Wana JF wenzangu wakubwa kwa wadogo, kuna kitu kinaitwa Environmental research, utafiti wa kimazingira. Watu wanaoishi na makada wa ccm wamethibitisha hali hii ambayo haijawahi kutokea ndani ya chama cha mapinduzi, kuwa takribani kila kada wa ccm ndani ya dakika tano anamfikiria Tundu Lissu eidha kwa mabaya au mema.
Hakuna hata kada yoyote wa ccm ambaye ameweza kukaa kwa muda mrefu bila kumuwazi Tundu Lissu. Mjomba wangu ambaye ni kada maarufu na mfia ccm amedai kuwa Tundu Lissu anamsababishia presha maana akimuwazia tu moyo unashituka, hivyo anamkosesha raha maana ana wasi wasi na jinsi anavyoungwa mkono na watu wengi. Mbaya zaidi ni pale anapoona baadhi ya makada wenzake kumuongelea vizuri kwamba Tundu Lissu ni msafi na ndiye anayemkabili Mh. Magu vilivyo.
Baba yangu mdogo yeye ni kada mtiifu wa CCM lakini wanatofautiana sana na mjomba wangu kwa kumuwaza Lissu kila mara kama mkombozi na mwenye uthubutu wa kumsema Mh.Magu bila kuogopa, maana baba mdogo anasema kuwa Magu anafanya kazi vizuri lakini ana kauli na kiburi cha kufikiri yeye ndio mtanzania anayejua mambo yote kuliko wengine na mwenye uchungu kuliko wote kitu ambacho anasema siyo kweli. Jambo lingine baba mdogo anasema ndani ya ccm wapo watu wengi ambao wanampenda Lissu kwa sababu hana tuhuma halafu amekuwa akitetea rasilimali na wananchi siku zote. Utafiti wa kimazingira umeonyesha makada wa ccm wanamuwazia Lissu sana kila baada ya 1-5 hadi tano lazima wafanye hivyo.
Hitimisho ni kwamba hakuna aliyetarajia ndani ya chama cha mapinduzi kama angetokea mtu yeyote katika uchaguzi huu ambaye angeweza kuleta changamoto kama Lissu anavyofanya leo. Kila mmoja alitarajia kuwa ccm isingeweza kutumia nguvu kubwa kunadi mgombea wao, ila mambo yamekuwa tofauti na matarajio. Hali ilivyo sasa inatisha maana kuna wasi wasi kwamba Lissu anaweza kuchukua nchi ndio maana imeanza kutumika nguvu kubwa ya vyombo vya dola na tume ya uchaguzi. Kumbuka mwanzoni mwa kampeni, mgombea wa Urais ccm alidai picha za mafuriko ya Lissu ni za 2015, makada wengine wakasema ni zakuedit, leo wanadai wanaofurika kwa Lissu siyo wapiga kura maana hawajaandikishwa. Lissu makada wa ccm wanakuwaza sana.