Karata nzuri iliyobaki kwa Mbowe ni kufanya maridhiano na Lissu, asisubiri aibu kuu siku ya uchaguzi

Issue sio Mbowe kushinda, issue ni mustakabali wa Chadema mkuu, ndo kinachotazamwa. Yeye atashinda kura za wajumbe ila ajue kwamba Lissu ndo ana mustakabali wa Chadema mpya
 
Hata hiyo 50% umempendelea, impact yake itakuwa ni kubwa sana
 
Umemalizia vizuri kabisa. Tatizo ni nyakati tulizopo ndo zinamkataa Mbowe. Sio kwamba Mbowe ni mbaya, ila nyakati hizi sio sahihi kwake kuendelea kuwa mwenyekiti wa Chama kikuu cha upinzani.

Taifa linavyokuwa kwenye mkwamo wa kidemokrasia, halafu wewe mwenyekiti unaendelea kuwalamba miguu hao hao watesi maana yake ni kwamba umeshindwa kusoma alama za nyakati na unafaa kupumzika.
 
Huu ndio ukweli wenyewe, na wajumbe watakaokuwa na jukumu la kufanya kazi hii bila shaka wanao uelewa huu vizuri vichwani mwao na siyo kwenye matumbo yao.
Na hapa ndipo busara ya wajumbe inapaswa kujionesha, ikiwa wanaweza kutafsiri na kufanya maamuzi kufuatana na mtizamo wa wapenzi na mashabiki wao
 
Na shida kubwa sana, kuna vijana wamepotea wengine wametiwa ulemavu kwasababu ya Chadema, kumbe mwenyekiti yupo na maridhiano ya siri huku wao wakichezea za ugoko. Unadhani ni kijana gani tena atakuwa tayari kufa kwa ajili ya chama?
 
Ahahahahaha!!!
 
Wale wapambe wa mkopo kutokq kwa jirani wapo kazini kumpasupport mipango yao iweze kutimia.
 
Mbowe hata akishindwa atapata heshima kuwa ni kiongozi pekee wa chama cha siasa aliyekubali kushindana na mtu mwenye nguvu na aliposhindwa, alikubali kushindwa. Akishindwa atabakia kuwa mjumbe wa Kamati Kuu wa kudumu. Kama mshindi atakuwa na akili atahakikisha anamtunzia heshima ili asikipasue chama zaidi maana Mbowe nae ana wafuasi wake ndani ya chama. Ni win win situation kwa Mbowe.

Amandla...
 
We mikopo Consultant tusubiri sanduku la kura ! Sasa uliona wapi Mwenye Nyumba eti akakaa kitako na mgeni kujadili eti aondoke au abaki katika nyumba ?? N auliona wapi mpangaji akampa masharti mwenye nyumba wake ??
Kwa CHADEMA Lissu ni mpangaji tu hawezi kujadiliana suala la nyumba na mwenyewe hata kidogo.
Sasa hilo suala la kuridhiana na Lissu waridhiane nini ??
 
Wanachama tuna wazoom, Mbowe atapigwa kipigo cha Mbwa koko. Mda mwalim
 
Wapambe, wakati mwingine ni watu wabaya sana. Wamemdanganya kuwa anakubalika. Lakini ukweli ni kwamba kuendelea kwake kuwa mwenyekiti wa Chadema, wapambe ndio watakuwa wanufaika wakuu, huku uhai wa chama ukiwa mashakani.
 
Mbowe amedanganywa Sana na machawa wake, hakupaswa kuchukua fomu Bali alipaswa kustaafu rasmi na kubaki rasmi kama mzee mstaafu na mjumbe wa kudumu wa kamati kuu wa chama
 
Ndo inavyotakiwa hivo, mambo ya siri siri hayatakiwi kabisa. TAL anaonesha mifano mizuri sana, hiyo ndiyo namna hata serikali inapaswa kuwa.

Mambo ya sirini hayana uwajibikaji
Unaweka mambo ya chama Siri, je ukishika serikali utafanyaje?lissu Yuko smart sana
 
Chama hata kipendwe vipi kama hakina pesa za kujiendesha ni kazi bure. Wagombea itabidi waulizwe watapata wapi pesa za kukiendesha chama? Mbowe ameonyesha kuwa ana uwezo wa kuzipata. Ukweli ni kuwa wachangiaji wengi wa CDM wasingependa majina yao yajulikane. Haswa wale wanaofanya biashara na serikali au wamo serikalini. Hawa wanajua wakimpa mchango wao anaweza kuufikisha bila kuwataja. Mbowe akitoa milioni 10 hamna atakayemuuliza amezitoa wapi. Sidhani kama watakuwa na imani hiyo kwa Lissu ambae amesema hataki siri. Kwa sababu hiyo atapata changamoto katika kuzikusanya. Hali hio inaweza kuwafanya baadhi ya wajumbe kumpigia kura Mbowe hata kama wanaelemea kwa Lissu.

Amandla...
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…