Kanisa la Tanzania linapitia kipindi kigumu sana. Mungu alinusuru

Kanisa la Tanzania linapitia kipindi kigumu sana. Mungu alinusuru

INJILI NI KUFUKA, KUZIKWA NA KUFUFUKA KWA YESU KRISTO.
TUBUNI UFALME WA MUNGU UMEKARIBIA... AMIN, OKOKA N.K

sadaka bila injili ya kuacha dhambi+kazi ya msalaba ni uhuni mtupu!
mama D

Kuhubiri injili ya kuacha dhambi na kazi ya msalaba na kuyaishi yale tunayoyahubiri kama wahubiri ndio njia pekee ya kweli na uzima.

Vinginevyo hata sadaka tunazotoa au zinazopokelewa makanisani zinaweza kuwa machukizo mbele za muumba.
Maana zipo taratibu za kutoa Sadaka kama agizo lisilo shurti.
 
Hizi ndio changamoto za kanisa LA Tanzania. Tuzidi kumuomba Mungu.

1. Mikutano ya The Big Octoba na The Big Novemba iliyokuwa inahuhubiri kuacha dhambi na kumrudia Kristo imekufa.

2. Mwamposa na Suguye wanauza vifaa vya uponyaji mafuta, maji, keki na vitambaa badala ya kuhubiri watu waache dhambi, pia hawataki kufungua matawi mikoani na kupanda makanisa.

3.RC nao wamechachamaa kwa michango kuanzia kwenye jumuiya hadi Parokiani. Huna hela huzikwi.

4. Mwakasege naye amechachamaa na masomo ya sadaka mwanzo mwisho, mfano semina ya Mbeya (26-30 Oct, 2022) somo ni sadaka tu hakuna kingine.

5. KKKT nao hawaeleweki wachungaji wanaowaiga wapentekosti/walokole ndio wanapata umaarufu mfano Kimaro na Mgogo wale wanaohubiri kilutheriluther hawana chao wala umaarufu.

6. TAG/EAGT hawana wainjilisti wakitaifa kama kina Moses Kulola wamebakia wapigaji tu.

7.Viongozi was dini kugombania mialiko sherehe za kitaifa ili wakalambe asali no aibu.

INAUMA SANA
Yaonekana has uliowaacha yaani Mzee wa Upako, Gwajima, Kakobe na Suguye has kazi zao unazikubali
 
Ondoa Hapo namba 3 umekosea.Tunaona shule hospitali vyuo n.k vyote hivi vinatoa huduma katika jamii wakati huo mapadre si watu matajiri kama ilivyo kwa wengine na injili inahubiriwa kama kawaida.
Nikuulize maswali mawili:

1. Unajua ada za shule za RC no sh.ngapi? Una mtoto au ndugu umewahi kumsomesha kwenye hizo shule? Ulilipa sh.ngapi? Ada+michango.

2. Umewahi kutibiwa bure kwenye hospitali za RC mfano Bugando au Tosamaganga Hospital au Peramiho??? Au umewahi kuuguza ndugu yako kwenye hizo hospitali bure?
 
Yaonekana has uliowaacha yaani Mzee wa Upako, Gwajima, Kakobe na Suguye has kazi zao unazikubali

Ila tusi Fikiri kuwa wale ambao hawakutajwa akina Molavian,Anglican, SDA, Mzee wa upoko, Mwingira, Kakobe nk nk huko ni kwema tutakuwa tunajidanganya. Ule upande wa pili sijui yanayoenddlea.
Upo sahihi
 
Mtuache wakatoliki michango yetu ni ya kufanya mambo ya maendeleo. Na injili lazima iwezeshwe utaenda kuhubiri injili kwa miguu. Mahema, vipaza sauti , viti vinalipiwa vyote hivyo. Muacheni Mwakasege achape injili.
 
Hizi ndio changamoto za kanisa LA Tanzania. Tuzidi kumuomba Mungu.

1. Mikutano ya The Big Octoba na The Big Novemba iliyokuwa inahuhubiri kuacha dhambi na kumrudia Kristo imekufa.

2. Mwamposa na Suguye wanauza vifaa vya uponyaji mafuta, maji, keki na vitambaa badala ya kuhubiri watu waache dhambi, pia hawataki kufungua matawi mikoani na kupanda makanisa.

3.RC nao wamechachamaa kwa michango kuanzia kwenye jumuiya hadi Parokiani. Huna hela huzikwi.

4. Mwakasege naye amechachamaa na masomo ya sadaka mwanzo mwisho, mfano semina ya Mbeya (26-30 Oct, 2022) somo ni sadaka tu hakuna kingine.

5. KKKT nao hawaeleweki wachungaji wanaowaiga wapentekosti/walokole ndio wanapata umaarufu mfano Kimaro na Mgogo wale wanaohubiri kilutheriluther hawana chao wala umaarufu.

6. TAG/EAGT hawana wainjilisti wakitaifa kama kina Moses Kulola wamebakia wapigaji tu.

7.Viongozi was dini kugombania mialiko sherehe za kitaifa ili wakalambe asali no aibu.

INAUMA SANA
Dah!, Mkuu umewaza mbali sana, MUNGU ATUSAIDIE TU.
 
Kwa kweli amekosea kwenye namba 3 eti huna hela huzikwi ??

Ni kuwa kama umejitenga na shughuli za kanisa nao wanakutenga huduma za kanisa
 
Back
Top Bottom