Kanisa Katoliki lapoteza Mapadri 25 na Watawa 60 kwa tatizo la upumuaji ndani ya miezi miwili


Pitia data tena
 
So unfortunate hii ikisemwa na mzungu ndiyo itaonekana ni science, wewe mbuntu basi ni ushirikina....Kuna watu hawasomeki kwanini walipewa akili kwenye vichwa vyao kama hawawezi ku ng'amua vitu simple na direct kama hivi mpaka mzungu aseme...
 
🙏🙏🙏
 
Usimuaibishe mzazi wako. Kwamba unaweza kupiga ban makanisa?. Kweli
 
Mzee ajitathimini sana kwenye hili suala la COVID-19 Vaccine - anaweza kujikuta kabakia peke yake!!
 
Hata watu wote wakikataa, ukweli utabaki kuwa Tanzania tuliponywa na Mungu dhidi ya Corona!! Mungu apishe mbali!! Tanzania tulionja tu harufu ya corona, hata sasa tunasikia harufu tu ya corona....
Amen...May God have mercy on us!
 
Mzee ajitathimini sana kwenye hili suala la COVID-19 Vaccine - anaweza kujikuta kabakia peke yake!!
What is the problem akibaki prke yake?

Kuna jinsi Mungu anaweza mheshimisha kwa utukufu wa jina lake..What if mataifa yote wakichanjwa na bado wakaendelea kufa na corona mpaka wakakubali kuwa hakuna chanjo?

Hufikiri hilo la wao kushindwa unamfikiria tu yeye kushindwa?
After all hakuna mashindano hapo...He is just not accepting everything because all are doing even of they are not certain...So far hakuna certainity kwenye hiyo chanjo yao let him be!
 
Hadi nimemuogopa hyo jamaa.Yaani bado kuna watu wanaamini kuwa bila sayansi tunaweza kuvuka pia.
Do not stoop so low...Science siyo lazima iwe hiyo ya mzungu...Science ni uwezo wa mwanadamu kung'amua what might be a solution to a specific problem ambayo kila mwanadamu amepewa intrinsic capability ya adaptation to any problem ambayo ndiyo science number moja, hizo zingine ni ego tu. It can happen by chance for new facts which after a number of repetition inaweza kuwa repeated....Acheni kudanganya raia...Huko vijijini unadhani hawafanyi science?
 
Msimshirikishe Mwenyezi Mungu kwenye maamuzi yenu nyie CCM. Mungu ametupa weredi wa kutambua na kujikinga na majanga hapa ulimwenguni. Soma kifungu hiki cha Biblia takatifu.

Hosea 4:6​

Watu wangu wanaangamizwa kwa kukosa maarifa; kwa kuwa wewe umeyakataa maarifa, mimi nami nitakukataa wewe, usiwe kuhani kwangu mimi; kwa kuwa umeisahau sheria ya Mungu wako, mimi nami nitawasahau watoto wako.
 
Huna tofauti na wale wasabato wanaotaka kwenda ulaya Bila nauli Wala tiketi..wakidai maombi yatawasafirisha...OMBA SANA MUNGU WAKO JITUME SANA KUFANYA KAZI
 
Kanisa limepoteza Imani hivyo wanavuna walichopanda.

Tunasahau hata wimbi la Kwanza hatukulishinda kwa nguvu zetu.

Petro alianza kuzama majini baada ya kupoteza imani.
Watakao kuelewa tuko wachache sana!

Yaani wimbi la kwanza tumelipita hadi mataifa yakashangaa, jiulize walio omba kuchezea mechi zao hata uwanja wa Taifa wakidai kwao kuna Corona!
 
Du!.. Huyu padri anamlalamikia nani sasa juu ya vifo vya mapadri wenzake na watawa?, Hivi tamko la Serekali la kukiri kuwa UVICO upo Tanzania ndilo lingebatirisha amri ya binadamu kufa ambayo ni ya uhakika kwa asilimia mia? Mimi nadhani angefurahi kuwa watawa na mapadri kwa wingi sana mwaka huu wameitika wito wa muumba wao na kwa kuwa wameishi maisha ya kiroho na kufanya yanayompendeza Mungu kama wanavyowafundisha waumini wao hivi sasa wamekaa mbinguni upande wa wenye haki, anapaswa kumtukuza Mungu kwa hilo na siyo kuingilia mambo ya wanasiasa wanaopinga na kukosoa kila kitu.
 
Ndugu Wanahabari, nadhani ni upuuzi wa kupindukia kuendelea kumsikiliza huyu Musiba, as 1. He is 100% inconsistent, 2. He has no basis for speaking and I am strongly discovering that he is looking for DC, RC, or any position to fill his empty stomach.
Hivi Wa-Tanzania, what is so special with Tanzania to the extent that every country on earth has the bad intention of harming us and not other countries. Musiba's claims are baseless.
 
Sasa ukweli huu niliyo utaja hapo juu ndio unamfanya Rais wetu JPM akatae kuingiza nchini chanjo zenye utata mkubwa
Sasa ni nini kinamzuia Raisi wetu kununua chanjo za covid 19 za laki mbili halafu awape wanasayansi wetu wazichunguze halafu watupe muongozo
Kuliko kupanda jukwaani bila ushahidi wa wanasayansi wetu wa Kitanzania bila utafiti
 
Kosa muhimu walilofanya wakatoliki na madhehebu mengine yote ni kuchelewa kujua na kukemea maovu yaliyoanza kuonekana mwanzo kabisa wa utawala wa Magufuli.

Aliwapumbaza na wakati mwingine kuwapa vitisho wasikemee, na wao wakakaa kimya wakidhani yatakwisha au yatafikia mwisho.
Pengine alijaribu kuchonganisha, dini na dini, kama waislam na wakristo ili pasiwepo na sauti moja ya kukemea mabaya yanayofanyika.

Wao, dini hawakuuona mchezo huu.

Kukaa kimya kwao kulichukuliwa kukubali au kuogopa, kwa hiyo Magufuli akaona mlango wazi wa kufanya lolote bila ya mtu, wapinzani wala dini kusema lolote.

Matokeo yake ndiyo haya sasa hivi.
 
Hivi unaelewa unachoandika, au unajipigia pigia tu kujaza maneno yasiyokuwa na maana?

"...abortion na wala family planning, je hiyo siyo science"? Nani kasema ni sayansi au ni sayansi, na inahusu nini na mjadala uliopo hapa.

Andiko lote, hata kama lingeandikwa na mtu aliyekwenda shule, lakini akawa ameliandika baada ya kilevi fulani lisingeweza kuwa mchanganyiko kama hili uliloleta hapa.

Sasa sielewi wewe ni mtu wa aina gani!
 
kufa tutakufa na wengine wataishi,hakuna binadamu anayeweza kuchukua tahadhari ya kifo
 
Imenibidi niku'quote' tu kwa haya uliyoandika leo, hata kama sitaongeza la ziada juu yake.

Ahsante.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…