Kardinali Pengo atua ofisini kwa Paul Makonda kumfanyia maombi maalumu ya baraka na kumpongeza kwa uteuzi

Kardinali Pengo atua ofisini kwa Paul Makonda kumfanyia maombi maalumu ya baraka na kumpongeza kwa uteuzi

Wewe huwa una chuki binafsi na watu inayokupofusha akili na macho. Chuki yako na hasira yako ni kwa kuwa umeona wamefika ofisini kwa Mwamba Makonda wakati wewe kila siku unaombea na kutamani mabaya yampate na atolewe hapo alipo. Napenda kukwambia tu kuwa hutafanikiwa hata kidogo na chuki zako. Makonda Mwamba ataendelea kusonga mbele kwa kuwa ameinuliwa na mkono wa Mungu na siyo mwanadamu aina yako
Kuna mtu aliwahi kumwita Jiwe Mh Mungu, tena zamani alikuwa anaheshimika kabisa. Sasa mtu kama wewe kuandika ujinga kama huu sidhani kama kuna jipya. Ila kuwa makini sana usije ukaleft group
 
Ndugu zangu Watanzania,

Kilichopatikana kwa Maombi hulindwa kwa Maombi na kilichopatikana kwa uchawi na makafara hulindwa kwa uchawi na makafara yakiambatana na matambiko yasiyo kwisha. Kwa kuwa Mwamba Mwenyewe Makonda amekuwa akipata vyeo na nafasi mbalimbali za uongozi ndani ya serikali na chama kwa njia ya maombi kwa Mwenyezi Mungu na hatimaye kujibiwa ,ndio maana ameendelea kujiweka karibu sana na Mungu,ndio maana ameendelea kujinyenyekeza mbela za Mungu na kumuomba Mungu kuendelea kuwa ndani yake na kumtangulia katika kazi zake.

Ndio maana viongozi mbalimbali wa kidini kutoka madhehebu mbalimbali wameendelea kumiminika ofisini kwake kumuombea na kumpa maneno ya hekima na baraka katika utumishi wake, wa kuwatumikia wana Arusha kwa haki na upendo kwa uweza wa Mwenyezi Mungu Mwenyewe.

Baada ya hapo majuzi Mtumishi wa Mungu Mwamposa kufika Ofisini kwa Mwamba Mwenyewe Makonda kumfanyia maombi na kufanya naye mazungumzo.leo tena kiongozi mwingine na mtumishi wa Mungu aliyewahi kuteuliwa na PAPA kiongozi mkuu wa kanisa katoliki Duniani kuwa Kardinali pekee hapa nchini leo hii ametua kwa kishindo kilichoiteka kanda ya kaskazini.

Huyu ni askofu mstaafu wa jimbo kuu la Dar es salaam Kardinali Pengo.ambapo amefika ofisini kwa kijana wake na kumpongeza sana tena sana na kwa upendo mkubwa kwa heshima kubwa sana aliyoipata ya kuendelea kuaminiwa na Mheshimiwa Rais wetu mpendwa na Jemedari wetu kipenzi cha watanzania Mama Samia Suluhu Hasssan ya kuongoza mkoa wa Arusha. Sanjari na hayo amemfanyia maombi maalumu ya kumuombea baraka na neema katika uongozi wake.ili jiji liendelee kuwa na amani na utulivu.Kardinali Pengo hakuwa peke yake bali aliambatana na viongozi mbalimbali kutoka kila pembe ya nchi yetu tena wa ngazi za juu kabisa alipowasili ofisini hapo.

Ndugu zangu Watanzania nilishawaambieni sana kuwa acheni kushindana na mwamba Makonda.huyu ni mpango wa Mungu,ameinuliwa na Mungu Mwenyewe.mtahangaika na kushindana naye lakini hamtaweza kumshusha kileleni. Mtavaa na kuvalishwa mahiriizii na kutambika ili mumshushe lakini hamtaweza.mtatoa kila aina ya makafara ,kujichanja kila aina ya madawa na kubaki na chale tupu miilini mwenu utafikiri mlidondokea kwenye kiwanda cha nyembe lakini hamtaweza kumshusha Mwamba Makonda kilele.

Huyu Mwamba analindwa na maombi na mkono wa Mungu Mwenyewe.ndio maana mnaona anavyojiamini kwasababu Mungu yupo ndani yake.na Mungu akiwa ndani yako huwezi kuingia gizani maana yeye ni nuru na mwanga usiozimika. Aliyepewa kapewa tu ndugu zangu.sisi wengine tuendelee na kazi tu kwa kadri Mungu alivyo tupangia. ..

Msaidizi na katibu binafsi wa Mheshimiwa Rais Mheshimiwa Waziri Rajabu amewahi kuandika katika mtandao kuwa usishindane na nyakati zinapokuwa kwa mwenzako .lakini pia heshimu nyakati na wakati unapokuwa kwa mwenzako ili nawe uje uheshimiwe wakati utakapo kuwa upande wako kwakuwa nyakati huzunguka..huu ni wakati wa Mhessimiwa Makonda uliopangwa na Mungu mwenyewe kuwatumikia watanzania.tumuache afanye kazi na tuache Majungu ndugu zangu.

Mimi sinaga wivu kumpongeza mtu anayefanya vizuri.ndio maana inafika wakati watu wananiita chawa wa mtu fulani na wengine wakifikia hadi hatua kufikiri kuwa nalipwa.mimi ukifanya vizuri huwa sina hiyana kukupongeza,.ndio maana huwa nampongeza sana Mheshimiwa Rais kwa uchapa kazi wake. Makonda ni mchapa kazi sana ndio maana nampongeza kwa uchapa kazi wake, uzalendo na ubunifu wake katika kutekeleza majukumu yake.

Kazi iendelee, mama Ametufikia na kuwafikia watanzania kwa utumishi wake uliotukuka wa kugusa maisha ya watanzania wanyonge wasio na Sauti.

Lucas Hebel Mwashambwa, Kijana mzalendo na mpenda nchi yangu.

PIA, SOMA:
Mimi ni Mkatoliki na nilikwisha sema muda mrefu. Hakuna la maana lolote ambalo huyu MUUAJI anachota kutoka kwa huyu Kadinali MNAFIKI Pengo.

Ho wawili Bashite na Pengo wakati wa Magufuli walikuwa ni Pete na chanda
 
Wewe huwa una chuki binafsi na watu inayokupofusha akili na macho. Chuki yako na hasira yako ni kwa kuwa umeona wamefika ofisini kwa Mwamba Makonda wakati wewe kila siku unaombea na kutamani mabaya yampate na atolewe hapo alipo. Napenda kukwambia tu kuwa hutafanikiwa hata kidogo na chuki zako. Makonda Mwamba ataendelea kusonga mbele kwa kuwa ameinuliwa na mkono wa Mungu na siyo mwanadamu aina yako
Mwamba mwenye mzigo kama barmaid wa kimboka!
 
Mimi ni Mkatoliki na nilikwisha sema muda mrefu. Hakuna la maana lolote ambalo huyu MUUAJI anachoto kutoka kwa huyu Kadinali MNAFIKI Pengo.

Ho wawili Bashite na Pengo wakati wa Magufuli walikuwa ni Pete na chanda
Acha kuwadhalilisha viongozi wa Dini kwa lugha za kuudhi.
 
Kuna mtu aliwahi kumwita Jiwe Mh Mungu, tena zamani alikuwa anaheshimika kabisa. Sasa mtu kama wewe kuandika ujinga kama huu sidhani kama kuna jipya. Ila kuwa makini sana usije ukaleft group
Endelea kuwa na mawazo ya kijinga na kishetani hivyo hivyo.
 
Wewe,nyamitako na huyo pengo wote hamna akili pumbavu kabisa
Nyamitako mwenyewe sasa:
Screenshot_20240415_144044_Gallery.jpg
Screenshot_20240415_144237_Google.jpg
 
we ni wa kufuatiliwa kila hatua nyau, mpaka tujue useme unayemtumikia.

unajifanya upo upande wa mama, kumbe unampaka mafuta kwa mgongo wa chupa.

chama chako tunakijua, rais unayemtaka 2025 tunamjua, na mpaka unavyotaka iwe kama mama samia akishinda tunajua.

we ni mtu mnafiki na hatari kwa ustawi wa taifa letu.
 
Mbona hueleweki na unakuwa ni kama mgonjwa aliyechanganyikiwa vile?
 
Back
Top Bottom