Kardinali Pengo atua ofisini kwa Paul Makonda kumfanyia maombi maalumu ya baraka na kumpongeza kwa uteuzi

Kardinali Pengo atua ofisini kwa Paul Makonda kumfanyia maombi maalumu ya baraka na kumpongeza kwa uteuzi

Mkuu wewe ni mtu mwenye upepo mkubwa Sana hapa JF lakini nahisi kuna Vitu huvijui au labda unavijuwa hapa unasherehesha tu.

Kanisa Katoliki lina Siri kubwà, huyo Pengo ni takataka tu hata huko kanisani.

Kitendo cha kuwekewa Askofu muandamizi kwenye Jimbo kuu maana yake Vatican ilicover tu image yake asistaafu Kwa aibu.

Pengo kitendo cha kukana waraka wa maaskofu tayari huyo ni Kafir.

Sijawahi kukubali Gwajima lakini siku Gwajima alipomtolea uvivu huyu Illuminati Pengo nilimuunga mkono Gwajima.

Watu kama Pengo ndio wamesababisha wengine sasa hivi hatuendi kanisani tunasali kwenye TV na kumuomba Mungu nyumbani.
 
Mkuu Nguruvi3 , serikali ndio haina dini ila watu wake wana dini zao, hakuna ubaya wowote, viongozi wowote wa dini, kumuombea, ofisini kwenye ofisi ya umma, and soon utamshuhudia Mufti, Malasusa, na Yuda Thadei Ruwa Ichi!.
P
Sasa mbona Ramadhan Dau aliitwa mdini?

Au tatizo ni Uislamu?

Tukianza kuleta duwa za masheikh kwenye ofisi za umma mtulie hivyohivyo na duwa tamu tutaleta na madufu ya watoto wa madrasa.

Cc: Mohamed Said
 
Hapo ni ushetani mtupu, hakuna kiongozi anatoka kwa Mungu, Mungu ni mtakatifu,
Idi amin, Adolf Hitler, Maghu,musolin, wote walikuwa viongoziviongozi, je wote walitoka kwa Mungu!?
 
Siku moja utakuja kujutia mawazo yako hayo ya kishetani.utawatafuta watumishi wa Mungu na hutawaona. Usilete utani kwenye mambo ya imani na kiroho.
Unadandia vitu husivyovijua, Viongozi wa dini wapo kwa ajili ya kila mtu hasa wadhambi wanawaitaji zaidi.

Wewe umeona issue kubwa Pengo kuonekana akimuombea Makonda.

Sijuhi cha ajabu ni ukadnari wa Pengo au Uaskofu wake?

Kama ni ukadnari waulize watu wa katoliki watakufafanulia kwamba hata brother (buruda) anaweza kuwa kadnari.

Ni sawa tu na Msukuma au Kibajaji kuwa Wabunge
 
1713251371833.png
 
Ndugu zangu Watanzania,


Kilichopatikana kwa Maombi hulindwa kwa Maombi na kilichopatikana kwa uchawi na makafara hulindwa kwa uchawi na makafara yakiambatana na matambiko yasiyo kwisha. Kwa kuwa Mwamba Mwenyewe Makonda amekuwa akipata vyeo na nafasi mbalimbali za uongozi ndani ya serikali na chama kwa njia ya maombi kwa Mwenyezi Mungu na hatimaye kujibiwa ,ndio maana ameendelea kujiweka karibu sana na Mungu,ndio maana ameendelea kujinyenyekeza mbela za Mungu na kumuomba Mungu kuendelea kuwa ndani yake na kumtangulia katika kazi zake.

Ndio maana viongozi mbalimbali wa kidini kutoka madhehebu mbalimbali wameendelea kumiminika ofisini kwake kumuombea na kumpa maneno ya hekima na baraka katika utumishi wake, wa kuwatumikia wana Arusha kwa haki na upendo kwa uweza wa Mwenyezi Mungu Mwenyewe.

Baada ya hapo majuzi Mtumishi wa Mungu Mwamposa kufika Ofisini kwa Mwamba Mwenyewe Makonda kumfanyia maombi na kufanya naye mazungumzo.leo tena kiongozi mwingine na mtumishi wa Mungu aliyewahi kuteuliwa na PAPA kiongozi mkuu wa kanisa katoliki Duniani kuwa Kardinali pekee hapa nchini leo hii ametua kwa kishindo kilichoiteka kanda ya kaskazini.

Huyu ni askofu mstaafu wa jimbo kuu la Dar es salaam Kardinali Pengo.ambapo amefika ofisini kwa kijana wake na kumpongeza sana tena sana na kwa upendo mkubwa kwa heshima kubwa sana aliyoipata ya kuendelea kuaminiwa na Mheshimiwa Rais wetu mpendwa na Jemedari wetu kipenzi cha watanzania Mama Samia Suluhu Hasssan ya kuongoza mkoa wa Arusha. Sanjari na hayo amemfanyia maombi maalumu ya kumuombea baraka na neema katika uongozi wake.ili jiji liendelee kuwa na amani na utulivu.Kardinali Pengo hakuwa peke yake bali aliambatana na viongozi mbalimbali kutoka kila pembe ya nchi yetu tena wa ngazi za juu kabisa alipowasili ofisini hapo.

Ndugu zangu Watanzania nilishawaambieni sana kuwa acheni kushindana na mwamba Makonda.huyu ni mpango wa Mungu,ameinuliwa na Mungu Mwenyewe.mtahangaika na kushindana naye lakini hamtaweza kumshusha kileleni. Mtavaa na kuvalishwa mahiriizii na kutambika ili mumshushe lakini hamtaweza.mtatoa kila aina ya makafara ,kujichanja kila aina ya madawa na kubaki na chale tupu miilini mwenu utafikiri mlidondokea kwenye kiwanda cha nyembe lakini hamtaweza kumshusha Mwamba Makonda kilele.

Huyu Mwamba analindwa na maombi na mkono wa Mungu Mwenyewe.ndio maana mnaona anavyojiamini kwasababu Mungu yupo ndani yake.na Mungu akiwa ndani yako huwezi kuingia gizani maana yeye ni nuru na mwanga usiozimika. Aliyepewa kapewa tu ndugu zangu.sisi wengine tuendelee na kazi tu kwa kadri Mungu alivyo tupangia. ..

Msaidizi na katibu binafsi wa Mheshimiwa Rais Mheshimiwa Waziri Rajabu amewahi kuandika katika mtandao kuwa usishindane na nyakati zinapokuwa kwa mwenzako .lakini pia heshimu nyakati na wakati unapokuwa kwa mwenzako ili nawe uje uheshimiwe wakati utakapo kuwa upande wako kwakuwa nyakati huzunguka..huu ni wakati wa Mhessimiwa Makonda uliopangwa na Mungu mwenyewe kuwatumikia watanzania.tumuache afanye kazi na tuache Majungu ndugu zangu.

Mimi sinaga wivu kumpongeza mtu anayefanya vizuri.ndio maana inafika wakati watu wananiita chawa wa mtu fulani na wengine wakifikia hadi hatua kufikiri kuwa nalipwa.mimi ukifanya vizuri huwa sina hiyana kukupongeza,.ndio maana huwa nampongeza sana Mheshimiwa Rais kwa uchapa kazi wake. Makonda ni mchapa kazi sana ndio maana nampongeza kwa uchapa kazi wake, uzalendo na ubunifu wake katika kutekeleza majukumu yake.

Kazi iendelee, mama Ametufikia na kuwafikia watanzania kwa utumishi wake uliotukuka wa kugusa maisha ya watanzania wanyonge wasio na Sauti.

Lucas Hebel Mwashambwa, Kijana mzalendo na mpenda nchi yangu.

PIA, SOMA:
Huyo Pengo ni bundi hadi useme atua ofisini kwa Makonda?
 
Back
Top Bottom