Stuxnet
JF-Expert Member
- Feb 12, 2011
- 18,875
- 29,427
Kimsingi Fr Kitima anatumia kiti cha kuwa Katibu Mkuu wa TEC (Baraza la Maaskofu Tanzania) kueneza hisia zake za kisiasa. Mbona watangulizi wake kwenye hicho cheo hawakuwahi kuingia kwenye siasa kiasi hiki??kuna siku huyo binamu yake Lisu aliongoza ibada ya wanaume katoliki hapo kanisa la kristu mfalme tabata, sasa kuna mzee moja wa makamu alikua ameketi pembeni yangu, aliniuliza huyu padre anazungumzia nini mbona kama anafanya siasa madhabahuni?, ananikwaza.
Baada ya muda mfupi yule Mzee alinyanyuka kwenye kiti na kuondoka zake nyumbani kabla ya ibada.🐒
Ingependeza sasa Fr Kitima avue kanzu ya Updre kama alivyofanya Dr Slaa na ajiunge kwenye majukwaa ya siasa rasmi.