Kanisa limepiga marufuku wanasiasa kusalimia kanisani, wamekosea sana

Walichelewa sana kufanya maamuzi hayo, matokeo mazoea!
Hata mikutano ya chama/serikali salamu iwe moja tu.....Jamhuri ya Muugano wa Tanzania...Kazi iendelee...
Haya mambo ya Tumsifu Yesu Kristo; Bwana Yesu Asifiwe; Mwanakondoo Ameshinda; Asalaam Alaykhum... tuyaache makanisani au misikitini.
 
Hayo mahitaji uliyoorodhesha sio hisani yote ni ya lazima kwa kila raia wa Tanzania!! Maan ndizo kodi za wananchi!! Ataeumia ni yule asietenda haki!!
 
Kwani kanisa linaendeshwa na serikali, yaani serikali inatoa ruzuku au ni kupitia sadaka na ufadhiri wa nje. Pia walichelewa kutoa matamko kama haya
 
Usichanganye dini na siasa,jiulize bungeni wageni huwa wanatoa neno?
 
Hapo ni katoliki unaongelea. Taasisi ya kidini yenye uchumi mzuri kuliko zote nchini
Unadhani watu hawajui kama Nyerere, Mkapa na Magufuli wote walikuwa wakatoliki? Unadhani hii ilitokea tu by chance?
 
Wao walimwaga mboga, sasa wenzao wamwemwaga Ugali kabisa
na kuosha chungu Cha ugali no ukoko.
Walipokuwa wakisema kwamba Viongozi wa Dini waache siasa wao ndo walikuwa wanakosea kabisa, kwani Siasa ni maisha, na kila Mwanadamu lazima siasa imguse Kwa namna moja au nyingine.
Ndo kwanza mwanzo!
 
Ccm ndiyo itakayo umia Kwa ujumla.
 
Mbona unakosa akili za kuzaliwa?
Kwa nini usiseme wakulima nao wasalimie kwenye vyombo vya kuabudu.
 
Kanisa na serikali nani anamuhitaji mwenzie sana? Bahati nzuri au mbaya ushindi hautegemei kura nyingi tu, muulize Nape atakutonya.
 
Fedha za Mchungaji zinatoka kwetu waumini sadaka na michango lakini fedha za waumini zitatoka kwa Mungu kwa maombi, kutoa sadaka na kufunga. Ugonjwa wa Mchungaji utapona kwa kuchangiwa pesa za matibabu na waumini lakini afya ya muumini itapatikana madhabahuni kwa kupmbewa na kutoa sadaka. Ndugu zangu ujinga huu hadi lini? Babu yangu aliniambiga kuwa wajinga hawaishi hadi Dunia itakapokwisha.

Watu wa dini wanadhani kuwa serikali inafahamu wizi wanaofanya kuwaibia raia kwa kisingizio cha Mungu na shebani/ibilisi.

Mungu yupo kweli lakini anachohitaji kwetu ni wewe kumshukuru tu kwa Kila jambo. Mungu hataki fedha maana fedha tumetengeneza sisi wanadamu kwa utundu wetu. Mtu anakusanya fedha akidai ni sadaka ya Mungu ni mwizi wa Hila sawa na wezi wengine.

Mungu hana mdomo Wala matumizi ya sadaka zetu bali zinaliwa na wanaozikuaanya. Kila kitu ni mali ya Mungu na vitu vyote ni vyake na vinatoka kwake hivyo hahitaji chochote kutoka kwetu zaidi ya kumuamini na kumshukuru tu kwa Kila jambo.
 
Wewe Tizo wa Mburahati unawadanganya watu hapa eti Serikali inaweza kulifutia usajili kanisa katoliki.

Bahari haipimwi kwa mtete.
 
Wewe Tizo wa Mburahati unawadanganya watu hapa eti Serikali inaweza kulifutia usajili kanisa katoliki.

Bahari haipimwi kwa mtete.
Kwa akili Yako ndogo unadhani kuwa kanisa liko juu ya serikali. Kwaakili Yako pia unadhani makanisa yote nchini yamesajiliwa kwa mujibu wa sheria na taratibu na kanuni, na yamepewa miiko na mistari ya kuzingatia usivukwe.
 

Hakuna taasisi yoyote ile humu nchini ambayo ni serikali proof au serikali resistant. Itategemea na unyeti wa jambo lenyewe.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…