Ana cards zipi? Hao Senate wenyewe wamemkatalia kuizinisha dollars zaidi ya bil 200 kwa ajili ya vita ya Iran.Angekuwa na hizo cards si angepata hizo USD bil 200.
Moja ya condition aliyo itoa Iran ni Myahudi kutoishambulia Lebanon na Iran alifungua mlango wa Hormuz baada ya Myahudi kuacha kuipiga Lebanon, Myahudi alipoanza kuipiga Lebanon akafunga tena mlango, sasa hapa mwenye kadi ni nani? Kwa hiyo niache kumuamini Kansela kisa mwanasiasa,kwani Trump unaye muamini wewe ni nani au mwanasayansi?
Halafu unaonekana hata maswala ya diplomasia huyajui, unakaza kichwa. US middle east ushawishi wake unaenda kupungua, hamna taifa litakubali tena ,US kujenga tena base zilizo lipuliwa,Qatar ameshaliongea hilo, Saudi, Bahrain, Jordan, UAE,Dubai wanafikiria kurestructure upya uhusiano wao na US.
EU na NATO wamekataa kumunga US kwenye hii vita, UK akaandaa mkutano wa mawaziri zaidi ya 40 kudiscuss jinsi ya kuufungua mlango wa Hormuz kidiplomasia, huku wakipingana na wazo la Trump kutumia nguvu kufungua Hormuz. Canada mshirika wa kariba wa US ,alikataa live kumuunga mkono US. Italy na Spain walimpiga marufuku US kutumia anga na millitary resources zao kuishambulia Iran,Spain alienda mbali wakaifukuza ndege ya kijeshi ya mizigo ya US iliyotua kwenye uwanja wake.Mpaka hapo unaona ushawishi wa US umepungua na kitendo cha ushawishi kupungua kunatokana na kufanya vibaya upande wa kidiplomasia matokeo yake hata dollars itaanza kupoteza ile nguvu yake sababu imejengwa kupitia ushawishi na ili uwe na ushawishi mkubwa basi kidiplomasia lazima uwe vizuri. Trump mwenyewe diplomasia ana zero kabisa kamtukana Macron, kawaponda NATO na kamtukana Mfalme wa Saudi nk.
Wewe kama unaangalia vita upade wa silaha Pekee yake basi hata dunia hujui inavyo enda, ila hii vita US amepoteza pakubwa sana na bado kila siku anazidi kupoteza.
Haya hiyo jana ,Canada anaanza kujitenga pole pole na US anataka kupunguza utegemezi, Qatar kishaanza na wenzake wengine middle east watafuatia bado NATO na EU.
View attachment 3580992
Kwenye hii vita kwa maana ya physically na kidiplomasia Iran amefanikiwa kuliko US na kwenye uwanja wa kivita kamuexpose US vibaya, sasa washajua weakness zake kwenye uwanja wa kivita kwa maana ya silaha zake, jinsi ya kucheza na mifumo yake ya kiulinzi ya anga pamoja na ndege zakeza F-35,F-16,Refuelling Aircraft Tankers na ndege radar zake zinazo tembea angani.
Haya lengine hili.
View attachment 3581313