Kanisa la Waadventist Wasabato limchukulie hatua za kidhamu mshiriki wao Mafwele

Hakuna mkate mgumu mbele ya chai buana.

Kanisa lolote ukiwa na kibunda wewe ni mfalme ndani ya hiyo himaya.

Hakuna imani ambayo inaweza kumtenga tajiri hata akiwa jambazi labda akamatwe na kushitakiwa na serikali hapo ndipo kanisa litatoa adhabu.

Hakimu na mwenye mamlaka wanasema ni Allah, mwenyeezi Mungu tu, ndiye anaweza kufanya tofauti na makanisa.

Vijana tafuteni pesa mpate ufalme wa dunia kila pahala.
 
basi naomba kanisa limhoji ndugu Mafwele na ashike Biblia mbele ya baraza la kanisa aape kama kweli hahusiki na tuhuma zinazotajwa dhidi yake.🥺🤔🙇🏿‍♂
 
Ellen G. White amekataa waumini kufanya siasa, amesema kazi pekee waliyonayo ni kueneza ujumbe wa malaika watatu.
Ellen G. White is not the authority of the church, neno lake sio amri, yeye alikuwa muumini kama wewe na mimi.

Ellen G. White alishauri waumini wa SDA wasijihusishe na siasa kwa sababu ya nature ya hayo mambo, ila hakuna marufuku au kufutwa ushirika ukijihusisha na siasa, kumbuka sio siasa zote chafu, kuna watu wanakuwa viongozi wanasaidia kweli watu, nikuulize swali kama Tanzania wote tungekuwa wasabato, na tumepigwa marufuku ya siasa nani angekuwa raisi sasa?? Nani angekuwa waziri??
Mama white ametuasa tujihusishe na siasa safi na sio siasa cha kuuana na machukizo kama zinazoendelea hapa Tz.


Just Think.
 
Naunga mkono hoja.
Kua mwaminifu, Mtii Mungu zishike Sheria za Nchi, Heshimu jamii mwisho Enjoy haya makanisa ni miradi ya watu utayataabikia sana na mwisho yatakusaliti na hayajawahi kua ja msaada wa kueleweka kwenye maisha zaidi ya kuaminishana umoja wa kinafiki.
 
Na jee; akiwa mwadilifu roho ya unabii inasemaje kwa hilo?
Roho ya Unabii, Roho ya Unabii......Bado manabii wa kweli wapo ck hizi au ni hawa matapeli wapiga hela?? (ref. Mathayo 24:11-24.)
 
Bro we ni msabato??

Mbona unatunga sana mambo
 
Nadhani Sasa ataanza kuvaa miwani nyeusi, mizura (boshori) kama Soudy Brown Kwa tunakoelekea,mwisho utaskia akutwa amejinyonga
 
Kwahiyo huamini kuwa alikuwa nabii? Hakuna sehemu yoyote ambayo ameshauri watu wajihusishe na siasa
Hujanielewa, nimesema alikuwa muumini kama mimi na wewe haimanishi nimemvua unabii wake au nimeshusha vyeo, lahasha ila nilichosema Mama White sio authority, authority ni Yesu pekee.
Ndio alishauri tusijihusishe na siasa, ila ni kwasababu ya nature ya siasa na siasa kwasababu ya siasa itself, kwan what is siasa?? Mtu akisema siasa za ujamaa unaelewa nn? Mtu akisema siasa za kipebari unaelewa nn??

Ndo maana nikasema sio siasa zote chafu.
 
Kua mwaminifu, Mtii Mungu zishike Sheria za Nchi, Heshimu jamii mwisho Enjoy haya makanisa ni miradi ya watu utayataabikia sana na mwisho yatakusaliti na hayajawahi kua ja msaada wa kueleweka kwenye maisha zaidi ya kuaminishana umoja wa kinafiki.
Mmmmh! 1. Kuwa mwaminifu✅
2. Mtii Mungu✔️✔️✔️
3. Zishike Sheria za nchi ☑️ it is subjective
4. Heshimu Jamii ☑️ It is subjective
5. Enjoy✔️
6. Haya makanisa ni miradi ya watu...............kuaminishana umoja wa kinafiki ✖️
 
Sawa. Je, ni kila kosa hufanyika hadharani kwa mujibu wa kanisa? Je, kwa mfano mtu amebakwa vichakani/porini huko kusiko na aliyeshuhudia tukio; sio sahihi kwamba aliyebakwa anasimama kuwa ndiye shahidi #1 wa kuaminika? Unamchukuliaje Sativa.
Kuepuka uzushi na sababu kanisa halikuweko huko vichakani

Hiyo kesi ikipelekwa mahakamani ikathibitika alibakac kanisa litachukua hatua mara moja tena kwa speed ya mwewe ikitoka tu hukumu
 
Wao si mahakama, kuna mipaka of which kanisa mamlaka yake yanaishia wapi
 
Mwimbaji yupi huyo?
 
Sawa endelea kuokotwa ukitosheka utapumzika, Watu wamepigwa tangu enzi za Dr Livingston na hakuna cha maana kanisa limefanya hushtuki?
 
Mwimbaji gani vilee
Au Marco?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…