Kanisa Katoliki lapoteza Mapadri 25 na Watawa 60 kwa tatizo la upumuaji ndani ya miezi miwili

Kanisa Katoliki lapoteza Mapadri 25 na Watawa 60 kwa tatizo la upumuaji ndani ya miezi miwili

Marekani wamekufa, Italia wamekufa, wazungu wengi wamekufa na wanaendelea kufa. Hawa ndiyo wataalamu na wanasayansi wa dunia, wanajua kujihami kuliko sisi, na watu makini na wenye maendeleo kuliko sisi. Hawa watu wameweka lockdown lakini korona imewafuata mpaka majumbani, hata viongozi wa nchi zao wamepatwa na huu ugonjwa. Swali ni Je? Nini unaweza kuwa utatuzi? Tusaidiane kutafakari tusiache misimamo ya kisiasa itutawale.
Huko wamekufa kwa corona, sasa hapa kwetu hakuna corona ni nini kinawaua ?
 
Marekani wamekufa, Italia wamekufa, wazungu wengi wamekufa na wanaendelea kufa. Hawa ndiyo wataalamu na wanasayansi wa dunia, wanajua kujihami kuliko sisi, na watu makini na wenye maendeleo kuliko sisi. Hawa watu wameweka lockdown lakini korona imewafuata mpaka majumbani, hata viongozi wa nchi zao wamepatwa na huu ugonjwa. Swali ni Je? Nini unaweza kuwa utatuzi? Tusaidiane kutafakari tusiache misimamo ya kisiasa itutawale.
Ungekuwa unafuatilia ungejua kuwa pamoja na kufa wengi bado wanapambana sana,yaani hakuna kujibweteka na kusema hatujui cha kufanya.na kwa sasa wameshapewa chanjo na wanaanza kuondoa lockdown pole pole.makadilio yao ni kuwa june mambo yatakuwa mswano na kurudi hali ya kawaida.

Kupatikana kwa chanjo pia ni juhudi kubwa.
 
Kanisa limepoteza Imani hivyo wanavuna walichopanda
Tunasahau hata wimbi la Kwanza hatukulishinda kwa nguvu zetu.
Petro alianza kuzama majini baada ya kupoteza imani
Hakuna cha kuisha kwa Corona wimbi la kwanza wala wimbi la pili. Corona imeendelea kuwepo hapa nchini tangu Desemba 2019 hadi leo. Mtanzania mwenye kuamini 'ushirikina' wa Magufuli kuhusu kukabiliana na janga la Corona atakuwa mjinga tu.
 
Hapo utajua kiasi gani waumini wamekufa pia.mapadri 25 na hao masister 60 wamekutana na wakristo wangapi katika kutoa huduma.
 
Kati ya hao Mapdre 25, mmoja Ni kaka yangu baba mmoja mama mmoja. Rest in Peace Our first Born.
Msg zako za Whasap nazisoma Sana naona kama upo hai brother![emoji24][emoji24]
Pole mkuu
 
Ka
Huyu Mungu si hirizi, anataka kila binadamu awajibike na atumie uwezo wake kufikiri. si kusema tu, tunasali - Ameongeza Padri Charles Kitima
Aiseee sasa Kama Mungu si hirizi kwa nini mapadre na maaskofu katoliki husisitiza watu kumuomba Mungu wakati yeye si hirizi? au kinga au msaada unaoonekana tele wakati wa Mateso yawe ya Corona au vinginevyo?

kanisa katoliki matapeli waumini wanaenda jumapili kufanya nini kanisani kila dominika wakati Mungu sio kinga yao na si hirizi? mkatoliki shituka .ina maana lengo watoe sadaka tu na kuondoka wakati huyo Mungu mnayesema mpe sadaka hana msaada kwao wala sio kinga yao?

Wakatoliki mnapeliwa .Hili tamko alilotoa ni la kipagani Mungu wetu ni kama hirizi ni kinga yetu mateso yasitupate yawe corona au majanga yeyote .Zaburi inatamka wazi kuwa Mungu wetu ni kimbilio na nguvu na msaafa wetu unaoonekana tele wakati wa mateso.Ni kimbilio letu iwe kwenye corona nk ndiye hirizi yetu.

Kwangu mimi Mungu ndiye hirizi yangu
 
Hata wangekufa milioni maisha yataendelea

America kwenyewe walikuwa wakifa mpaka 4,000 mwa siku japo waliweka na lockdown na wana miundombinu safi ya kiafya.
 
Back
Top Bottom