Kardinali Pengo atua ofisini kwa Paul Makonda kumfanyia maombi maalumu ya baraka na kumpongeza kwa uteuzi

Dr....
Nimerejea kwako.

Nimekuitika na kuandika historia ya TANU ilivyofungamana na dini.

Soma majibu ya post yangu.
Yametoka matusi.

Huna la kusema?

Mimi nikishaona mtu anatukana basi humwepuka kabisa.

Sijibu matusi.
Humnyamazia.
Mzee niwie radhi, ungeingia kwenye profile yangu ungeona last time nilikuwa online Saa ngapi hapa JF.

Ndio nimerudi nyumbani Saa hizi, nitadeal na kila aliyekutukana, Mimi ni mtoto wa Mjini born at ocean road.
 
Hivi kwanini huyu RC anapenda makamera kiasi hichi, na hizo zote ni gharama zake binafsi na kila tukio anataka lirushwe kwenye mitandao, hapa kuna kitu sio bure, kama sio malengo maalum ya serikali ili vijana wapoteze muda wao mwingi kujadiri upambuvu na kuacha mambo muhimu basi ni ujinga wa hali ya juu.
 
Ya Mungu mpe Mungu, ya kaisari mpe kaisari! Unafikiri atamuanika mganga wake wa kienyeji ili mumuone? Katika ccm hakuna Mungu!
 
Hahaha Nchi hii kuna wakuu wa mikoa wangapi au kuna mikoa mingapi na kwanini aombewe huyu yeye tu kila siku?
Kardinali anazunguka mikoa yote au wanafanya show Arusha pekee?

Kuna vitu hata havina tija, Kateuliwa kwa sababu wanaamini anaweza kufanya kazi iliyombele yake.

Afanye sasa, kesha ogopa au anatishwa na kivuli chake mwenyewe?

Maombi kila siku ya kazi gani? Kazi ataanza lini?
 
Mkuu Nguruvi3 , tena kuna mengine hayajasemwa, CAG Prof. Assad alipokua CAG, kwa vile yeye ni mtu wa swala 5, alijenga chumba maalum cha kuswalia, kwenye ofisi ya umma!.

Mimi naendelea kusisitiza, nchi yetu haina dini na serikali yetu haina dini bali watu wake wana dini zao!, hakuna ubaya wowote mtu yoyote, kuja kuombewa na kiongozi wa dini yeyote maombi ya kawaida, kwenye ofisi za umma. Maaskofu waje, mapadre waje, masheikh waje, mitume na manabii waje, hata watu wa tunguli pia waje!.

Kitu ambacho sio right ni kufanya any religious rites kwenye ofisi ya umma!. Huwezi kufanya adhimisho la misa, ibada, sadaka, kafara, manyanga, au kuleta tunguli!.

Sala tuu hazina shida yeyote!. Ila pia Tanzania tuna shida fulani kwenye udini na siasa za nchi yetu, mimi nimefanya observation kwa muda mrefu, kila rais wa Tanzania anapokuwa Mkristo ni lazima awe Mkatoliki!. Nikajiuliza jee inatokea tuu by chance, it's just a coincidence, or it's a premeditated moves?. Nasubiria atakayefuatia baada ya Samia, then nita confirm!. Niliuliza Kama Sauti Hii ni Sauti ya Kweli, Nimeelezwa Mpango Ndio Mpango Mzima!. Swali ni... Akiwa Mkristo, Kwanini ni Lazima Awe Mkatoliki?!
P
 
Sasa mbona Ramadhan Dau aliitwa mdini?

Au tatizo ni Uislamu?

Tukianza kuleta duwa za masheikh kwenye ofisi za umma mtulie hivyohivyo na duwa tamu tutaleta na madufu ya watoto wa madrasa.

Cc: Mohamed Said
Dau iliitwa mdini kwasababu kadhaa wa kadhaa, naomba nisizitaje hapa, rukhsa kuleta kila aina za dua za masheikh hata wa kutoka Mecca, ila dufu, sadaka, kafara, na albadir, hapana!.
P
 
Huachi kwenda kwenye nyumba ya ibada kwasababu tuu umekwazika au fulani amekukwaza!.
P
 
Haya mambo ya imani za watu na kazi za utumishi wa uma vina uhusiano gani? Mbona nchi zilizoendelea huwa hatuayoni au wanatuficha.

Hapa kwetu watawala badala ya kufanya kazi zao wao wako na matukio ya ajabu ajabu tu.
Hizi ofisi huwa zina mpango kazi/Job description na qualification au huwa wanagawa tu kama zawadi?

Huwa natamani nifahamu majukumu yao ni yapi na yanatekelezwaje yani ile instrument ya kazi inamtaka afanye nini ili asipofanya tumuhoji. Yani kila mkuu wa mkoa au wilaya anasarakasi zake hakuna uniformity.

Tuna vyeo vingi lakini hakuna tija, halafu tunalalamika hatuoni maendeleo, Yatatoka wapi kama pesa zote wanalipwa watawala?

Kwani Rais hana uwezo kupunguza idadi ya mikoa au wilaya ni kuongeza tu?
 
I seee this how CCM leaders to fool Infront of our eyes, Mimi naona wote wanahitaji maombi 😂
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…