Kardinali Pengo atua ofisini kwa Paul Makonda kumfanyia maombi maalumu ya baraka na kumpongeza kwa uteuzi

Kardinali Pengo atua ofisini kwa Paul Makonda kumfanyia maombi maalumu ya baraka na kumpongeza kwa uteuzi

Hili jambo halikupaswa kutendeka katika Ofisi ya Umma.

Haiwezekani Viongozi wadai kutochanganya siasa na dini lakini wanafanya kinyume
Hivi akitokea Mufti wa Waislam naye anamuombea dua mtu wake Ofisini namna hiyo, tunaipeleka wapi nchi?

Mh Rais, huioni hatari hii? Hivi kweli Nyerere angelikubali hili kitokee?

JokaKuu Pascal Mayalla
 
Hili jambo halikupaswa kutendeka katika Ofisi ya Umma.

Haiwezekani Viongozi wadai kutochanganya siasa na dini lakini wanafanya kinyume
Hivi akitokea Mufti wa Waislam anamuombea dua mtu wake Ofisini nanmna hiyo, tunaipeleka wapi nchi?

Mh Rais, huioni hatari hii? Hivi kweli Nyerere angelikubali hili kitokee?

JokaKuu Pascal Mayalla
Acha wivu wako wewe. Mmeanza kuweweseka kama kawaida yenu machadema
 
Inafurahisha kuona Keyboard warriors wakidai wao ndio wanaoujua Ulimwengu wa Imani zaidi ya Dizaini za Kadinali!

Wacha nicheke kwanza, naomba nicheke😂😂😂😂😂😂😂🤦🏾‍♂️

Haya magaidi yanamkufuru Mungu Muumba?

Inashangaza na kuchekesha.
 
Kanisa Katoliki Tanzania kwanini mnaacha Makonda anatumia udhaifu wa Uzee unaomsumbua sasa Kadinali Pengo Kujijenga zaidi Kisiasa kwa Maslahi yake ya Ndoto ya kuja kuwa Rais wa Tanzania hasa mwaka 2030? Kanisa langu Katoliki ule Umakini wenu ninaouheshimu mliokuwa nao katika Sakata la DP World mbona siuoni katika huu Upuuzi wa RC Makonda dhidi ya Kadinali Mstaafu Pengo?

Makonda acha kupoteza muda na Kuhangaika hutokuja kuwa Makamu wa Rais au Rais wa Tanzania hata Siku moja Ok?
 
Huwenda Mh. Paul alishindwa kuongea lugha moja na Mwadhamu Askofu Amani hasa kuhusu madawa ya kulevya.

Mh. Paul aliwahi kujipambanua kupambana na madawa ya kulevya kipindi akiwa RC wa Dar, na Baba Askofu aliliongelea swala la madawa kweye azimisho la Hayati Sokoine.

Najaribu kuwaza jambo, huwenda Baba askofu alikuwa anaongea jambo na Mh. Paul lakini hakueleweka hatimaye kukosa majibu pale pale.

Namuamini sana Baba askofu Amani na ni moja ya maaskofu wenye ujasiri, msimamo na ngangari kweli. Huyu aliwahi kueleza msimamo fulani sijui ulikuwa ni wake binafsi au wa kanisa enzi za Mwendazake hasa kuhusu taasisi za elimu zinazomilikiwa na kanisa.

Huwenda Baba Kadnali ameenda kutetea jambo lile lile na Mh. Paul, pengine ndio msimamo wa kanisa kwa Arusha kwa sasa.

Sina majibu mimi nawaza tu.
 
.leo tena kiongozi mwingine na mtumishi wa Mungu aliyewahi kuteuliwa na PAPA kiongozi mkuu wa kanisa katoliki Duniani kuwa Kardinali pekee hapa nchini ,Huyu ni askofu mstaafu wa jimbo kuu la Dar es salaam Kardinali Pengo.
Asante kwa uzi huu, Muadhama Polycarp, Kardinali Pengo, sio Kardinali pekee nchini, alitanguliwa na Muadhama Lauriani, Kardinali Rugambwa, na sasa pia tuna Kardinali Rugabwa mwingine!.
P
 
Hili jambo halikupaswa kutendeka katika Ofisi ya Umma.

Haiwezekani Viongozi wadai kutochanganya siasa na dini lakini wanafanya kinyume
Hivi akitokea Mufti wa Waislam naye anamuombea dua mtu wake Ofisini namna hiyo, tunaipeleka wapi nchi?

Mh Rais, huioni hatari hii? Hivi kweli Nyerere angelikubali hili kitokee?

JokaKuu Pascal Mayalla
Mkuu Nguruvi3 , serikali ndio haina dini ila watu wake wana dini zao, hakuna ubaya wowote, viongozi wowote wa dini, kumuombea, ofisini kwenye ofisi ya umma, and soon utamshuhudia Mufti, Malasusa, na Yuda Thadei Ruwa Ichi!.
P
 
Kiimani kila mmoja anawajibika kwa anayoyatenda,huyu anapenda dhambi ile yule anaichukia,kuwa Mkatoliki hakumuondolei mtu kuwa na avipendavyo au kukengeuka.

Kanisa Katoliki siyo la mtu mmoja kiasi kwamba hata akitenda jambo lionekane litayagusa maisha ya waamini wenzake moja kwa moja,kama ingekuwa ni hayo makanisa ya mabati ya mifukoni ndiyo muhusika angejiuliza mara mbili mbili mbili.
 
Back
Top Bottom