Kardinali Pengo katika ibada ya kipaimara inayofanyika jimboni Dar es Salaam muda huu anazungumzia hali ya hofu iliyotanda nchini na kuifananisha na hofu waliyokuwa nayo mitume baada ya Yesu kuuwawa.
Mwadhama anasema hali hii haijapata kujulikana Tanzania na sababu za mauaji haya hazijulikani wazi ni nini. Asema ni madhambi gani yaliyopelekea Tanzania yetu kupitia hali hii?
Kardinali anawataka watu kujiuliza je, wanashiriki katika kuleta hali ya hofu? Anasema suluhisho sio nguvu za silaha wala majeshi, bali ni msamaha na maendoleo ya dhambi.
Mwadhama anasema watanzania wanalia hawaipendi hali hii. Anawataka vijana wa kipaimara kuondoa hofu kwa jamii. Anamalizia kwa kuwataka Wakatoliki kuwa chanzo cha kuondoa hofu na kuleta amani nchini.