Kanisa Katoliki mnazingua, michango imekuwa kero

Hili suala miaka ya karibuni limewachosha waumini wengi, ndo maana imefika hatua hata waumini wengine kutopenda kwenda kanisani wala jumuiya,.
Siku hizi kama mtu huna sadaka huwezi kwenda kanisani, maana wananyanyua bench moja baada ya nyingine.
Ikifika zamu ya bench lako unainuka kuwasapot unaelekea toilet
 
Taasisi za kiroho zinapaswa kuwa na miradi ya kuwaingizia vipato kama vile fremu za maduka,mashine za kusaga nafaka,miradi ya ufugaji wa kuku n.k.....Waumini wanapaswa kupunguziwa mizigo ya michango kwa sababu wanatoa sana sadaka na zaka na kingine huwa nashangaa Zaka huwa zinawafikia walengwa yaani wajane,mayatima,wenye madeni,wazee wasiojiweza,walemavu. Zaka zinapaswa kutangazwa kuwa awamu hii tumepeleka zaka katika makundi flani ya wahitaji
 
Kanisa Katoliki mnazingua, michango imekuwa kero
Badala ya kusema 'Kanisa Katoliki' nilitegemea useme 'Parokia ya Mt. fulani'. Ukisema Kanisa Katoliki unamaanisha ni utaratibu wa RC ulimwenguni kote, kumbe ni kwenye Parokia yako na labda nyingine baadhi. Huo ni utaratibu na mara nyingi unakuwa umewekwa na Kamati Tendaji ya H/Walei ya Parokia husika. Njia sahihi ni kufikisha ujumbe katika vikao vya Halmashauri ya Walei ya Parokia yako.

Mfano mimi huku, Parokia yangu haina utaratibu huo wa 'kuwakomboa watoto', ila kuna utaratibu fulani walianza kuutekeleza wa kuweka vikapu vya Simba na Yanga kama inavyofanyika kwenye baadhi ya kumbi za harusi, tukawapiga stop na wakaacha. Hapo nisingeweza kuhukumu kuwa Kanisa Katoliki linachangisha kwa vikapu vya Simba na Yanga, ningesema Parokia yangu ya Mt. Maria Magdalena Vingunguti inatufanyia hivyo
 
Haya mambo usizungumze tu kama muumini wa Mwamposa au nabii wanaoota kama uyoga siku hizi.
Katoliki ni moja, kanisa la kimapokeo. Ukisema ni Parokia yake n.k unakuwa unamaanisha?
Yupo sahihi kuzungumzia Parokia, maana nyingine zipo katika hatua ya ujenzi wa Kanisa, nyingine zina kanisa ila zinajenga mradi fulani kama vile ukumbi wa sherehe, nyingine zinakichangia kigango hadi hatua fulani ili kijitegemee nk. Michango ambayo ni common katika Kanisa Katoliki ni zaka, mavuno na ada za kupata sakramenti kadhaa kwa ajili ya mambo ya kiutawala kama vile kutengeneza vyeti.
 
Unapinga nini wakati unaambiwa Kanisa ni moja, takatifu, katoliki na la mitume
 
Hawa jamaa nawashangaa sana
Mkoloni alijenga makanisa mpaka leo yapo nao wakajiongeza na kuzungusha maduka kwa baadhi ya makanisa
Wanakusanya kodi miaka
Mimi nadhani wao ndio wangekuwa wanawapa wasiojiweza hela na wale waliokuwa wanatoa hata miaka 40 na sasa ni wazee
Wapewe za bure na matibabu pia
Kama ni Dini na sio biashara basi watoe kama sadaka na wao
 
Kanisa katoliki lina miradi kibao kuanzia mashule, hospitali na vyuo vikuu, mfano kama Msimbazi Center inaingia pesa ya kutosha, kwa waumini waendelee kukamuliwa? Hizi pesa zinakwenda wapi?
 
Hahahaha ckujua waumini mnateseka ivi hapa duniani hahaha Bado apo hamna ukakika kama mtaenda mbinguni
 
Noma sana tuandamane ama nini😂🖐️
 
Sio kweli hata ukienda nchi jirani nao ni hivyohivyo nafikiri haujui chanzo cha hiyo michango ni nini, lazima ujue mzizi wake ndipo unaweza kutatua hilo tatizo, malengo ya dini yalishapotea kama ilivyo elimu nyingine.Swali aliyefanya hesabu ya mwaka 19001 na ya sasa hivi ni sawa? Hesabu ilishabadirika kulingana na wakati nayo dini ni hivyohivyo ila kwa sasa kilichobakia ni vitisho, kutengwa nk.Mimi nimekwambia sitaki kwenda mbinguni kwanini wewe ikuume mpaka uunde kamati ya kunitenga kwenye jamii ninayoishi nayo?.
 
Ila wamezidi kutoa sana michango
 
Me catholics wanachonikwaza ni pale tunapochanga kwenye jumuia kujenga buildings for social welfares kama Dispensary, ukumbi or whatever alau ukishakamilika hawa wanajumuia wa chini kabisa huku, waliojinyima kujenga hivyo vitega uchumi, hawapati incentives yeyote kwenye matumizi ya vitu walivyojenga kwa gharama zao. Inaumiza sana maana hatuombi iwe for free lakini unaweza sema kwa mwaka kila mwana jumuia hai apewe angalau discount charges ya hata 15% kila mara anapoenda ku seek huduma ambayo alichangia kwenye uanzishaji wake.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…