu walioiba kikombe cha hostia ambacho walikipata kama zawadi kwa kila jimbo toka kwa Papa alipotembelea Tanzania.

Siku ya Jumatatu, wakati ibada ikiendelea, kimbunga kikali kikaipiga nyumba ile iliyohisiwa ni ya wahusika wa wizi, na watu watatu 3 walikufa. Je, walikuwa ndio wahusika halisi kama hisia za watu au ilikuwa ni coincidence tu, Mungu ndiye anajua.
 
Huna akili hivi makanisa yapo mangapi nchi nzima waende kuvamia huko
Sasa Mkuu ulitaka makanisa yote ya RC yavamiwe kwa siku moja!?...so hiyo ingeleta mtikisiko mkubwa?...sasa kama wavamizi wame target Eneo lile kutokana na aina ya waumini, au ulinz hafifu wa kanisa husika, unawezaje ku rule out kinachoendelea sasa na hilo tendo ovu?!
 
Una uhakika waliofanya huo uvamizi ni wana CCM?
 
Back
Top Bottom