MAPITO Mwanza
JF-Expert Member
- Aug 21, 2018
- 4,236
- 5,907
Umweli mwingiii
Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Sadaka ya Yesu Kristo msalabani (sacrifice) haifanani kamwe na fedha na mali. Huku ni kuudharau msalaba.Point no 4, Refer sadaka aloitoa Mungu kumtoa Yesu Kristo, Ibrahimu kumtoa Isaka. Hivyo basi huoni ya kuwa Mungu mwenyewe ndio muanzilishi wa Sadaka???
Sadaka ni divine invitation, Kamsome Kornelio, Dorcas na Daudi.
Usilolijua...Kuna padre ameangusha ghorofa karibu na kibanda changuOndoa Hapo namba 3 umekosea.Tunaona shule hospitali vyuo n.k vyote hivi vinatoa huduma katika jamii wakati huo mapadre si watu matajiri kama ilivyo kwa wengine na injili inahubiriwa kama kawaida.
Pia udini.. naongea Kila mara hamna dini inayookoa mtu ..Ukristo sio dini, shida inaanza tunapolazimisha Ukristo uwe dini.. lazima ufanye hivi upate majibu, lazima ufanye hivi uwe mtakatifu.. mambo ya kujitakasa takasaYesu Kristo hakuja kufungua majengo ama taasisi ziitwazo Kanisa. Kimsingi Kanisa ni kusanyiko - congregation - eklesia. Kristo alikuja kutangaza habari njema ya ufalme wa Mungu. Taasisi zilizojiita "Kanisa" ni mpango wa mwanadamu kumtafuta Mungu, lakini mpango wa Mungu kumtafuta mwanadamu ni kufa na kufufuka kwa Yesu Kristo.
Tumeitwa kuwa ufalme wa makuhani:
Ufunuo wa Yohana 5:9
Nao waimba wimbo mpya wakisema, Wastahili wewe kukitwaa hicho kitabu na kuzifungua muhuri zake; kwa kuwa ulichinjwa, ukamnunulia Mungu kwa damu yako watu wa kila kabila na lugha na jamaa na taifa,
Ufunuo wa Yohana 5:10
ukawafanya kuwa ufalme na makuhani kwa Mungu wetu; nao watamiliki juu ya nchi.
Hawa ni wana wa ufalme wa makuhani kwa Mungu, kutoka dunia yote. Kumbuka Kristo katika mafundisho yake aliongelea agenda moja tu, UFALME WA MUNGU. Ili kuwa raia wa ufalme wa Mungu ni lazima uzaliwe huko, ndio maana ya kuzaliwa mara ya pili. Mungu ni Roho na ufalme wake ni wa kiroho. Huwezi kuwa mwana wa ufalme kwa jinsi ya kimwili bali kwa kuutiisha mwili ni kumfanya Roho atawale. Hili ndio aina ya Kanisa aliloacha Kristo, Kanisa la wamwabuduo halisi.
Makanisa mengi leo hii yapo kimwili tu huku yakijiita wana wa Mungu. Sio kila ajiitaye Mkristo ni mwana wa Mungu, church membership haikufanyi kuwa mwana. Ndio hizo taratibu na sheria nyingi za makanisa. Makanisa ya mali na mafanikio, makanisa yanayolilia milki za dunia. Hayo yanekoma kuwa makanisa ya Mungu aliye hai, ekklesia
Umuombe Mungu yupi huyo? You are doomed.Hizi ndio changamoto za kanisa la Tanzania. Tuzidi kumuomba Mungu.
1. Mikutano ya The Big Octoba na The Big Novemba iliyokuwa inahuhubiri kuacha dhambi na kumrudia Kristo imekufa.
2. Mwamposa na Suguye wanauza vifaa vya uponyaji mafuta, maji, keki na vitambaa badala ya kuhubiri watu waache dhambi, pia hawataki kufungua matawi mikoani na kupanda makanisa.
3.RC nao wamechachamaa kwa michango kuanzia kwenye jumuiya hadi Parokiani. Huna hela huzikwi.
4. Mwakasege naye amechachamaa na masomo ya sadaka mwanzo mwisho, mfano semina ya Mbeya (26-30 Oct, 2022) somo ni sadaka tu hakuna kingine.
5. KKKT nao hawaeleweki wachungaji wanaowaiga wapentekosti/walokole ndio wanapata umaarufu mfano Kimaro na Mgogo wale wanaohubiri kilutheriluther hawana chao wala umaarufu.
6. TAG/EAGT hawana wainjilisti wakitaifa kama kina Moses Kulola wamebakia wapigaji tu.
7.Viongozi was dini kugombania mialiko sherehe za kitaifa ili wakalambe asali no aibu.
INAUMA SANA
Hajui maana ya sadaka. Sadaka kwake ni kutoa pesa kwa Mwakasege ili akatumie atakavyo.Braza umewahi kumsikiliza hapo kwenye sadaka anaongelea nini kabla ya kumjudge? Maana wakati mwingine ni unfair.
Kanisa ni jumuiya huru, uwe na mchango au usiwe nao, uwe na hela au usiwe nayo, ubaya ulioposasa huku RC tunapeana mpaka risiti za michango ya jumuiya...hizo ni sadaka hapa panaboa sana.Hiyo namba 3, waumini tuko imara sana. Maana michango yote tunayochanga ni kwa ajili ya kulitegemeza Kanisa la Mungu.
Halafu ifikie wakati tuwe wakweli! Hakuna binadamu asiyeishi katika Jumuiya! Sasa kama wewe jumuiya yako ni ya wavuta bangi, inakuwaje tena unataka uzikwe na jumuiya nyingine?
Kama kuna kitu sintokuja kurudia kutoa ni mchango wa kujenga mradi wa kanisa!! Iwe ni hospitali, shule, hotel, au gesti hausi, SITOI, kkkt arusha ilinipa somo.Ondoa Hapo namba 3 umekosea.Tunaona shule hospitali vyuo n.k vyote hivi vinatoa huduma katika jamii wakati huo mapadre si watu matajiri kama ilivyo kwa wengine na injili inahubiriwa kama kawaida.
Mkuu nakuomba PM kakaMwakasege naye amechachamaa na masomo ya sadaka mwanzo mwisho, mfano semina ya Mbeya (26-30 Oct, 2022) somo ni sadaka tu hakuna kingine.
Hiyo namba 3 sio changamoto ya RC kuyumbisha kanisa, amekwepa kusrma changamoto za ukweli, uzinzi wa mapadri na mauaji kanisani tena mauaji ya mapadri ni changamoto kubwa sana huko RCHiyo namba 3, waumini tuko imara sana. Maana michango yote tunayochanga ni kwa ajili ya kulitegemeza Kanisa la Mungu.
Halafu ifikie wakati tuwe wakweli! Hakuna binadamu asiyeishi katika Jumuiya! Sasa kama wewe jumuiya yako ni ya wavuta bangi, inakuwaje tena unataka uzikwe na jumuiya nyingine?
RC changamoto yao kubwa kwasasa ni uzinzi wa mapadri, pia mauaji ya mapadri kanisani na hakuna kesi inafikirisha sanaTumsifu Yesu Kristo Tate Mkuu
Watu wanasahau kwamba makanisa na misikiti inaendeshwa kwa sadaka na kutoa sadaka ni maelekezo ya Mungu bila shurti
UsihukumuKwa kweli amekosea kwenye namba 3 eti huna hela huzikwi ??
Ni kuwa kama umejitenga na shughuli za kanisa nao wanakutenga huduma za kanisa
Sasa nyinyi wafuasi wa Ellen G White mna unafuu gani!! Mnashindwa kula hata kitimoto, kwa sababu za kipuuzi tu!Nendeni kwa wasabato. Case closed