PreGE2025 Kanuni za Uchaguzi Mkuu; Wabunge, Madiwani, na Mawakala hawatapewa nakala za Matokeo wala hayatabandikwa

PreGE2025 Kanuni za Uchaguzi Mkuu; Wabunge, Madiwani, na Mawakala hawatapewa nakala za Matokeo wala hayatabandikwa

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla)
chaguzi huru, za haki na huru za Tanzania haziendeshwi na upotoshaji au uropokaji kama huo ulowasilisha hapo juu,

Zinaendeshwa kwa mujibu wa sheria na katiba ya na si vinginevyo šŸ’
Sawa weka zakwako AMBAZO hazijapotoshwa Komredi
 
Gentleman,
huu ni upotoshaji na hakujawahi kua na script ya uchochezi kama hiyo kwenye chaguzi za Tanzania.
Matokeo hutangazwa kwenye vituo vya kupigia kura na kubandikwa kwenye mbao za matangazo na kila mTanzania anajua na kufahamu hivyo na sio upotoshaji huo šŸ’
 

Attachments

  • GoY5Z2JWAAAtRrA.jpg
    GoY5Z2JWAAAtRrA.jpg
    84.3 KB · Views: 20
Ninayo pdf nikuwekee ushahidi hapa, au mtafuta Uzi?
Gentleman,
hili ni jukwaa huru la wadau wa siasa sio mambo ya hovyo hovyo ambayo kimsingi lazima yafutwe tu,

na mimi nasema yafutwa tu kwasababu hakuna namna nyingine sasa šŸ’
 
Walioziandaa na Waliosaini hizi kanuni walikuwa na akili zao au walishikiwa. Eti Leo ACT nao wanalipongeza Kanisa Katoliki kama sio unafiki ni nini.

Chadema wako sahihi kabisa. No Reforms, No Election.

View attachment 3310384
Imagine huyu aliyesaini huu ugoro ni Mtanzania aliyesoma kwa shida na ni Baba wa familia Kabisa anayetegemewa
 
Wanaweka Sheria za kwenda mahakamani kudai haki yako ukihisi umeibiwa ubunge halafu wanakutengenezea mazingira ya kukupoka ushahidi, haki unapoteza. Ndo maana wasira anasema " haki Iko ndani ya amani". Yani wanatulazimisha tuendelee kukariri propaganda Yao ya AMANI...AMANI....AMANI.MSITUONE WAPUMBAVU BWANA ARGH!!
 
Mipango ya Wizi live live, halafu wanajaribu kuzuia Wagombea wasiwe na Ushahidi..!

Ni ujinga tu kuingia Uchaguzi Kwa Masharti Aina hii...! Pesa za Uchaguzi zingeenda kufanya Vitu vingine.
 
Walioziandaa na Waliosaini hizi kanuni walikuwa na akili zao au walishikiwa. Eti Leo ACT nao wanalipongeza Kanisa Katoliki kama sio unafiki ni nini.

Chadema wako sahihi kabisa. No Reforms, No Election.

View attachment 3310384
Kwanza tujiulize Faida ya kanuni hiyo ni nini? Kutakuwa na hasara gani iwapo matokeo ya uchaguzi yatawekwa wazi ili wananchi wayajue?

kinacho onekana wazi katika ujinga huu ni kwamba, hiyo tume inatafuta mwanya wa kufanya uovu wake bila ya kuhojiwa na yeyote!
Huku ndiko kuufanya uchaguzi uwe HURU na wa HAKI?

Hizi kanuni zenyewe zinaonekana lengo lake ni kuiruhusu Tume ifanye mambo yake gizani; na tayari inaonyesha kuwa Kanuni ni chombo cha kukandamiza vyama vya upinzani. Tayari CHADEMA wamekwisha tangaziwa kiyama chao, kwa kuenguliwa kwenye uchaguzi wote kwa miaka mitano!
Hii siyo kuikomoa CHADEMA pekee, bali ni kuwakomoa wapiga kura ambao wangependa kukipigia kura chama hicho. Utawanyima vipi wananchi kwa mamilioni HAKI yao ya kuwachagua viongozi wanaowataka.
Unataka mamilioni ya watu hawa wafanye nini ili HAKI yao ilindwe?

Hii tume haifai, na kamwe isiruhusiwe kujishughulisha na maswala yoyote ya uchaguzi ndani ya nchi hii.
 
Wanaweka Sheria za kwenda mahakamani kudai haki yako ukihisi umeibiwa ubunge halafu wanakutengenezea mazingira ya kukupoka ushahidi, haki unapoteza. Ndo maana wasira anasema " haki Iko ndani ya amani". Yani wanatulazimisha tuendelee kukariri propaganda Yao ya AMANI...AMANI....AMANI.MSITUONE WAPUMBAVU BWANA ARGH!!
HAKI kamwe haiwezi kuwa ndani ya AMANI. HAKI ndiyo inayozalisha AMANI.
Popote palipo na HAKI, dhulma, uovu na chuki huondoka.
HAKI HUINUA TAIFA.
 
Back
Top Bottom