Ni muda wa kuangalia management companies au raia wa kigeni wenye sifa sahihi na kuwapa kazi za kusimamia taasisi zote za kibiashara zinazomilikiwa na serikali sio bandari tu.
Muhimu ni kuwekeana mikataba ya performance targets.
Juzi Suma JKT imezindua kituo chao mafuta kwa hakiba ya hela zao; kwa sababu hakuna ubadhirifu kama ilivyo kwenye taasisi za serikali.
Kwanini TPDC aina vituo vya mafuta kuwa mshindani ndani ya soko. Moja ya sababu ni kwamba mteja wake mkubwa wa gas hivi sasa ni TANESCO na Dangote. TANESCO toka wameanza kupewa gas na TPDC awajawahi lipa ata centi 5, gas ambayo wanatumia kufanyia biashara na juzi hilo deni la TPDC serikali wamelifuta.
Watu ambao wameshindwa kuwalipa taasisi ambayo inauwazia malighafi wanayozalishia, hapo hapo wameenda kuingia mkataba wa kununua umeme wa jua; kipindi ambacho watakuwa na uzalishaji wa ziada bwawa la Nyerere.
Nimewatolea mfano tu hao TANESCO lakini wote TTCL, ATCL, NHC, TPDC, TRC na ikiwezekana halmashauri kama kuna uwezo wa kuajiri wageni katika nafasi ya wakurugenzi iwe hivyo.
Ifike wakati tuambizane ukweli watanzania hasa wanaoteuliwa na serikali awawezi kazi; unahitajika utaratibu mwingine ukizingatia sector zingine zina multiplier effect kubwa ya uchumi kama bandari.
Serikali isiishie na bandari tu, waende mbele wenyeji awawezi kazi.