Mifuko ya hifadhi za jamii inapata faida kubwa sana,kutokana na uwekezaji wa michango ya wanachama kwenye Treasury Bond na rasilimali zisizo hamishika Kama majengo,madaraja, hostel,na nyumba nk.
Lakini mifuko ya hifadhi za jamii, wakati wa kikokotoa mafao hususani NSSF wanachukua jumla ya michango ya mwanachama kama alivyochangua kwa kipindi chake cha utumishi wake bila kuhuisha na faida iliyopatikana kutokana na uwekezaji wa michango yake au mfumuko wa bei.
Mfuko wa PSSSF wao wanachukua michango ya miezi mitatu ya mwisho, kufanyia kikokotoo Cha mafao ya mtumishi kwa miaka yote ya utumishi wake.
Ushauri
1). Serikali iangalie uwezekano wa kuhuisha mafao ya kila mwezi kwa Wastaafu wa zamani,to take into inflation rate and super profit accruing from membership contribution invested in various ventures.
2). Kwa kuwa NSSF walishaanza kuwalipa Wastaafu 25% malipo ya mkupuo,Ni vema kwa wahanga wa kikokotoo hicho wafanyiwe mapitio na kulipwa stahiki zao.
3). Serikali itoe kanuni kwa NSSF kutumia michango inayotokana na mshahara ya mwisho (Kama wanavyofanya PSSSF) kikokotoa mafao ya wanachama wao.
4). NSSF Iwe inatoa mchanganuo wa mafao ya Wastaafu,kwa maana sasa hivi, imekuwa siri hata mstaafu mwenyewe hapewe.Ni Sheria ya Siri ni kati ya Mteja na taasisi,kwa nini mteja asipewe nakala ya namna mfuko ulivyofikia malipo ya mkupuo na ya kila mwezi.