Kanisa la Tanzania linapitia kipindi kigumu sana. Mungu alinusuru

Kanisa la Tanzania linapitia kipindi kigumu sana. Mungu alinusuru

Hizi ndio changamoto za kanisa LA Tanzania. Tuzidi kumuomba Mungu.

1. Mikutano ya The Big Octoba na The Big Novemba iliyokuwa inahuhubiri kuacha dhambi na kumrudia Kristo imekufa.

2. Mwamposa na Suguye wanauza vifaa vya uponyaji mafuta, maji, keki na vitambaa badala ya kuhubiri watu waache dhambi, pia hawataki kufungua matawi mikoani na kupanda makanisa.

3.RC nao wamechachamaa kwa michango kuanzia kwenye jumuiya hadi Parokiani. Huna hela huzikwi.

4. Mwakasege naye amechachamaa na masomo ya sadaka mwanzo mwisho, mfano semina ya Mbeya (26-30 Oct, 2022) somo ni sadaka tu hakuna kingine.

5. KKKT nao hawaeleweki wachungaji wanaowaiga wapentekosti/walokole ndio wanapata umaarufu mfano Kimaro na Mgogo wale wanaohubiri kilutheriluther hawana chao wala umaarufu.

6. TAG/EAGT hawana wainjilisti wakitaifa kama kina Moses Kulola wamebakia wapigaji tu.

7.Viongozi was dini kugombania mialiko sherehe za kitaifa ili wakalambe asali no aibu.

INAUMA SANA
Kiukweli ni changamoto sanaa aiseee!
 
Kiukweli sasa hivi wahuni wamekua wengine makanisani ndio maana masanja na yeye ana "kanisa" lake,
kuna yule wa nywele na kucha na yeye ana la kwake yani upuuzi mtupu

yani imekua mtu akiwa maarufu kwenye kitu flani basi anawaza kufungua "kanisa" apige hela,
na ukiingia humo ndani hutosikia habari za acha dhambi ujiandae kwenda mbinguni, wao Kila siku wanaongea habari za sadaka na mafanikio lakini cha ajabu viongozi wa hayo "makanisa" wanakua matajiri waumini wanazidi kua maskini

Ukikutana na mabinti wa hayo "makanisa" humo ndani ndio utachoka zaidi mavazi wanayo vaa kama wanaenda "kidimbwi" ukiuliza kulikoni unaambiwa eti "mungu anaangalia moyo sio mavazi"
Mungu aingilie kati
 
Hiyo namba 3, waumini tuko imara sana. Maana michango yote tunayochanga ni kwa ajili ya kulitegemeza Kanisa la Mungu.

Halafu ifikie wakati tuwe wakweli! Hakuna binadamu asiyeishi katika Jumuiya! Sasa kama wewe jumuiya yako ni ya wavuta bangi, inakuwaje tena unataka uzikwe na jumuiya nyingine?

Tumsifu Yesu Kristo Tate Mkuu

Watu wanasahau kwamba makanisa na misikiti inaendeshwa kwa sadaka na kutoa sadaka ni maelekezo ya Mungu bila shurti
 
Kazi tunayo kuna muda watu wanakabiliwa na changamoto kiasi kwamba hawaelewi wanataka nini ili watatue hizo changamoto

Watajaribu kila njia na mbinu wanayojulishwa ndiyo sababu kubwa ya jamii kubwa kuyumba kiimani.
 
Tumsifu Yesu Kristo Tate Mkuu

Watu wanasahau kwamba makanisa na misikiti inaendeshwa kwa sadaka na kutoa sadaka ni maelekezo ya Mungu bila shurti
INJILI NI KUFUKA, KUZIKWA NA KUFUFUKA KWA YESU KRISTO.
TUBUNI UFALME WA MUNGU UMEKARIBIA... AMIN, OKOKA N.K

sadaka bila injili ya kuacha dhambi+kazi ya msalaba ni uhuni mtupu!
mama D
 
Ni sahihi kwa mtazamo wakonkwa kuwa unaangalia wachungaji na watumishi maarufu ila sisi huku vijijini bado tunapiga Injili na Mambo yanaendelea.
Safi sana mkuu. Barikiwa.

Injili iende mbele
 
Back
Top Bottom