Kanisa Katoliki hakika linadhihirisha unyenyekevu wa moyo.
Ukisoma katika andiko hilo kuna sehemu wanahimiza. Naomba kunukuu;
"Kwa kipindi hicho jamii nzima ya waumini katika Jimbo la Rulenge - Ngara inahimizwa kusali,kufunga, kufanya toba na malipizi kwa Mwenyenzi Mungu ili abadilishe mioyo ya watu wenye nia ovu kwa mambo matakatifu"
Pamoja na najisi iliyofanyika na watu hao, kanisa haliwaombei laana. Kanisa haliwaombei kifo, wala haiitishi Albadiri kwa ajili ya kuwaombea mateso.
Bali kanisa linaomba ili Mwenyenzi Mungu aweze kubadili mioyo yao. Nia zao mbaya zikapate kutoweka na wapate kumrudia Mungu kwa moyo wa toba.
Hapa kanisa linaiishi neno la Mungu la kutotaka kulaani ili tusijelaaniwa.
Ee Mwenyenzi Mungu wasamehe watu hao na mioyo yao ikajihisi wenye kukosa na wapate kurudi kwako tena.
Amen.