Kanisa la Tanzania linapitia kipindi kigumu sana. Mungu alinusuru

Kuna kutoa sadaka na kutupa sadaka.

Sent from my 2201116TG using JamiiForums mobile app
 
Kweli kabisa mkuu
 
Wewe uliyefurahia mateso na dhuluma kwa wapinzani sahau mbingu.
 
Nikuulize wewe, Kabla ya kuwalaumu wengine...
Je umeacha alama gani kwenye kazi ya Mungu...?
 
Afadhali wewe umesema ukweli.
Watu wengi kwa sasa wanaenda kanisani ili wakifa au wakifiwa wasikose watu wa kutosha kuwazika.
 
Mimi nadhani ktk bandiko lako hoja #3 ihusuyo RC ungeitoa maana mimi binafsi nachangia Kanisa na taasisi zake hata nikiwa nje ya Kanisa au jumuiya,pia hakuna kitu kinaitwa "kama huna hela hupewi huduma za kikanisa”

Najua wewe siyo RC ila kama unaijua Radio Maria huwa kuna mchango wa kuiwezesha(maana haina matangazo yoyote ya kibiashara so ada yake pamoja na mishahara ya wafanyakazi inatoka kwetu sisi waamini) mwaka huu inatakiwa zaidi ya 1bill ambayo wasikilizaji tunaichanga tukiwa hata hatujuani,imani hakuna kulazimishana kama wewe huko uliko unalazimishwa ni wewe usituweke wote kwenye kundi moja
 

Ndugu umekuwa msemaji wa kanisa lipi la Tanzania ? Kuona uchungu ni jambo moja kuchukua hatua ni jambo jingine wewe umechukua hatua gani ? Kinachowasibu watu (hapa nasisitiza watu sio dini au imani zao ) ni suluhu ya shida zao sio kingine,yeyote atakaye leta suluhu ya shida zao atapata heshima kwao na kama huna usijewaza watu watabaki na wewe then uwaambie waende kwa amani huku wakiteswa na ibilisi haitawezekana . Kama kuna uwongo kwa hizo imani wewe LETA UKWELI WAKE tunataka majibu ya changamoto zetu hilo tu .
 
Bora utoe sadaka kuliko kununua bando la 5000 kufatilia UMBEA insta na fb
Hakuna kilicho bora. Tena kutoa sadaka kwa matapeli wanaojiita ni watu wa Mungu ni hatari hata kuliko kuangalia umbea. Kutoa sadaka kwa matapeli ni kuunga mkono kazi ya shetani.
 
Nikuulize wewe, Kabla ya kuwalaumu wengine...
Je umeacha alama gani kwenye kazi ya Mungu...?
Bora usiache alama yoyote kuliko kuharibu alama zilizokwishawekwa na wakristo wa kweli wa mwanzo. Matapeli wanaojiita viongozi wa dini wamekuwa wengi na hawa kazi yao kubwa imekuwa ni kufuta zile alama ambazo zilikwishawekwa. Wamewakatisha tamaa baadhi ya wakristo baada ya kugundua uovu wao.
 
Watu hawataki kwenda Kanisani, Jumuiya hawaendi, michango hawatoi lakini wanataka wakipatwa na matatizo Kanisa liwasaidie au wakifariki wazikwe na Kanisa.
 
Haisemwi uende ukatibiwe bure au ukasomeshe mtoto bure!

Tuchukulie mfano suala la matibabu,matibabu angalao yanakuwa ktk hali ya utulivu nilikuwa na mama yangu mgonjwa juzi mwezi wa saba niliona.hiyo serikali inashindwa kutibu raia wake na kodi wanalipa itakuwa kanisa?dawa watanunua na nini watawalipaje wafanyakazi?
 
Eti mgogo na kimaro wanaiga staili ya wa pentekoste kuhubiri, ungekuwa unajua historia ya injili ungejua muhubiri aliyezaa upentekoste alikuwa Martin Luther mluteri usingeandika ulivyoandika,na ungejua kategori za watumishi wanavyoitwa usingehukumu watumishi kirejareja hivyo wapo watumishi wameitwa kuhubiri uchumi kibiblia kwa hiyo mostly watahubiri katika mlengo huo,n.k
 
Mwakasege naye amechachamaa na masomo ya sadaka mwanzo mwisho, mfano semina ya Mbeya (26-30 Oct, 2022) somo ni sadaka tu hakuna kingine.
Huu ni uzushi na ujinga na Uzindaki wa kiwango Cha juu, hakuna ibada kwenye spiritual world isiyoambatana na sadaka ndo maana kwenye ibada yeyote Ile sadaka ni muhimu ili kufanya upatanisho kwenye spiritual

Ukienda kwa waganga wa kienyeji lazima utoe sadaka ni ili wafanye upatanisho kwenye ulimwengu wa Roho

Sadaka inatumika na miungu kukamata mioyo yao ni mjinga pekee anayepinga sadaka, kama hutaki sadaka ni vizuri ukaachana na mambo ya kiroho
 
Kaandika ujinga mtupu
 
Shule Zina walimu nani atawalipa hospital inahitaji vifaa na madaktari nani atakayewaalipa

Ni jambo la kuogofya kuona mwanaume analilia vitu vya bure
 
Watumishi wameitwa kuhubiri uchemi kibiblia? Mbona unatupiga fix jamani? Hao hao watumishi walioitwa kuhubiri uchumi wakitaka gari la kutembea wanaomba mchango kwa waumini na waumini wakitaka gari wanaambiwa waombewe na mhubiri aliyewaomba mchango. Kwa nini yeye mhubiri asiombe gari kwa njia ya maombi?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…