Kanuni mpya Kikokotoo Inaondoa ubabe wa NSSF. Siasa za Magufuli ziliwabeba waonevu NSSF

Mshahara wako ni shilingi ngapi mpaka zikife mil 200 ulizochangia ?
Hesabu rahisi, nikifanya kazi kwa miaka 36, ukaitafuta miezi iliyopo ndani yake, ukaitawanya hiyo 200m kwa hiyo miezi, kisha ukaipasua kati, utajua kiasi cha mshahara ninachozungumzia hapo!
 
Ni vile tu haturuhusiwi kutukana humu; kuizngumzia SSRA ambayo day one imeingia kazini ikatengeneza mgogoro mkubwa na wafanyakazi kwa kuondoa fao la kujitoa halafu mtu (hapo kwenye mtu ndio nilitaka kutumia neno baya ) anakuja kuisifia? SSRA imeanzishwa kabla ya Magufuli, uwepo wa SSRA ilikua tatizo kubwa, inakula pesa za mifuko halafu haizalishi, jinga kabisa. Rest in peace mwamba Magufuli, wavivu, wezi, majizi na mafisadi ndio wanao furahia your absence.
 
Kumbuka JPM hakuridhia kikokotoo.
Alitoa miaka 5 kiangaliwe upya.
Mpaka anafariki miaka mitano ilikuwa haijafika.
Kama umefanyiwa uhuni pole.
JPM asilaumiwe kwa hili
Uhuni na siasa kuwadanganya wajinga, kama hakuridhia angekataa kisitumike, kitendo cha kusema miaka mitano kingaliwe wakati huo mifuko ikiendelea kutekeleza maamuzi ya bunge maana yake alipiga siasa ili wananchi wasio elewa kama kawaida mshangilie na kupiga makofi. Na yeye akipata hela ya kufanya miradi yake.
 
Nimegundua wengi hamuelewi hii mifuko ya hifadhi ya jamii ni nn na hata maana ya hayo mafao.
 
Watu bado wapo kwente koma awahamini kama mama ndio kashika usukani na abiria wanafuraha swala kikotoo mheshimiwa Rais anatakiwa apongezwe kwa nguvu zote, atleast wastaafu kilio chao kimesikika nyie mnaoendelea kuponda endeleeni gari ndio limeshawaka alitarajii kuzima leo wala kesho ..viva samia.
 
Hapo nimeponda nini sasa?
 
Mhhh Tanzania ina wajinga wengi sana sana!
 
Fao la kujitoa na lirudishwe...
Hili la muhimu aisee, NSSF walinitesa maana mie contract iliisha nikauchuna miezi kadhaa ndio nikaenda kufungua yaani kufika pale wakaja na issue za fao la kukosa ajira (33% ya salary for 6 months) yaani nilitaka kuanguka ukizingatia nilikaa miezi 6 mambo yalivyoanza kuwa tight nikaenda...nikapigwa miezi 2 tena mbele ndo wakaanza kuingiza hiyo hela yao kila mwezi kwa miezi 6. Ilivyoisha mzigo ukakata nikaanza kupambana nilipwe zote nikaambiwa yaani mpaka miezi 18 iishe tangu nilipolipwa mafao ya kukosa (nikapoa kabisa)

Ilibidi nibaki kuhesabu miezi maana barua hawajibu, ukiingia twitter mpaka facebook hawajibu labda kama unatoa pongezi ndio utajibiwa, yaani juzi kati miezi kadhaa iliyopita ndio nikalipwa (nilicho experience hiyo issue yao haifanyi kazi)
 
Mifuko ya hifadhi za jamii inapata faida kubwa sana,kutokana na uwekezaji wa michango ya wanachama kwenye Treasury Bond na rasilimali zisizo hamishika Kama majengo,madaraja, hostel,na nyumba nk.
Lakini mifuko ya hifadhi za jamii, wakati wa kikokotoa mafao hususani NSSF wanachukua jumla ya michango ya mwanachama kama alivyochangua kwa kipindi chake cha utumishi wake bila kuhuisha na faida iliyopatikana kutokana na uwekezaji wa michango yake au mfumuko wa bei.
Mfuko wa PSSSF wao wanachukua michango ya miezi mitatu ya mwisho, kufanyia kikokotoo Cha mafao ya mtumishi kwa miaka yote ya utumishi wake.

Ushauri

1). Serikali iangalie uwezekano wa kuhuisha mafao ya kila mwezi kwa Wastaafu wa zamani,to take into inflation rate and super profit accruing from membership contribution invested in various ventures.
2). Kwa kuwa NSSF walishaanza kuwalipa Wastaafu 25% malipo ya mkupuo,Ni vema kwa wahanga wa kikokotoo hicho wafanyiwe mapitio na kulipwa stahiki zao.
3). Serikali itoe kanuni kwa NSSF kutumia michango inayotokana na mshahara ya mwisho (Kama wanavyofanya PSSSF) kikokotoa mafao ya wanachama wao.
4). NSSF Iwe inatoa mchanganuo wa mafao ya Wastaafu,kwa maana sasa hivi, imekuwa siri hata mstaafu mwenyewe hapewe.Ni Sheria ya Siri ni kati ya Mteja na taasisi,kwa nini mteja asipewe nakala ya namna mfuko ulivyofikia malipo ya mkupuo na ya kila mwezi.
 
Kumbuka JPM hakuridhia kikokotoo.
Alitoa miaka 5 kiangaliwe upya.
Mpaka anafariki miaka mitano ilikuwa haijafika.
Kama umefanyiwa uhuni pole.
JPM asilaumiwe kwa hili
Mkuu hauko sahihi. Sheria ya kubadilisha kikotoo ilipelekwa na kupitishwa bungeni na Jennistèr Mhagama wakati wa JPM. Sheria hii ililalamikiwa sana na wadau na hasa Bungeni. Mbunge wa Kigoma (marehemu kwa sasa) alillamika sana na alisema namnukuu " sheria hii inaenda kuumiza wastaafu".
Ilivyoanza kutumika ndiyo vilio vikaanza hapo JPM akasema kiangaliwe upya, watu wakashangilia wasijue kuwa bila kubadilisha sheria Yale ni maneno tu hayana nguvu ya kisheria. Sawa hivi wastaafu wengi wanategemea wakienda kudai pension yap wanakutana na kikotoo cha JPM kwa sababu mifuko inafuata shèria na siyo maneno.
 
Hapo ni uonevu tu bora mtu apewe mafao yake yote atajua mwenyewe na maisha yake maana serikali haina guarantee ya maisha ya mtu kusema eti umlipe pension kila mwez utajuaje miaka aliyobakiza kuishi baada ya kustaafu..?
Waliopitisha hayo mambo hawajafanya fair mtu apewe chake basi kwan hata akizitumia vibaya wao wanaumia nn..
 
Kwa sasa wanatumia fomula mpya!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…