Kanisa limepiga marufuku wanasiasa kusalimia kanisani, wamekosea sana

Kanisa limepiga marufuku wanasiasa kusalimia kanisani, wamekosea sana

Labda maana yake ni kwamba serikali ina uwezo wa kufuta si tu kanisa bali hata kufuta kila kinachohusiana na kanisa zikiwemo hizo huduma za kijamii ulizozitaja,watu wana jeuri aisee!
kama unaweza kusajiri utashindwaje kufuta usajiri?
 
Vizuri sana ila wakiwa na halambee wasiwaalike pia kutaka michango yao
Wataalikwa kama waumini wengine. Hii itasaidia hasa kipindi hiki cha kampeni, ambacho wanasiasa hupendi kujiongezea political Mileage kwa kupenda kuzungumza madhabahuni. Madhabahuni ni sehem Takatifu, paheshimiwe
 
Kama wiki mbili zilizopita tupo msibani Mhe Diwani alipewa nafasi ya kuongea neno baada ya kumaliza alichoongea akawaambia waombolezaji wapige makofi mengi kwa mama aibu iliyompata anaijua mwenyewe.
hawakujua watendalo, mama amepewa na katiba uwezo wa kufuta hati na kubadilisha matumizi ya ardhi, kama akiona inafaa anaweza kubadilisha matumizi ya eneo lile la msimbazi center pale kuwa maegesho ya bodaboda/wapiga kura wake.
 
hutaki mwanasiasa asalimie kanisa af unataka achangie mifuko Mia ya cement ......
Wash e NZI kweli.

Mwanasiasa asipopewa priority kanisani, viongozi wa dini watalala njaa.
Siku wakatoliki wakisema waumini wao wasiende kupiga kura ulishwahi kufikiria ilo
 
Na wanasiasa waache kuita watu wa dini kuomba kwenye mikutano yao, kwanza sala na Dua zenyewe zinakuwa za mashaka sidhani hata Mola anazikubali, walinde tu polisi inatosha!
 
Si wae
Kanisani ni mahali pa ibada, watu wamekuja kusali, hivyo blah blah za wanasiasa hazina nafasi. Kanisa katoliki lilichelewa sana kuja na hilo tamko.
nde huko kwenye makanusa mengine wakahubir mambo yao? Kwani lazima RC? Waende kwa Gwajima.
 
Kanisani ni mahali pa ibada, watu wamekuja kusali, hivyo blah blah za wanasiasa hazina nafasi. Kanisa katoliki lilichelewa sana kuja na hilo tamko.
Tunasubiri tamko la kukataa kupokea Rudhuku kutoka kwa wanasiasa ambao kimsingi ndio wapitishaji kwamaana ya Serikali iliotokana na wanasiasa hao wanaokatazwa kusalimia kanisani.
 
Kanisa ni asasi ya kiraia inayohitaji ulinzi na huduma nyingine za kiraia kama polisi, maji, umeme, barabara, usajiri, misamaha ya Kodi, ardhi, nk. Waumini ni raia pia wanaishi kwenye jamii. Huduma zote hizi zinategemea wanasiasa ili zipatikane kanisani pia.

Kupiga marufuku wanasiasa kwenda kusema chochote kanisani bila kubagua anatoka chama gani ni vita nyingine kati ya kanisa na mamlaka.

Sijui nani ataumia kama ikiwa hivi.
kwa hiyo kampeni zao satapigia wapi? wapi watatukuzwa kwamba ni chaguo la mungu?
 
Vizuri sana ila wakiwa na halambee wasiwaalike pia kutaka michango yao
Huwa hawaalikwi bali wanajialika wenyewe for politics milage.

Yaani Padri anaumizwa vile na hakana tamko lolote la serikali la kuwashughulikia wahusika. Halafu wake wapande Madhabahuni bila aibu kuendesha siasa uchwara, eti Kanisa liwaache??
 
Ni wakati wa Serikali kuanzisha Makanisa yake kama ni rahisi...!

Lazima kuheshimu Taasisi zingine.
 
Kanisa ni asasi ya kiraia inayohitaji ulinzi na huduma nyingine za kiraia kama polisi, maji, umeme, barabara, usajiri, misamaha ya Kodi, ardhi, nk. Waumini ni raia pia wanaishi kwenye jamii. Huduma zote hizi zinategemea wanasiasa ili zipatikane kanisani pia.

Kupiga marufuku wanasiasa kwenda kusema chochote kanisani bila kubagua anatoka chama gani ni vita nyingine kati ya kanisa na mamlaka.

Sijui nani ataumia kama ikiwa hivi.
Si mlisema dini na siasa zitenganishwe.
 
Siku wakatoliki wakisema waumini wao wasiende kupiga kura ulishwahi kufikiria ilo
Huyo kiongozi ambae atawaawafundisha waumini wake ujinga huo lazima mtamhurumia kwa atakachokutana nacho. Hakuna Mchungaji anaemiliki watu. Na miongoni mwa waumini wapo na watu wa usalama wa nchi, watamnasa tu
 
Vizuri sana ila wakiwa na halambee wasiwaalike pia kutaka michango yao
Ujenzi wa makanisa mpaka yakamilike kwani unategemaga harambee za wanasiasa? kwamba pasipo wanasiasa kusimama kwenye mimbari na kupiga tantalila ujenzi hauwezi fanyika?
 
Ujenzi wa makanisa mpaka yakamilike kwani unategemaga harambee za wanasiasa? kwamba pasipo wanasiasa kusimama kwenye mimbari na kupiga tantalila ujenzi hauwezi fanyika?
Hiyo building permit si wanaipata kutoka serikalini, na kiwanja je?. Jua kuwa ardhi yote ni mali ya serikali, majengo yote ya watu binafsi na private wamepangishwa tu kwa miaka ama 33 au 99, baada ya hapo lazima ukaombe tena , unaweza kukubaliwa au kukataliwa,
 
Back
Top Bottom