Kanisa Katoliki lapata Papa mpya wa 267, ni Robert Francis Prevost kutoka Marekani, ataitwa Papa Leo XIV

Naona safari ya KWENDA ROME imekaribia kwa kweli....

Wale WA airlines njoon inbox tupeane deal ya TKT..mwamba kaingiaaa Rome
 
Yametimia: Papa Mpya kutoka Chicago Marekani, Cardinal Robert Prevost, akichagua jina Papa Leo X1V:

Kwa wanauliza mambo haya yalianzia wapi:

Muda mfupi Yesu kabla hajakamatwa, alipata wasaa wa kuongea na wanafunzi wake kama kawaida yake. Katika mazungumzo yake ya mwisho mwisho, Injili inatuonesha namna alivyomkabidhi Petro jukumu la kusimamia kanisa akisema maneno haya:

" Nami nitakupa wewe funguo za ufalme wa mbinguni, na lolote utakalolifunga duniani, litakuwa limefungwa mbinguni, na lolote utakalolifungua duniani, litakuwa limefunguliwa mbinguni." Maneno mazito kwelikweli!

Baadaye tena alikuwa na mazungumzo tena na Petro:

"Walipokwisha kula, Yesu alimwuliza Simoni Petro, “Simoni, mwana wa Yohane! Je, wanipenda mimi kuliko hawa?” Naye akajibu, “Naam, Bwana; wajua kwamba mimi nakupenda.” Yesu akamwambia, “Tunza kondoo wangu.” Kisha akamwambia mara ya pili, “Simoni mwana wa Yohane! Je, wanipenda?” Petro akamjibu, “Naam, Bwana; wajua kwamba nakupenda.” Yesu akamwambia, “Tunza kondoo wangu.” Akamwuliza mara ya tatu, “Simoni mwana wa Yohane! Je, wanipenda?” Hapo Petro akahuzunika kwa sababu alimwuliza mara ya tatu: “Wanipenda?” Akamwambia, “Bwana, wewe wajua yote, wewe wajua kwamba mimi nakupenda.” Yesu akamwambia, “Tunza kondoo wangu!

Yesu akaendelea kumwambia tena:

"Kweli nakuambia, ulipokuwa kijana ulizoea kujifunga mshipi na kwenda kokote ulikotaka. Lakini utakapokuwa mzee utanyosha mikono yako, na mtu mwingine atakufunga na kukupeleka usikopenda kwenda.” (Kwa kusema hivyo, alionesha jinsi Petro atakavyokufa na kumtukuza Mungu)

Huyu ni yule Petro aliyedai hamjui Yesu usiku ule Yesu alipokamatwa, akaulizwa mara tatu akikana mara zote, mara ya tatu Yesu akageuka akamtazama, na jogoo akawika, kama ambavyo Yesu alimwambia itatokea. Udhaifu wa kibinadamu lakini kazi aliiweza.

Naam, safari ya Petro haikuwa rahisi. Baada ya kusimamia kuimarisha Ukristo yeye na wenzake, Petro alisulubiwa kwa amri ya Nero, mtawala wa Warumi, akining'inizwa miguu juu kichwa chini katika eneo linaloitwa sasa St. Peter's Basilica,eneo maalum kwa makusanyiko ya waumini Katoliki kote duniani, eneo ambalo watu walimwaga Papa Francis na walimsubiri Papa mpya, mjini Vatican ( ambao upo katikati ya mji wa Rome 🤣🤣)

Historia ya Papa huyu mpya wa kwanza kutoka Marekani, inaanza leo, akiwa amebeba jukumu alilokabidhiwa Petro, na mrithi wa Petro, na kuendelea, kuwachunga kondoo wa Bwana wanaokadiriwa kufikia 1.6 bilioni.

Tumuombee!
 
Attachments

  • Screenshot_20250508-204815_Google.jpg
    Screenshot_20250508-204815_Google.jpg
    658.4 KB · Views: 22
Aanzee na Sudan kusini
Aende congo
Arudi somalia
Aende.....
All d best papaa

Haooo WA gaza na Yemen watajijua wenyeweeeee pambana na sisi utukumbuke
 
Yametimia: Papa Mpya kutoka Chicago Marekani, Cardinal Robert Prevost, akichagua jina Papa Leo X1V:

Kwa wanauliza mambo haya yalianzia wapi:

Muda mfupi Yesu kabla hajakamatwa, alipata wasaa wa kuongea na wanafunzi wake kama kawaida yake. Katika mazungumzo yake ya mwisho mwisho, Injili inatuonesha namna alivyomkabidhi Petro jukumu la kusimamia kanisa akisema maneno haya:

" Nami nitakupa wewe funguo za ufalme wa mbinguni, na lolote utakalolifunga duniani, litakuwa limefungwa mbinguni, na lolote utakalolifungua duniani, litakuwa limefunguliwa mbinguni." Maneno mazito kwelikweli!

Baadaye tena alikuwa na mazungumzo tena na Petro:

"Walipokwisha kula, Yesu alimwuliza Simoni Petro, “Simoni, mwana wa Yohane! Je, wanipenda mimi kuliko hawa?” Naye akajibu, “Naam, Bwana; wajua kwamba mimi nakupenda.” Yesu akamwambia, “Tunza kondoo wangu.” Kisha akamwambia mara ya pili, “Simoni mwana wa Yohane! Je, wanipenda?” Petro akamjibu, “Naam, Bwana; wajua kwamba nakupenda.” Yesu akamwambia, “Tunza kondoo wangu.” Akamwuliza mara ya tatu, “Simoni mwana wa Yohane! Je, wanipenda?” Hapo Petro akahuzunika kwa sababu alimwuliza mara ya tatu: “Wanipenda?” Akamwambia, “Bwana, wewe wajua yote, wewe wajua kwamba mimi nakupenda.” Yesu akamwambia, “Tunza kondoo wangu!

Yesu akaendelea kumwambia tena:

"Kweli nakuambia, ulipokuwa kijana ulizoea kujifunga mshipi na kwenda kokote ulikotaka. Lakini utakapokuwa mzee utanyosha mikono yako, na mtu mwingine atakufunga na kukupeleka usikopenda kwenda.” (Kwa kusema hivyo, alionesha jinsi Petro atakavyokufa na kumtukuza Mungu)

Huyu ni yule Petro qliyedai hamjui Yesu usiku ule Yesu alipokamatwa, akaulizwa maravtatu akazuga, mara ya tatu Yesu akahe7ka akamtqzama, na jogoo akawika. Udhaifu wa kibinadamu lakini kazi aliiweza

Naam, safari ya Ptero haikuwa rahisi. Naada ya kusimamia kuimarisha Ukristo Yeye na wenzake, Petro alisulubiwa miguu juu kichwa chini katika eneo linaloitwa sasa St. Peter's Basilica,eneo maalum kwa makusanyiko ya waumini Katoliki kote duniani, eneo ambalo watu walimwaga Papa Francis na walimsubiri Papa Mpya:

Historia ya Papa huyu mpya inaanza leo, akiwa amebeba jukumu alilokabidhiwa Petro, na mrithi wa Petro, na kuendelea, kuwachunga kondoo wa Bwana wanaokadiriwa kufikia 1.6 bilioni.

Tumuombee!
Umetishaaaa

Amen n Amen
 
Back
Top Bottom